Filtrar por gênero
Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
Haki ya Mungu ipo wazi na ni tofauti kabisa na haki za wanadamu. Haki ya Mungu imefunuliwa katika injili ya maji na Roho ambayo ilitimizwa kwa ubatizo wa Yesu toka kwa Yohana na damu yake Msalabani. Tunapaswa kurudi katika imani inayoamini katika haki ya Mungu kabla hatujachelewa. Je, unafahamu ni kwa nini ilimpasa Yesu kubatizwa na Yohana Mbatizaji? Ikiwa Yohana asingelimbatiza Yesu, basi dhambi zetu zingekuwa hazikupitishwa kwa Yesu. Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye mkuu kuliko wanadamu wote, na ule ubatizo ambao alimpatia Yesu ulikuwa ni sharti muhimu la Mungu ili kuweza kuzipitisha dhambi zetu toka kwetu kwenda kwa Yesu. Yesu alibatizwa ili kuzibeba dhambi zote za ulimwengu katika mabega yake, kisha aliimwaga damu yake Msalabani ili kulipa mshahara wa dhambi hizo zote. Mambo haya yote yamebadilisha kikamilifu uelewa wangu wa zamani juu ya kuzaliwa tena upya wakati nilipokuwa nikifahamu juu ya damu ya Msalaba tu. Kwa sasa Mungu ametufundisha juu ya haki ya Mungu jinsi ilivyo ili kwamba tuweze kufahamu na kuamini kikamilifu katika haki yake. Ninamshukuru Bwana kwa baraka hizi zote. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
- 30 - SURA YA 7-1. Utangulizi Kwa Sura ya 7
Kwa kuutambua ukweli kuwa kabla ya ukombozi wake mwili wake ulikuwa umehukumiwa kifo na Sheria ya Mungu, basi ndio maana Mtume Paulo alilifanya ungamo lake kwa kuamini kuwa alikuwa ameifia dhambi katika Yesu Kristo. Kabla hatujakutana na haki ya Mungu—yaani kabla hatujazaliwa upya—sisi ambao tunamwamini Kristo tulizoea kuishi chini ya himaya na laana ya Sheria. Hivyo, ikiwa tusingekutana na Yesu ambaye ametuletea haki ya Mungu basi Sheria ingeendelea kututawala. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 18min - 29 - SURA YA 7-2. Kiini cha Imani ya Paulo: Ungana na Kristo Baada ya Kuifia Dhambi (Warumi 7:1-4)
Je, umewahi kuona bunda la nyuzi zilizojisokota? Ikiwa unajaribu kuifahamu sura hii pasipo kuufahamu ukweli wa ubatizo wa Yesu ambao Mtume Paulo aliuamini, basi ni hakika kuwa imani yako itakuwa katika wakati mgumu kuliko hapo kabla. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 49min - 28 - SURA YA 7-3. Sababu Inayotufanya Tumsifu Bwana (Warumi 7:5-13)
Ninamsifu Bwana ambaye ameniongoza hadi kuonana na ninyi watu wa Mungu kwa mara nyingine tena. Kwa kweli ninamshukuru sana Mungu kwa kunibariki na kunifanya niishi maisha yenye furaha hadi leo hii. Mungu ameendelea kuwa pamoja nami na amekuwa akinihurumia ingawa kulikuwa na nyakati ambazo nilikuwa najisikia kukatishwa tamaa, nyakati ambazo nilikutana na magumu na kupata udhaifu ndani yangu katika vipindi mbalimbali. Mungu amekuwa makini na amekuwa upande wangu katika maisha yangu yote katika shida na katika furaha. Hakukuwa na wakati wowote ambapo Mungu aliniacha hata kwa sekunde moja. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 29min - 27 - SURA YA 7-4. Miili Yetu Ambayo Inautumikia Mwili Tu (Warumi 7:14-25)
Sisi hatuwezi kufanya jambo lolote ikiwa Mungu hatendi kazi akiwa upande wetu. Mungu wetu anatutunza na anatusaidia. Hebu tuliangalie Neno la Mungu. Warumi 7:14-25 inatueleza sisi kuwa Mtume Paulo alijiona yeye mwenyewe kuwa anaishi katika mwili hali akiwa ameuzwa chini ya dhambi. Pia aligundua kuwa kwa sababu ya sheria mwili hauwezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kufanya dhambi muda wote atakapokuwa hai. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 32min - 26 - SURA YA 7-5. Mwili Unaitumikia Sheria ya Dhambi (Warumi 7:24-25)
Biblia inatueleza sisi pia kuwa, “kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.” Na hizo ndio sheria zinazotutawala. Mioyo yetu imeumbwa kumpenda Mungu na kuupenda ukweli, lakini ni kawaida kwa mwili kuitumikia sheria ya dhambi. Neno la Mungu linatueleza sisi kuwa moyo unaitumikia injili na haki ya Mungu ilhali mwili unaitumikia dhambi tu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 38min - 25 - SURA YA 7-6. Tumsifu Bwana, Mwokozi wa Wenye Dhambi (Warumi 7:14-8:2)
Wanadamu wote walirithi dhambi toka kwa Adamu na Hawa na wakafanyika kuwa mbegu ya dhambi. Hivyo sisi ni viumbe wenye dhambi. Kwa asili tunazaliwa kama uzao wa dhambi na hivyo tunajikuta ni viumbe wenye dhambi. Watu wote duniani hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kuwa wenye dhambi kwa sababu ya baba yetu wa kwanza Adamu ingawa hakuna yeyote anayetaka kuwa mwenye dhambi. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 45min - 24 - SURA YA 8-1. Utangulizi Kwa Sura ya 8
Pengine sura ya 8 inaweza kuelezewa kuwa ni sura muhimu sana miongoni mwa sura kadhaa za kitabu hiki cha Warumi. Paulo anatufunulia jinsi ambavyo haki ya Mungu ilivyo ya kushangaza kwa kupitia mada mbalimbali ambazo zinapatikana katika kitabu hiki. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 06min - 23 - SURA YA 8-2. Haki ya Mungu, Utimilifu wa Hitaji la Sheria Kwa Mwenye Haki (Warumi 8:1-4)
Warumi 8:1-4 inatueleza sisi juu ya aina ya imani ambayo wale walio katika Kristo wanayo. Siri ya kifungu hiki ni kwamba tunaweza kukutana na maagizo yote ya Sheria katika haki ya Mungu kwa imani yetu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 33min - 22 - SURA YA 8-3. Mkristo ni Nani? (Warumi 8:9-11)
Ikiwa mtu ni Mkristo wa kweli au la mtu huyo anatofautishwa kwa kigezo ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yake au la. Inawezakanaje kwa mtu kuwa Mkristo ikiwa mtu huyo hana Roho Mtakatifu katika moyo wake? Paulo anatueleza sisi kuwa hata kama tunamwamini Yesu hilo sio suala muhimu sana bali ikiwa tunamwamini Yesu hali tukiwa tumeigundua haki ya Mungu au la. Imani ya kweli inayohitajika kwa watakatifu ni ile imani ambayo iko tayari kupokea na kufanywa makao ya Roho Mtakatifu. Uwepo wa Roho Mtakatifu ndio unaoweza kukutambulisha ikiwa wewe ni Mkristo au la. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 04min - 21 - SURA YA 8-4. Kuwa na Mawazo ya Kimwili ni Kifo, Bali Kuwa na Mawazo ya Kiroho ni Uzima na Amani (Warumi 8:4-11)
Watu wamekuwa wakiteseka kwa karne tano zilizopita hali wakidanganywa na mafundisho potofu ya kiimani kama vile Fundisho la Utakatifu Unaozidi, Fundisho la Kuhesabiwa Haki kwa Imani, na mafundisho mengine ambayo yanasisitiza kuwa ukombozi unawezekana kwa kupitia sala za toba. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 32min - 20 - SURA YA 8-5. Kutembea Katika Haki ya Mungu (Warumi 8:12-16)
Mtume Paulo, kama mtu aliyepokea wokovu toka kwa Mungu alisema kuwa wale waliozaliwa tena upya hawapaswi kuishi kwa jinsi ya mwili bali kwa jinsi ya Roho. Hasahasa Paulo alisema kuwa ikiwa sisi ambao tunayo haki ya Mungu tutaishi kwa jinsi ya mwili basi tutakufa, na kwamba kama tutaishi kwa jinsi ya Roho basi tutaishi. Hivyo ni lazima tuamini katika ukweli huu. Je, inakuwaje basi kwa wale wanaoamini katika haki ya Mungu? Je, wanapaswa kuishi kwa mujibu wa haki ya Mungu au kwa tamaa ya mwili? Ni lazima watambue kile kilicho sahihi na kisha waiadabishe miili yao ili kujitoa kwa kazi za haki ya Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 08min - 19 - SURA YA 8-6. Wale Waurithio Ufalme wa Mungu (Warumi 8:16-27)
Watu wote ambao wamesamehewa dhambi zao wanaamini katika injili ya maji na Roho na wana Roho Mtakatifu katika mioyo yao. Katika 1 Yohana 5:10 Biblia inasema, “Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake”. Yeye aliye na haki ya Mungu katika moyo wake anaye huyo Roho Mtakatifu ndani yake, na ni imani katika injili ya maji na Roho inayomfanya Roho Mtakatifu aweze kukaa milele katika moyo wa mtu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 45min - 18 - SURA YA 8-7. Kuja Kwa Bwana Mara ya Pili na Ufalme wa Milenia (Warumi 8:18-25)
Wale ambao ni wenye haki kwa kuamini katika haki ya Mungu basi hao wameupokea utukufu wa mbinguni. Hii ndiyo sababu wanateseka pamoja na injili ya maji na Roho ya Yesu ili kuwavika watu wote kwa utukufu huo wa mbinguni. Waamini wanajitoa wao wenyewe kwa injili ya haki ya Mungu na kisha wanateseka hapa duniani kwa sababu kushiriki katika mateso ya Kristo ni utukufu na haki. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 16min - 17 - SURA YA 8-8. Roho Mtakatifu Anayewasaidia Wenye Haki (Warumi 8:26-28)
Roho Mtakatifu yumo katika mioyo ya wale wanaoamini katika haki ya Mungu. Roho Mtakatifu anawafanya wao kuomba na anawasaidia kufanya hivyo. Pia Roho Mtakatifu huugua kwa kufanya maombi kwa niaba yao kusikoweza kutamkwa. Hii ina maanisha kuwa Roho Mtakatifu anawasaidia kuomba kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Hii ndiyo sababu wale wanaoamini katika haki ya Mungu wanaitwa wana wa Mungu. Bwana anawaahidia wao kuwa atakuwa pamoja nao wakati wote hadi mwisho wa dahari. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 03min - 16 - SURA YA 8-9. Vitu Vyote Vinafanya Kazi Pamoja Kwa Ajili ya Mema (Warumi 8:28-30)
Leo, hebu tukiangalie kifungu hicho hapo juu kinachotoka katika Warumi sura ya 8. Kifungu kinasema kuwa Mungu alituchagua tangu asili, alituita, na akatutukuza sisi tulio katika Yesu Kristo Mwana wa Mungu. Tutazungumzia juu ya hili na jinsi watu wanavyolielewa Fundisho la Utakazo Unaozidi. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 35min - 15 - SURA YA 8-10. Mafundisho ya Kidini Yenye Makosa (Warumi 8:29-30)
Vifungu hivyo vinatueleza sisi kuwa Mungu alichagua tangu asili ili kuwaokoa watu katika Yesu Kristo. Ili kufanya hivyo, Mungu amewaita wao katika Kristo, amewahesabia haki wale aliowaita, na amewatukuza wale aliowahesabia haki. Misingi yote ya maandiko imepangwa na kutekelezwa kwa kupitia Yesu Kristo. Hivi ndivyo kitabu cha Warumi kinavyotueleza, lakini wanatheolojia wengi na watumishi wa uongo wameubadilisha ukweli huu ulio wa wazi kuwa katika fundisho la kawaida la dini hali likiwa na mawazo na matakwa yao binafsi na wanalieneza fundisho hilo kwa nguvu. Sasa tunageukia kuchunguza jinsi watu wengi wanavyouelewa vibaya ukweli huu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 30min - 14 - SURA YA 8-11. Upendo wa Milele (Warumi 8:31-34)
Ikiwa Mungu alikwisha amua kutufunika sisi kwa haki yake katika Yesu Kristo hata kabla ya uumbaji, basi hakuna mtu anayeweza kusumbua na kuharibu mpango huo. Kwa kuamini katika haki ya Mungu, na wala si kwa kupitia katika Fundisho la Kuhesabiwa Haki kwa Imani, basi wale ambao wamekuwa hawana dhambi kiuhakika ndio watoto wa kweli wa Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 05min - 13 - SURA YA 8-12. Ni Nani Anayeweza Kudiriki Kusimama Kinyume Nasi? (Warumi 8:31-34)
Katika Warumi 8:31-34, Paulo anashuhudia juu ya upendo wa Kristo usioweza kutenganishwa na waamini kwa kufanya majumlisho ya injili ya maji na Roho na kisha kufikia hitimisho lake la mwisho. Kifungu hiki kinaelezea furaha kuu ya wokovu ambayo imefikiwa katika kiwango cha juu cha imani. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 37min - 12 - SURA YA 8-13. Ni Nani Atakayewatenga Wenye Haki na Upendo wa Kristo? (Warumi 8:35-39)
Aya ya 35 inasema, “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?” Ni nani anayeweza kututenga na upendo wa Kristo uliotolewa kwa wale wanaoamini katika injili ya maji na Roho ambayo ina haki ya Mungu ndani yake? Je, mateso na matatizo vinaweza kutukata toka katika upendo huo? Je, yale mapigo makuu ya miaka saba yanaweza kututenga na upendo huo wa Yesu? Kwa kweli hapana! https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 36min - 11 - SURA YA 9-1. Utangulizi Kwa Sura ya 9
Kwa nini Paulo alisema kuwa anahuzuni sana na uchungu unaoendelea katika moyo wake kwa ajili ya watu wake? Ni kwa sababu Paulo alikuwa ana kitu anachokitaka kwa ajili ya ndugu zake, na ndio maana alikuwa radhi kulaaniwa na kukatwa toka katika Kristo kwa ajili yao. Kwa mujibu wa mwili wake, Paulo alipenda sana kwamba watu wake waweze kuokolewa. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 32min - 10 - SURA YA 9-2. Ni Lazima Tufahamu Kuwa Kuchaguliwa Tangu Asili Kulipangwa Ndani ya Haki ya Mungu (Warumi 9:9-33)
Hebu sasa tuweke umakini wetu juu ‘kuchaguliwa tangu asili kulikopangwa na Mungu”. Ili kuelewa kiusahihi juu ya maana ya kuchaguliwa tangu asili, basi tunapaswa kulizingatia Neno la Mungu lililoandikwa, na kisha tukajisahihisha sisi wenyewe ikiwa kuna kitu kibaya katika imani zetu. Katika hili, tunapaswa kwanza kutambua kuwa ni kwa nini Mungu alimpenda Yakobo huku akimchukia Esau. Pia tunahitaji kuchunguza ikiwa uelewa wa Ukristo wa sasa juu ya kuchaguliwa tangu asili kama haujatoka nje ya Maandiko. Sisi sote ni lazima tuwe na uelewa sahihi wa kuchaguliwa tangu asili kulikopangwa na Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 36min - 9 - SURA YA 9-3. Je, Ni Makosa Kwa Mungu Kumpenda Yakobo? (Warumi 9:30-33)
Katika kutuita sisi sote Bwana wetu alisema, “Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi” (Mathayo 9:13). Ni lazima tutambue kuwa karama ya wokovu hairuhusiwi kwa wale wanaoifuata haki yao wenyewe, ili kuepuka hali hii tunapaswa kuamini katika haki ya Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 28min - 8 - SURA YA 10-1. Utangulizi Kwa Sura ya 10
Je, kuna watu ambao wanaifuata haki yao wenyewe huku wakiwa wanaiamini injili ya maji na Roho? Maandiko yanasema kuwa watu wa jinsi hiyo wasioiamini haki ya Mungu na badala yake wanaifuata haki yao wenyewe wanasimama kinyume na Mungu. Watu hawa watafanya nini? https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 39min - 7 - SURA YA 10-2. Imani ya Kweli Huja Kwa Kusikia (Warumi 10:16-21)
Aya ya 17 inasema, “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” Je, imani inayomwokoa mtu katika dhambi zake zote inatoka wapi? Imani ya kweli inakuja kwa kulisikia Neno la Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 34min - 6 - SURA YA 11-1. Je, Waisraeli Wataokolewa?
Warumi 11:1 inasema, “Basi, nauliza, Je! Mungu aliwasukumia mbali watu wake? Hasha! Kwa kuwa mimi nami ni Mwisraeli, mmoja wa wazao wa Ibrahimu, mtu wa kabila la Benyamini.” Kwa maneno mengine, Mungu hakuwaacha Wasraeli kwa kuwa hata Paulo mwenyewe alikuwa ni Mwisraeli. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 15min - 5 - SURA YA 12-1. Zifanye Upya Akili Zako Mbele za Mungu
“Ibada yenye maana” ni kitu gani? Imetafsiriwa kama “tendo la kiroho la ibada” katika Biblia ya Kiingereza ya (NIV), imetafsiriwa kama ambayo tunapaswa kumpatia Mungu. Kumpatia Mungu ibada yenye maana kuna maanisha ni kuitoa miili yetu kwa Mungu katika kuifanya kazi yake ya haki. Kwa kuwa tumeokolewa, basi tunahitaji kuitoa miili yetu na kukubaliwa na Mungu katika kuieneza injili ya haki. Ibada yenye maana ambayo tunapaswa kumpatia Mungu ni kuitoa miili yetu katika utakatifu na kumpatia Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 28min - 4 - SURA YA 13-1. Ishi Kwa Ajili ya Haki ya Mungu
Ni lazima tuishi katika mipaka ya desturi za kijamii. Mungu alituamuru kuwaogopa na kuwaheshimu wale walio na mamlaka katika maisha yetu yote ya kimwili na kiroho. Mungu anatoa mamlaka kwa maofisa wa serikali kwa sababu maalumu na kwa hiyo hatupaswi kuwadharau. Ni lazima tuukumbuke msemo wa Paulo akisema, “Msiwiwe na mtu cho chote isipokuwa kupendana” (Warumi 13:8). https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 11min - 3 - SURA YA 14-1. Msihukumiane
Paulo aliwaonya watakatifu huko Rumi kwamba wasihukumiane wala kubishania imani za wao kwa wao. Kwa wakati huo, kwa kuwa kulikuwa na watu ambao walikuwa ni waaminifu sana na wale ambao hawakuwa waaminifu sana katika kanisa la Rumi, basi hali hiyo ilisababisha kulaumiana na kubishania imani kati ya wao kwa wao. Ikiwa jambo hili litatokea kwako basi unapaswa kuheshimu imani ya mtu mwingine na jitahidi kuepuka mabishano yoyote na watumishi wa Mungu. Kwa kweli suala la kuwainua na kuwajenga watumishi wake si kazi yetu bali ni kazi ya Mungu mwenyewe. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 18min - 2 - SURA YA 15-1. Hebu Tuihubiri Injili Katika Ulimwengu Wote
Wale wanaoamini katika haki ya Mungu hawapaswi kuitafuta hai yao wenyewe kwa kuwa Yesu Kristo hakuitafuta haki yake mwenyewe. Wenye haki wanaishi kwa ajili ya Ufalme wa Mungu na wanaihubiri injili kwa ajili ya mema ya wengine. Paulo alisema kuwa wenye nguvu wanapaswa kubeba mapungufu ya wadhaifu badala ya kujipendeza wao wenyewe. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 21min - 1 - SURA YA 16-1. Salimianeni
Katika utangulizi wake, Mtume Paulo aliwaambia watakatifu waliokuwapo Roma na kwetu sisi kwamba tunapaswa kusalimiana. Je, ni nani tunayeweza kumsalimia kwa moyo wote katika Bwana katika kipindi hiki? Kwa kweli tunaweza kuwasalimia watumishi kwa furaha na waamini wanaolihubiri Neno la Mungu katika ulimwengu mzima. Tunaweza kuwa na ushirika na wale waliookoka kwa kuvisoma vitabu vya injili ya maji na Roho. Sisi pia tuna makanisa, waamini, na watumishi wa Mungu ambao tunaweza kusalimiana nao katika Kristo. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Fri, 13 Jan 2023 - 23min
Podcasts semelhantes a Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (II)
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Espacio en blanco Radio Nacional
- Les Grosses Têtes RTL
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR