Podcasts by Category
Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu
- 580 - Fahamu njia za kupinga ukatili dhidi ya Wazee.
Karibu ungane nami Mtangazaji wako Ester Magai Hangu, katika kipindi cha Elimu Jamii, Studio nipo na Bi. Millen Makundi, Mratibu wa dawati la Wazee Halmashauri ya jiji la Dar es salaam, leo anatufundisha kupinga ukatili dhidi ya Wazee.
Fri, 31 May 2024 - 579 - Je, wazifahamu aina nzuri za malezi ya vijana katika Familia?
Ungana na Ester Magai Hangu, katika kipindi cha Malezi na makuzi ya Vijana, Mwezeshaji ni Sister Theresia Karugaba kutoka Ofisi za haki za Binadamu kitengo cha maendeleo ya jamii, Jimbo Katoliki Zanzibar, leo anazungumzia aina za malezi.
Fri, 31 May 2024 - 578 - Je, kuna utofauti wa sala kati ya Majimbo ya kusini na Majimbo mengine ya Tanzania?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, tukiungana na Frateri Petro Mikao, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, akijibu swali lililoulizwa na Msikilizaji wetu likisema, kwanini kuna utofauti katika baadhi ya sala kama vile sala za asubuhi na sala za jioni katika Majimbo ya kusini chini ya Jimbo Kuu la […]
Fri, 31 May 2024 - 577 - Amka na Mama kipindi cha kawaida cha mwaka [sehemu ya kumi na tisa]
ungana nami Martin Joseph, katika kipindi cha Amka na Mama, ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali zikituamsha na kutuongoza katika siku yetu mpya, karibu tumuimbie Bwana katika roho na kweli.
Fri, 31 May 2024 - 576 - Ifahamu historia ya Nabii Ezekieli.
Karibu katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Mwezeshaji ni Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu la Mwanza, akielezea historia ya Nabii Ezekieli.
Fri, 31 May 2024 - 575 - Ni kwa namna gani utandawazi unatumika katika uinjilishaji?
Karibu katika kipindi cha Fahamu wito wako, Mwezeshaji ni Padre Innocent Bahati Mushi kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, Jimbo Kuu la Arusha, anaendelea kutufundisha juu ya uhusiano wa utandawazi na uinjilishaji. Mtangazaji wako ni Martin Joseph.
Fri, 31 May 2024 - 574 - Je, ni vigezo gani vinatumika kumchagua Katekista?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, leo Frateri Petro Mikao anajibu swali linalosema nini maana ya Katekista na vigezo gani vinatumika kumchagua Katekista
Fri, 31 May 2024 - 573 - Je, miujiza ya Ekaristi Takatifu inaadhimishwaje?
Karibu ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera na Paroko wa Parokia ya Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba, anatufundisha nguvu ya Ekaristi Takatifu katika maisha ya Mkristo.
Fri, 31 May 2024 - 572 - Amka na Mama kipindi cha kawaida cha mwaka [Sehemu ya kumi na nane]
ungana nami Martin Joseph, katika kipindi cha Amka na Mama, ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali zikituamsha na kutuongoza katika siku yetu mpya, karibu tumuimbie Bwana katika roho na kweli.
Fri, 31 May 2024 - 571 - Amka na Mama cha kawaida cha mwaka[ Sehemu ya kumi na saba]
ungana nami Martin Joseph, katika kipindi cha Amka na Mama, ikiwa ni mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali zikituamsha na kutuongoza katika siku yetu mpya, karibu tumuimbie Bwana katika roho na kweli.
Fri, 31 May 2024 - 570 - Je, Waamini, Kanisa na taasisi zake zifanye nini kwa wasioheshimu, kuthamini na kutunza uhai.
ungana na John Samky katika kipindi cha Familia bora na nyumba aminifu, Studio nipo na Paschal Maziku, Federika Bayaga, Katekista Vicent Nathanael na Respicius Mwombeki, Wakufunzi wa familia bora katika nyumba aminifu, wanaelezea mada ya je, Waamini, Kanisa na taasisi zake zifanye nini kwa wanaoendeleza utamaduni wa kifo kwa kutoheshimu utu, kutunza na kutothamini uhai?
