Filtrer par genre

SAUTI-SIKIKA

SAUTI-SIKIKA

Jeremiah Paul Wandili

Sauti iliyo ndani yako ina nguvu kuliko sauti nyingi zilizo nje yako. Kubali kusikiliza sauti yako ya ndani. Sauti ya ndani ina nguvu ya kuleta mabadiliko. Ipo nguvu ya ndani katika sauti yako.

10 - Sauti Ya Matumaini-Amos Mwijonge.
0:00 / 0:00
1x
  • 10 - Sauti Ya Matumaini-Amos Mwijonge.

    Usipofuta kibao, huwezi jua kwanini gari la taka linaoshwa hili liweze kubeba taka tena. Maana cha muhimu kwetu sio miaka uliyoishi katika maisha yako, cha muhimu kwetu ni thamani ya maisha yako katika miaka uliyoishi. Kumbuka mito hainywi maji yake na miti haili matunda ya mti wake. Sikiliza sauti ya Amosi.... kumbuka hautakumbukwa kwa ulichojifunza, utakumbukwa kwa ulichofundisa wengine duniani. Fuatilia kazi nzuri za Amosi hapaMaisha ni mchezo wa kupona...... 

    Fri, 12 Jun 2020 - 04min
  • 9 - Sauti Ya Dr Mipango-Waziri wa Fedha na Mipango, Tanzania

    Mh, Waziri Dr. Phillip Mipango, anasikika moja kwa moja kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipaza sauti kulelezea Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2020/21 na hali ya Uchumi wakatika wa Bunge la Bajeti Tarehe 11/06/2020. Je, unajua sekta zenye kuwekewa kipaumbele kwa Mwaka 2020/21 na je, unajua #Covid19 imetikisa Uchumi... sikiliza upate kujua mpango wa Serikali katika kuimarisha Afya, Miundombinu, Elimu na Maendeleo kwa ujumla. 

    Thu, 11 Jun 2020 - 59min
  • 8 - Sauti Ya Joel Nanauka-Lijue Kusudi Lako

    Kila siku unapo amka unapaswa kujiuliza maswali haya; Je, ni maswali gani na kuna sauti gani katika kujiuliza maswali hayo ili uweze kujua kusudi lako. Fuatilia Dakika 3 katika mfululizo wa Sauti Sikika, isikilize Sauti ya Joel Nanauka. Pia unaweza kumfuatilia Joel katika Mitandao ya Kijamii, Instagram; https://www.instagram.com/joelnanauka_/ na Facebook; https://web.facebook.com/jnanauka/ pia katika Channel yake ya Youtube; https://bit.ly/Joel-Nanauka-Youtube  

    Wed, 10 Jun 2020 - 03min
  • 7 - Sauti Ya Theresia- Sauti yake akizungumzia Mabadiliko Chanya wakati wa Covid-19.

    Theresia anasimulia namna ambavyo Covid19 imekuwa ni changamoto chanya kwake. Maana Theresia amechukulia covid19 katika uhalisia wake zaidi yeye alijiepusha kuishi kwa hofu. Anasisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhali na kufuata maelekezo ya wataalamu wa Afya. Amezungumza mengi, ikiwemo swala zima la kujenga mahusiano mazuri na familia, kutumia muda mzuri pia kujiendeleza. Hongera sana Theresia kwa Sauti yako katika Mabadiliko Chanya. Kumbuka unaweza kushare Sauti yako kwa namba +255758044443. 

    Tue, 09 Jun 2020 - 20min
  • 6 - Sauti Ya Mabadiliko

    Unajua, mabadiliko ni mchakato, ni hatua.. lakini je unajua Mabadiliko ni gharama? na ili kufikia mabadiliko lazima ulipe gharama. Podcast hii inakupa nafasi ya kufahamu sauti ya mabadiliko ili uweze kujiandaa kuisikiliza na kulipa gharama katika kufikia mabadiliko. Ahsante sana, karibu. Tuma maoni yako na sauti yako ya Mabadiliko katika namba hii ilisajiliwa Whats App +255758044443 nasi tutashare podcast yako. Ahsante sana, furahi sauti ya mabadiliko.  

    Tue, 09 Jun 2020 - 25min
Afficher plus d'épisodes