Filtrar por gênero

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12069 - Vijana wajumuishwe kwenye majadiliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi - Nasra
0:00 / 0:00
1x
  • 12069 - Vijana wajumuishwe kwenye majadiliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi - Nasra

    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania umewajumuisha watoto kwenye harakati za kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Huko Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 tunamsikia Nasra Abdallah, mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania akizungumzia kilichompeleka, anachoondoka nacho na ujumbe wake kwa  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

    Fri, 22 Nov 2024
  • 12068 - Kuna mkwamo kwenye mkutano wa COP29 huku mapendekezo mapya yakitaka nchi tajiri kuzilipa masikini dola bilioni 250 kwa mwaka

    Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea. 

    Hakika vuta nikuvute bado inaendelea hata sasa washiriki wako mezani kwakikuna vichwa na kujadili mapendekezo mapya. Mkwamo huo umetokana na kushindwa kuafikiana katika masuala kadhaa kubwa likiwa ufadhili wa  mabadiliko ya tabianchi na hususasn kuhusu ni kiasi gani cha fedha nchi zinazoendelea zinapaswa kupokea kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 na wapi fedha hizo za ufadhili zitatoka.

    Nchi zinazoendelea zinataka kulipwa dola trilioni 1.3 kwa mwaka lakini hilo halijaafikiwa na mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na raia wa mkataba huo wa UNFCCC yanaonyesha tofauti kubwa na safari ndefu ya kufikia muafaka.

    Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya yaliyowasilishwa leo mezani na Rais wa COP29 Mukhtar Babayev yanataka nchi zinazoendelea kupokea dola bilioni 250 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2035 kwa ajili ya kuchukua hatua didi ya mabadiliko ya tabianchi.

    Na maesema “Fedha hizi zitatoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta za umma na za binafsi, na kitaifa na kimataiifa ikiwemo vyanzo mbadala”.

    Wakati pia COP29 ikitoa wito wa kufikia lengo la ufadhili wa dola trilioni 1.3 ifikapo mwaka 2035 pia imezikaribisha nchi zinazoendelea kutoa michango ya ziada.

    Kiwango kilichopendekezwa cha ufadhili kinatarajiwa kuzusha vuta ni kuvute katika majadiliano hayo kwa siku nzima ya leo huenda hadi kesho ingawa mkutano huo unahisi ahuweni kwamba kuna kiwango kilichowasilishwa na unataka hitimisho la mkutano haraka iwezekanavyo. Je nchi zinazoendelea zitapokea vipi pendekezo hili jawabu bado halijulikani. Wapenzi wa UN News Kiswahili endeleeni kufuatilia kwenye kurasa zetu kufahamu hatma ya mkutano huo.

    Fri, 22 Nov 2024
  • 12067 - 22 NOVEMBA 2024

    Hii leo jaridani tunaangazia majadiliano huko Baku Azerbaijan kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi, na kazi za walinda amani kutoka Tanzania TANZBATT-11 huko DRC. Makala inaturejesha kataika mkutano wa COP29 na mashinani inatupeleka Namibia, kulikoni?

      Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea.Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto.Makala inakupeleka Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 kumsikia kijana kutoka Tanzania akizungumzia kilichompeleka, anachoondoka nacho na ujumbe wake kwa  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, tunasikia kauli ya Willem Westhuizen, mkulima kutoka Namibia, akielezea changamoto zinazotokana na ukame unaoathiri maisha yao kila siku”.  

    Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu! 

    Fri, 22 Nov 2024
  • 12066 - Mafunzo ya walinda amani kutoka Tanzania huko Beni yajengea uwezo walimu kusaidiana na watoto

    Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto. 

    Video ya MONUSCO ikianza na walinda amani wakijongea kwa jamii, Kapteni Noella Nyaisanga kiongozi wa kikundi hicho cha wanawake cha kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania kwenye MONUSCO, TANZBATT-11 anaeleza jinsi kikundi chao kinavyosogea kwa jamii na hasa watoto ili kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi kwenye eneo hili la Beni, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. Anafafanua zaidi lengo lao.

    Lengo ni kujenga uaminifu kwa raia ambao tunawalinda. Kwa hiyo tukaamua kuandaa masomo shuleni, ambayo yataweza kuwaimarisha wao, kuwasaidia tatizo la kuwa wameathirika kisaikolojia.

    Zavadi Mbambu ni miongoni mwa walimu waliopatiwa mafunzo ya kusaidia watoto walioathiriwa na changamoto lukuki ikiwemo mapigano. Akisema stress, anamaanisha msongo.

    “Unakuwa na wanafunzi wanaokuwa na msongo wa mawazo kutokana na jambo ambalo wanaishi, na hata mauaji. Kuna wale ambao hata wameua wazazi wao , hata familia yao yote.  Na kwa hao wanafunzi wanapoingia shuleni , wanakuwa kama hawako ndani, fikra zao zinakuwa mbali .  Lakini kupitia mafunzo nimewaelewa , na tumejua namna gani ya kuishi nao. Na tayari mabadiliko yameanza kuonekana.”

    Pacifique Kyakimwa, mmoja wa wanafunzi anasimulia mkasa mmoja.

    “Kuna mwenzetu  aliyekuwa na tatizo, yaani tukiwa ndani ya shule, alikuwa anacheka, yaani anatusumbua hadi hatumwelewi mwalimu. Lakini tangu wameanza kufundisha hili somo, wameanza kuelewa . Ameanza kuwa na akili inayotumika vizuri. Mafunzo haya yamefika wakati tunahitaji , na imetusaidia sana.”

    Fri, 22 Nov 2024
  • 12065 - Jinsi usawa wa kijinsia na rika katika umiliki wa ardhi unavyochochea ukulima na uhakika wa chakula Kenya

    Mpango wa Usimamizi wa Ardhi (Land Governance program) uliopatiwa jina "Kusaidia kufikia Ajenda 2030 kupitia mageuzi chanya ya ugatuzi wa ardhi (land reforms) katika maeneo ya ardhi za jamii nchini Kenya" umeboresha uhakika wa kupatikana kwa chakula na lishe kupitia upatikanaji wa ardhi kwa wote nchini Kenya. Programu hii imezinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya (EU) katika kaunti 9 ikilenga kuimarisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi na umeimarisha usimamizi wa ardhi kwa ajili ya maisha bora na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika kaunti zote zinazotekeleza. Kupitia video iliyoandaliwa na FAO, Cecily Kariuki anaeleza matokeo yake.

    Mpango wa Usimamizi wa Ardhi (Land Governance program) uuliopatiwa jina "Kusaidia kufikia Ajenda 2030 kupitia mageuzi chanya ya ugatuzi wa ardhi (land reforms) katika maeneo ya ardhi za jamii nchini Kenya" umeboresha uhakika wa kupatikana kwa chakula na lishe kupitia upatikanaji wa ardhi kwa wote nchini Kenya. Programu hii imezinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya (EU) katika kaunti 9 ikilenga kuimarisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi na umeimarisha usimamizi wa ardhi kwa ajili ya maisha bora na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika kaunti zote zinazotekeleza. Kupitia video iliyoandaliwa na FAO, Selina Jerobon anaeleza matokeo yake katika makala hii..…

    Wazee wa jamii za kijiji cha Maiyanat iliyoko katika kaunti ya Turkana kaskazini-magharibi mwa Kenya wanafanya kikao cha pamoja hapa, wakiwa wamevalia mavazi yao ya kitamaduni, watoto wakiwa pembeni wakifuatilia kinachoendelea. Wanajadili matumizi mazuri ya mashamba ya jamii zao kwa kuzingatia usawa wa kijinsia na marika yote.

    Je, awali umiliki wa ardhi ulizingatia usawa huu? Ratinui Macharia ni mwenyekiti wa ardhi ya jamii ya Maiyanat, anasema,

    “Awali, wanawake na vijana hawakuruhusiwa kushiriki au hata kuchaguliwa kwenye kamati ya ardhi lakini sasa imetuleta sote pamoja.”

    Lois Kimere ni mwanamke mwanachama wa kamati ya ardhi Maiyanat.

    “Kulingana na jamii za Maiyanat, wanawake hawakuwa wanaonekana kama watu wenye uwezo wa kuchangia maendeleo ya kijamii. Tulihamasisha wanawake kuhusu mambo ya ardhi, uongozi katika vijijini na katika ngazi za kitaifa hususani serikali, na katika bishara.”

    Kwa msingi wa dharura, awamu ya kwanza na ya majaribio ya mpango huu ilitekelezwa katika kaunti za Laikipia, Nandi, Pokot magharibi, Baringo, Vihiga, Marsabit, Kajiado, Samburu, Tana River na Turkana.

    Asha Lekudere ni mwanachama wa ardhi ya jamii ya sereolipi, anasema FAO imeimarisha mtazamo wao.

    “Zamani tulikuwa na shamba la kikundi. Kisha FAO ikatupeleka kwenye mafunzo kadhaa. Niliweza kujifunza maana ya umiliki wa ardhi kwa jamii yetu ya samburu, uwezo wetu na haki za wanawake.”

    Chini ya ajenda ya ardhi ya jamii, programu iliwezesha mila shirikishi na jumuishi katika usimamizi wa ardhi kwa njia ya usawa wa jinsia na rika zote.

    Na hatua gani zinaweza kuchukuliwa mizozo inapotokea? Mpango wa usimamizi wa ardhi umekuza mfumo mbadala wa mahakama, wa kupigania haki za kibinadamu unaojulikana kama AJS, njia bora ya kusuluhisha kesi mashinani na kuachilia ardhi itumike kwa ajili ya jamii zote haraka iwezekanavyo.

    Jonathan Osewu, Msajili wa ardhi  katika kaunti ya Kajiado anasema,

    “Katika utamaduni wetu wa kimasai tunazo njia nyingi sana za kutatua mizozo. Kwa hivyo AJS ilipoletwa, ilikuwa ni njia bora ya kuimarisha utaratibu wetu wa jadi wa kutatua kesi.”

    Na isitoshe, njia za teknolojia za kutoa ramani ya ardhi na rasilimali yote kwa muonekano wa anga, GIS ili kusaidia kufanya maamuzi ya kesi haraka, pia imechangia utangamano katika jamii husika. Vituo hivi vimetekelezwa katika sehemu nyingi ikiwemo kaunti ya Vihiga. Wilber Ottichilo, Gavana wa mkoa wa Vihiga anatoa shukrani kwa FAO.

    “Kama kaunti ya Vihiga,…

    Thu, 21 Nov 2024
Mostrar mais episódios