Wed, 29 May 2024 - 569 - Fahamu utofauti wa Sakramenti na Visakramenti.
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, leo Frateri Hugo Venance Kabogo anajibu swali ni nini tofauti ya Sakramenti na Visakramenti?
Wed, 29 May 2024 - 568 - Fahamu maana ya kupalizwa Bikira Maria mbinguni.
Karibu usikilize kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, leo Frateri Franco Abel Ubamba kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, anajibu swali liliulizwa je, kupalizwa Bikira Maria Mbinguni maana yake nini?
Wed, 29 May 2024 - 567 - Kwanini vitendo vya utoaji mimba vinashamiri katika jamii?
Ungana na Mtangazaji Agatha Kisimba, katika kipindi cha Pro life utetezi wa uhai, leo Wakufunzi wetu kutoka Pro life Tanzania, Antony Lihepa, Janeth Akarro na Witness Joachim, wanatuelimisha juu ya sababu za kushamiri kwa vitendo vya utoaji mimba.
Wed, 29 May 2024 - 566 - Ifahamu sheria ya Ekaristi Takatifu namba 906-916.
Karibu ungane na Raymond Karega, katika kipindi cha Sheria za Kanisa, Mwezeshaji ni Padre Ladislaus Mgaya, Mwanasheria wa sheria za kanisa kutoka Jimbo Katoliki Njombe, akituongoza katika muendelezo wa mada ya sheria za Ekaristi Takatifu na akijikita zaidi katika sheria namba 906 – 916.
Wed, 29 May 2024 - 565 - Fahamu ujumbe wa Baba Mtakatifu Fransisko kwa siku ya Watoto ulimwenguni.
Karibu ungane na Happiness Mlewa katika kipindi maalumu, ambapo Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa matangazo Radio Maria Tanzania, anazungumzia ujumbe wa Baba Mtakatifu Fransisko juu ya siku ya Watoto ulimwenguni.
Wed, 29 May 2024 - 564 - Ifahamu nguvu ya Ekaristi Takatifu katika Maisha ya Mkrsito.
Karibu Ungane nami Agatha Kisimba, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera na Paroko wa Parokia ya Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba, akituelimisha juu ya nguvu ya Ekaristi Takatifu katika maisha ya Mkristo.
Wed, 29 May 2024 - 563 - Amka na Mama [Sehemu ya kumi na sita]
L'articolo Amka na Mama [Sehemu ya kumi na sita] proviene da Radio Maria.
Wed, 29 May 2024 - 562 - Je, Wafahamu juu ya fumbo la Ekaristi Takatifu na Uinjilishaji?
Ungana na Esther Magai Hangu, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi studio tupo na Padre Padre Deodatus Kagashe Katunzi Mkurugenzi wa Radio Mbiu kutoka Kagera , ambapo leo tunaangazia ni, Ekaristi na Unjilishaji ?
Wed, 29 May 2024 - 561 - Fahamu namna kumlinda Mtoto na kumpatia haki zake za msingi.
Karibu Ungane na Esther Magai Hangu katika Kipindi cha Elimu Jamii, mwezeshaji Bwana Anetus Asingizibwe Mwenyekiti wa Kampeni ya kupinga ukatili shujaa na Maendeleo Simaujata kutoka Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, mada Usalama wa Watoto kwa Maendeleo ya Taifa.
Wed, 29 May 2024 - 560 - Fahamu faida ya kuanzisha Jumuhia ndogondogo katika Kanisa na kuelekea Maadhimisho ya Miaka 50.
Karibu uungane na Mtangazaji Elizabeth Masanja katika kipindi cha Utume wa Walei, Mwezeshaji Damiani Ndimbo pamoja Varerian Mushi Wajumbe wa kamati ya Uinjilishaji Jimbo kuu la Dar es Salaam. Mada Jumuhia ndogondogo kuelekea maadhimisho miaka ya 50 tangua kuanzisha kwake .
Wed, 29 May 2024 - 559 - Mfahamu kwakina juu ya Nabii Isaya katika Bibilia Takatifu.
Karibu usikilize Kipindi cha Ujumbe wa Biblia na Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Jimbo Kuu la Mwanza, ambapo katika kipindi hiki anaendelea kufafanua juu ya Ofisi ya Yesu na Mgawanyo wake Mfahamu kwa kina juu ya Nabii Isaya katika Bibilia .
Wed, 29 May 2024 - 558 - Fahamu kwanini watu wanakatazwa kuacha kutenda dhambi?
Karibu ungane na Frateri Abeli Lubamba kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Agustino Peramiho-Jimbo kuu la Songea, katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, na leo anajibu swali linalo hoji nini maana ya dhambi.
Wed, 29 May 2024 - 557 - Je, Wafahamu kwanini wale Mitume kumi na 12 wa Yesu kati yao hakukuwa hata na Mwanawake?
Karibu ungane na Frateri Julian alfonce Kibungu kutoka Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu Igagulo, Jimbo katoliki la Mafinga , katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, anadavua juu ya swali linalo hoji kwanini Mitume wa Yesu hakukuwa hata Mwanawake bali walikuwa waume tu.
Wed, 29 May 2024 - 556 - Fahamu madhara ya matumizi haramu ya madawa ya kulevya kwa Vijana.
Karibu katika uungane na Happiness Mlewa katika kipindi cha Uraibu, mwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha, kutoka Jimbo Katoliki Moshi, leo anatuongoza katika mada ya Uraibu wa madawa, akijikita zaidi katika madhara ya matumizi haramu ya madawa ya kulevya kwa vijana katika jamii.
Fri, 24 May 2024 - 555 - Je, wafahamu Umuhimu wa kubatizwa katika Roho Mtakatifu?
ungana na Askofu Mkuu Mstaafu Josaphat Louis Lebulu wa Jimbo Katoliki Arusha, katika kipindi cha Roho Mtakatifu na Kanisa ambapo leo tunajifunza Roho Mtakatifu ni Msaidizi wa Baba Mtakatifu.
Fri, 24 May 2024 - 554 - Ni, kwa namna gani Tumtumikie Mungu kwa Upendo?
ungana na Bi Rose Gerald Katibu Kamati ya Uinjilishaji Jimbo kuu la Dares saalam, katika kipindi cha Utume wa walei ambacho hukujuia Mubashara kila siku ya Ijumaa saa nane mchana na kurudiwa siku ya Alhamisi saa nne kamili usiku, mada ni Roho mtakatifu ni Upendo Tumtumikie Mungu kwa Upendo.
Fri, 24 May 2024 - 553 - Je, Kifo ni adhabu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Maurus Msigwa, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Mwanadamu hufa, je kifo ni adhabu?na je mbona mtu akitambua makosa yake akaona anastahili kufa, kwanini huwa hafi?
Fri, 24 May 2024 - 552 - Je, wafahama umuhimu wa Dhamana?
Ungana na Mtangazaji Elizabeth Masanja katika kipindi cha Ijue Sheria mada inayo zungumziwa ni juu ya Suala dhima la dhamana, Mwezeshaji ni Mh Rehema Mayagilo Hakimu Mkazi wa Mahakama Kuu kanda ya Iringa.
Wed, 22 May 2024 - 551 - Askofu Ludovick Joseph Minde. “Palipo na Sala kuna Roho Mtakatifu “
Karibu katika kipindi cha Nena nami Bwana ambapo anayenena nasi ni Mhashamu Ludovick Joseph Minde ALCP/OSS, Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi.
Wed, 22 May 2024 - 57min - 550 - Je, ni halali kurudia Ubatizo ?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Novati Mtapanya, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema je ni halali kurudia ubatizo ikiwa cheti cha ubatizo kipo mbali na mahali unapoishi na kwanini tunarudia ubatizo ikiwa cheti cha ubatizo kipo mbali na mahali tunapotakiwa kupata […]
Wed, 22 May 2024 - 549 - Ni, haki zipi Abiria anapaswa azingatie pindi yupo Barabarani?
Ungana nami Happiness Mlewa Katika Kipindi cha Usalama wa Barabarani, mada inayozungumziwa Haki na wajibu wa Abiria, Wawezeshaji ni kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, Mkaguzi wa Polisi Dumu Mwalugenge, Staff Sajenti Olele Chuwa koplo Abdaah Ismail.
Wed, 22 May 2024 - 51min - 548 - Ni, kwanini Dunia inadhimisha siku ya Uchangiaji Damu Tarehe 14 mwezi sita wa kila Mwaka.
Kuelekea siku ya Uchangiaji Damu Duniani tarehe 14 mwezi wa sita kila mwaka, karibu ungane na Bi Mariam Juma, Afisa Mhamasishaji Jamii kutoka Mpango wa Taifa Damu Salama katika kipindi cha Elimu Jamii,anatuelezea kuhusu Umuhimu wa uchangiaji Damu.
Wed, 22 May 2024 - 49min - 547 - Fahamu thamani ya Matunda ya Roho Mtakatifu kwa Mkristo mbatizwa.
Ungana na Fredy William katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi studio tupo na Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo ya Radio Maria Tanzania, ambapo ni muendelezo wa mada Matunda ya Roho Mtakatifu.
Wed, 22 May 2024 - 53min - 546 - Ni, Kwa namna gani Matunda ya Roho Mtakatifu yanashiriki kuinjilishi kwa haraka?
Ni dakika 55 ya Katekisimu Katoliki Shirikishi studio tupo na Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo ya Radio Maria Tanzania, ambapo leo tunaangazia Matunda ya Roho Mtakatifu.
Wed, 22 May 2024 - 50min - 545 - Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya kumi na tano]
L'articolo Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya kumi na tano] proviene da Radio Maria.
Wed, 22 May 2024 - 49min - 544 - Je, Ibrahimu alifanya makosa na alitubu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Julian Alfons Kidungu, Kutoka Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu Mdabulo Jimbo Katoliki Mafinga, swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Ibrahimu alipozaa na kijakazi baada ya kushauriwa na Sara Mkwee alipona hapati Mtoto. Je, Ibrahimu alifanya makosa? Kama alifanya makosa mbona katika Bibilia […]
Mon, 20 May 2024 - 25min - 543 - Je, Skapulari ni alama gani katika Kanisa Katoliki?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Ayubu Polycarp Mwashibili, kutoka Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji Makongolosi, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema nini maana ya Skapulari?
Mon, 20 May 2024 - 24min - 542 - Fahamu madhara ya vidhibiti mimba.
Ni kwa mara nyingine ninakualika katika kipindi cha Pro – Life utetezi wa uhai, ambapo leo tutajikita kuangazia hitimisho la mada ya vidhibiti mimba.
Fri, 17 May 2024 - 49min - 541 - Je, waufahamu waraka wa kitume wa Baba Mtakatifu Yohane Paulo II, heshima kwa wanawake?
Karibu katika Kipindi cha Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican, Mwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha wa Jimbo Katoliki Moshi, mada anayotufundisha siku ya leo ni Waraka wa Kitume wa Baba Mtakatifu Yohane Paulo II heshima kwa wanawake.
Fri, 17 May 2024 - 56min - 540 - Ufahamu uhusiano wa Sakramenti ya Daraja Takatifu ya Upadre na historia ya Nabii Isaya.
Karibu usikilize Kipindi cha Ujumbe wa Biblia na Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Jimbo Kuu la Mwanza, ambapo katika kipindi hiki anaendelea kufafanua juu ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ya Upadre, akijikita zaidi katika historia ya Nabii Isaya.
Fri, 17 May 2024 - 56min - 539 - Je, kuna umuhimu gani wa kusindika vyakula?
Karibu katika kipindi cha Chakula na Lishe, leo tupo na Bi. Maria Ngilisho, Afisa lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), leo akituongoza katika kujifunza Umuhimu wa kusindika Vyakula. Mtangazaji wako ni mimi Ester Magai Hangu jumuika nasi hadi tamati.
Fri, 17 May 2024 - 51min - 538 - Je, wafahamu faida ya mazoezi katika Mwili wa Binadamu?
Ungana na Mtangazaji Agatha Kisimba katika kipindi cha Chakula na Lishe,leo tukiwa naye Mwezeshaji Bi. Maria Ngilisho, Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), mada tunayoiangazi ni Lishe na kuushughulisha Mwili.
Fri, 17 May 2024 - 48min - 537 - Fahamu wajibu wa Wazazi na Walezi juu ya Uraibu wa Mitandao kwa Watoto.
Karibu Ungane na Mtangazaji Happiness Mlewa, katika kipindi cha Uraibu na Padri Richard Matanda Tesha kutoka Jimbo Katoliki Moshi, leo tunaangazia Wajibu wa Wazazi na Walezi juu ya Uraibu wa Mitandao kwa Watoto.
Fri, 17 May 2024 - 536 - Je, wafahamu umuhimu wa Methali katika Jamii?
Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha Elimu Jamii leo tupo na Msanifu Lugha, Kusanja Emmanuel Kusanja, kutoka Baraza la Kiswahili Taifa [BAKITA] mada ni Umuhimu wa Methali katika Jamii.
Fri, 17 May 2024 - 52min - 535 - Fahamu zaidi kuhusu Uinjilishaji wa haraka na Utandawazi.
Ungana nami Martin Joseph, katika kipindi cha Fahamu wito wako kinachoandaliwa na Padre Innocent Bahati Mushi, kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela Jimbo kuu la Arusha ambapo ni muendelezo wa mada ya Utandawazi.
Fri, 17 May 2024 - 58min - 534 - Ni, kwa namna gani Moyo Mtakatifu wa Yesu unainjilisha kwa haraka?
Ungana na Erick Paschal, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi studio tupo na Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo ya Radio Maria Tanzania, ambapo leo tunaangazia ni, kwa namna gani Moyo Mtakatifu wa Yesu unainjilisha kwa haraka?
Fri, 17 May 2024 - 53min - 533 - Je, Karismatiki Katoliki haikubaliki ndani ya Kanisa ?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Daudi Fungameza, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kikundi cha Karismatiki Katoliki kilianzishwa na nani? na kwanini Kikundi hicho kinaonekana kama hakikubaliki ndani ya Kanisa?
Fri, 17 May 2024 - 22min - 532 - Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya kumi na nne]
L'articolo Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya kumi na nne] proviene da Radio Maria.
Fri, 17 May 2024 - 49min - 531 - Fahamu utofauti kati ya Mwezi Mei na miezi mingine.
Karibu Ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera na Paroko wa Parokia ya Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba ni muendelezo wa mada Faraja ya Imani.
Fri, 17 May 2024 - 530 - Fahamu hatua za kuzifikia Sakramenti ya Upadre na majukumu yao.
Ungana na Padre Titus Aamigu katika kipindi cha Ujumbe wa Bibilia, mada ni juu ya Sakramenti ya Upadre.
Wed, 15 May 2024 - 55min - 529 - Fahamu namna ya Utume wa Walei Jimbo kuu la Dar es salaam Walivyo jipanga kuimalisha Imani kwa Waamini.
Karibu uungane na Mtangazaji Elizabeth Masanja katika kipindi cha Utume wa Walei, Mwezeshaji Padre Vitalis Kasembo Mkrurugenzi wa Utume wa Walei Jimbo kuu la Dar es salaam ameambatana na Dokta Hellen Makwani Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, wanaendelea na mada Clinic ya Uongozi.
Wed, 15 May 2024 - 528 - Fahamu namna ya watu walivyo shiriki kuinjilisha kwa haraka.
Ungana na Mtangazaji Fredy William katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi , Mwezeshaji Padre Dominic Mavula, Mkurugenzi wa Matangazo ya Radio Maria Tanzania, akiendelea kueelezea mada ya Injilisha kwa haraka.
Wed, 15 May 2024 - 55min - 527 - Fahamu upendo wa Yesu kwa Binadamu.
Karibu ungane na Martin Joseph katika kipindi cha Nena Nami Bwana, Mwezeshaji ni Padre Denis Mrimila, kutoka Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Kihesa Kanisa Kuu, Jimbo Katoliki Iringa, leo ananena nasi juu ya Upendo wa Yesu kwa Binadamu.
Wed, 15 May 2024 - 36min - 526 - Fahamu msimamo wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kuhusu ulinzi wa Watoto.
Ungana na Mtangazaji Happiness Mlewa katika kipindi cha Kutoka Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania, TEC, Mada inayozungumziwa ni juu ya ulinzi wa mtoto, Mwezeshaji Padre Paulino Mlingo, Mratibu kitengo cha ulinzi wa mtoto kutoka Baraza la Maaskofu Tanzani, TEC.
Wed, 15 May 2024 - 44min - 525 - Ifahamu nafasi ya Bikira Maria katika mahitaji ya Binadamu.
Karibu ungane na Ester Magai katika kipindi cha Mtaguso Mkuu wa Vatcan, muwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha, kutoka Parokia ya Mtakatifu Thomas Mtume Mrao Rombo, Jimbo Katoliki Moshi, leo anazungumzia nafasi ya Bikira Maria katika mahitaji ya Binadamu.
Wed, 15 May 2024 - 55min - 524 - Je, Wafahamu kwanini kulianzishwa na Madhehebu tofauti ya Kikristo katika Kanisa?
Karibu uungane na Mtangazaji Joyce Jonatus katika kipindi cha Maswali Yahusio Imani, Mwezeshaji Frateri Noa Jeshua Mwamfupi kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho – Jimbo kuu la Songea, akijibu swali linalo hoji, Je, kulikuwa na ulazima gani kuwepo na madhehebu tofauti ya Kikristo kwa kuwa wote wana muamini Mungu mmoja.
Wed, 15 May 2024 - 27min - 523 - Fahamu changamoto za kuheshimu utu na kutunza uhai.
ungana na Happiness Mlewa, katika kipindi cha Familia Bora na Nyumba Aminifu, Studio yupo na Paschal Maziku, Katekista Vicent Nathanael, Federika Bayaga, Benjamini Wasonga, Respicius Mwombeki na Consolata Mayemba, wakizungumzia changamoto zinazozikumba familia na jamii kiasi cha kokosa kuheshimu utu na kutunza uhai.
Wed, 15 May 2024 - 52min - 522 - Je, wafahamu kwanini Mapadre hawaoi?
Karibu ungane na Frateri Michael Paulo Mangazini, katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea. Swali linalotolewa majibu ni kwanini Mapadre hawaoi, kwani wao hawana tamaa kama binadamu wengine, na kama wanayo tamaa je si dhambi, wakati mwenyezi Mungu amesema nendeni duniani mkazaliane je hawajakengeuka agizo […]
Wed, 15 May 2024 - 28min - 521 - Ifahamu Sheria Na. 897-958 ya Ekaristi Takatifu?
Ungana na Padre Ladislaus Mgaya, Mwanasheria wa Sheria za Kanisa kutoka Jimbo Katoliki Njombe ambapo leo tunaangazia muda na mahali la Adhimisho ya Ekaristi Takatifu.
Wed, 15 May 2024 - 55min - 520 - Je, Wafahamu namna ya kupata Wito?
Ungana na Martin Joseph katika kipindi cha Elimu Jamii, Wawezeshaji Padre Isidory Tarimo, kutoka Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea, pamoja na naye Padre Abraham Nestory (OFM conv) Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Clara Mongola Ndege, Shirika la Ndugu wa Wadogo wa Fransisko wa Konventual,mada nii Miito.
Fri, 10 May 2024 - 58min - 519 - Roho Mtakatifu ni nani katika maisha yetu?
Karibu ungane nami Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Roho Mtakatifu na Kanisa leo tupo Askofu Mkuu Mstaafu Josaphat Louis Lebulu wa Jimbo Katoliki Arusha akizungumzia Zawadi ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu.
Wed, 15 May 2024 - 518 - Je, wafahamu Ubikira wa Milele wa Bikira Maria?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Franco Abel Ubamba , kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema naomba kujua juu ya Ubikira wa milele wa Maria.
Wed, 15 May 2024 - 26min - 517 - Ni, tofauti ipi iliyopo kati ya dhambi ya Mauti na dhambi isiyo ya Mauti?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Samson Peter Tibianus, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema nini tofauti ya Dhambi ya mauti na dhambi isiyo ya mauti kadiri ya mafundisho ya Kanisa Katoliki?
Wed, 15 May 2024 - 23min - 516 - Fahamu namna ya Utandawazi unavyo leta tija na faidi katika Jamii.
Ungana na Mtangazji Martin Joseph katika kipindi cha Fahamu wito wako, kinacho andaliwa na Padre Innocent Bahati kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela Jimbo kuu la Arusha, mada inayozungumziwa ni muendelezo mwa mada ya Utandawazi.
Fri, 10 May 2024 - 53min - 515 - Kwanini Kanisa Katoliki lilianzisha Jumuiya ndogondogo za Kikristo?
Kariba uungane na Mtangazaji Agatha Kisimba katika kipindi cha Utume wa Walei, Wawezeshaji na Kamati ya Uinjilishaji Jimbo kuu la Dar es salaam akiwemo, Walimu Damian Moses Ndimbo, Veran Mushi, Eleutery Kobelo na , mada iliyopo kwa leo ni Kristo mfufuka na Jumuiya ndogondogo za Kikikristo.
Fri, 10 May 2024 - 55min - 514 - Ni, kwa namna gani mwezi Mei ni Faraja ya Imani?
Karibu Ungane nami Erick Paschal, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera na Paroko wa Parokia ya Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba ni muendelezo wa mada Faraja ya Imani.
Fri, 10 May 2024 - 56min - 513 - Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya Kumi na tatu]
L'articolo Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya Kumi na tatu] proviene da Radio Maria.
Fri, 10 May 2024 - 53min - 512 - Ufahamu uhusiano kati ya Martin Luther na Kanisa la KKKT.
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Desderius Mwambaluka, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema ufahamu uhusiano kati ya Martin Luther na Kanisa la KKKT?
Wed, 15 May 2024 - 29min - 511 - Ni, kwanini Padre anavaa kanzu Jeusi ?
Ungana na Mhashamu Method Kilaini, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba katika muendelezo wa kipindi cha Historia ya Kanisa Maswali na majibu kutokana na mada mbalimbali zilizowasilishwa katika vipindi vya nyuma.
Wed, 08 May 2024 - 57min - 510 - Ni, kwa jinsi gani Bikira Maria ni Faraja ya Imani?
Karibu Ungane nami Fredy William, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera na Paroko wa Parokia ya Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba ni muendelezo wa mada Faraja ya Imani.
Wed, 08 May 2024 - 55min - 509 - Zifahamu mbinu za matumizi Sahihi ya Watembea kwa Miguu wawepo Barabarani.
Ungana na Mtangazaji Happiness Mlewa Katika Kipindi cha Usalama wa Barabarani, mada inayozungumziwa matumizi Sahihi ya Watembea kwa Miguu, Wawezeshaji ni kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, Mkaguzi wa Polisi Dumu Mwalugenge, Staff Sajenti Olele Chuwa koplo Abdaah Ismail.
Wed, 08 May 2024 - 49min - 508 - Je, unafahamu umuhimu wa Kanisa kuweka Sikukuu ya Pentekoste?
Karibu Ungane na Mtangazaji Happiness Mlewa katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Daudi Fungameza kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa lina hoji Pentekoste ni Sikukuu ya namna gan?
Wed, 08 May 2024 - 27min - 507 - Je, wafahamu madhara ya vidhibiti mimba na maisha ya Vijana na Dunia ya leo.
Karibu katika kipindi cha Pro Life -utetezi wa uhai, ambapo leo Wakufunzi wetu kutoka Pro Life Tanzania Bwana Anthony Lihepa, Bi. Janet Akkaro, Bwana Godfrey Mkaikuta, Bi.Witnes Joackim na Bi. Frida Manga, wanatuongoza katika hitimisho la mada madhara ya vidhibiti mimba.
Wed, 08 May 2024 - 56min - 506 - Je, wafahamu umuhimu wa kutunza uhai kwenye maisha ya Ndoa?
Ungana na Mtangazaji Happines Mlewa, Katika kipindi cha Familia Bora na Nyumba Aminifu Mwezeshaji ni Paschal Maziku akizungumzia juu ya kuheshimu na kutunza uhai katika Ndoa.
Mon, 06 May 2024 - 50min - 505 - Je, wafahamu msingi katika Ndoa?
Ungana na Mtangazaji Happines Mlewa, Katika kipindi cha Familia Bora na Nyumba Aminifu Mwezeshaji ni Paschal Maziku ambapo ni Muendelezo wa mada umuhimu wa kutunza uhai katika maisha ya Ndoa.
Mon, 06 May 2024 - 53min - 504 - Nini, maana ya Faraja?
Karibu Ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera na Paroko wa Parokia ya Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba. Mada Faraja ya Imani
Mon, 06 May 2024 - 56min - 503 - Ni, Kwa namna gani Bikira Maria ni Mama mwenye Unyenyekevu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Ayubu Polycarp Mwashibili, kutoka Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji Makongolosi Jimbo kuu la Mbeya Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Bikira Maria ni Mama mwenye unyenyekevu naomba kupewa maelezo kwa namna gani ?
Mon, 06 May 2024 - 26min - 502 - Tutafsiri vipi ndoto za Kikristo?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Ayubu Polycarp Mwashibili, kutoka Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji Makongolosi Jimbo kuu la Mbeya Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema siku hizi kumekuwa na watu wengi wanaojiita watafsiri wa ndoto, sasa tutafsiri vipi ndoto za Kikristo?
Mon, 06 May 2024 - 24min - 501 - Zifahamu Sheria za Ekaristi Takatifu.
Karibu uungane na Raymond Karega katika kipindi cha Sheria za Kanisa, kwa namna ya kipekee Padre Ladsilaus Mgaya, Mwanasheria wa Sheria za Kanisa kutoka Jimbo Katoliki Njombe, anazungumzia sheria za Ekaristi Takatifu.
Sun, 05 May 2024 - 52min - 500 - Ufahamu Uraibu wa tabia ya uongo.
Ungana na Happiness Mlewa katika kipindi cha Uraibu, muwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha, kutoka Jimbo Katoliki Moshi, mada anayozungumzia ni tabia ya uongo.
Sun, 05 May 2024 - 57min - 499 - Fahamu uhusiano wa utandawazi na wito wako.
Karibu ungane na Martin Joseph katika kipindi cha Fahamu Wito Wako, Muwezeshaji ni Padre Innocent Bahati Mushi, kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, Jimbo Kuu la Arusha, mada anayozungumzia ni mambo ya utandawazi.
Fri, 03 May 2024 - 47min - 498 - Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya kumi na mbili]
L'articolo Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya kumi na mbili] proviene da Radio Maria.
Fri, 03 May 2024 - 50min - 497 - Je, Mei mosi ni sikukuu ya Kikanisa au ya Kiserikali?
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, kutoka seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, na Frateri Jackob Venusto Mkandawile anajibu swali lililoulizwa je, Mei mosi ni sikukuu ya Kikanisa au ya Kiserikali, na kwanini Mtakatifu Yosefu aliwekwa msimamizi wa Wafanyakazi?
Fri, 03 May 2024 - 29min - 496 - Fahamu Historia ya Rozari Takatifu.
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Ayubu Polykap Mwashibili, kutoka Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji Jimbo kuu la Mbeya Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Rozari Takatifu ni nini? na naomba nijue na Historia yake
Fri, 03 May 2024 - 55min - 495 - Fahamu maana ya Mirathi na faida zake.
Karibu uungane na Mtangazaji Elizabeth Masanja katika Kipindi cha Ijue Sheria, Mwezeshaji ni Mheshimiwa Hassan Mlanga, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Bomani Iringa Mjini, Mada tunayojifunza siku ya leo ni maana ya Mirathi, faida yake na mchakato wa ufuatiliaji.
Fri, 03 May 2024 - 50min - 494 - Ni, kwa namna gani Maandiko Matakatifu yanatualika kuinjilisha kwa haraka?
Karibu Ungane nami Erick Paschal, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera na Paroko wa Parokia ya Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba. