Filtra per genere

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu

1062 - Huu ndiyo uhusiano wa Huruma ya Mungu na Manabii.
0:00 / 0:00
1x
  • 1062 - Huu ndiyo uhusiano wa Huruma ya Mungu na Manabii.

    Karibu uungane nami Esther Magai katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera, akitufundisha juu ya huruma yake ni ya milele akijikita zaidi katika Manabii na Huruma ya Mungu.

    Thu, 21 Nov 2024 - 52min
  • 1061 - Je, unafahamu huruma ya Bikira Maria kwa Wanadamu?

    Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, Majibu yanatolewa na Frateri Ayubu Polycarp Mwashibili kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu katoliki Songea, katika Swali hili naomba kueleweshwa juu ya unyenyekevu wa Mama Bikira Maria na Huruma kwa Mama Bikira Maria.

    Thu, 21 Nov 2024 - 23min
  • 1060 - Sikiliza tafakari ya Injili ilivyoandikwa na Luka 19:1-10.

    karibu katika kipindi cha Tafakari Nasi, Mwezeshaji ni Padre John Bosco kutoka Jimbo Kuu la Dar es salaam, leo anatutafakarisha juu ya Injili ya Luka 19:1-10.

    Thu, 21 Nov 2024 - 25min
  • 1059 - Fahamu njia rahisi ya kujisajili na mfuko wa bima ya Taifa (NHIF) kwa Wanafunzi.

    Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Elimu Jamii, Mwezeshaji ni Dkt. Raphael Malaba, Meneja wa Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF) Mkoa wa Kinondoni, akitufundisha juu ya matumizi ya mifumo katika usajili wa Wanafunzi.

    Thu, 21 Nov 2024 - 51min
  • 1058 - Fahamu historia ya Mfalme Herode.

    Karibu katika kipindi cha ujumbe wa Biblia, Mwezeshaji ni Padre Titus, Mtaalamu wa Maandiko Mtakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu la Mwanza akizungumzia juu ya Mfalme Herode.

    Thu, 21 Nov 2024 - 51min
Mostra altri episodi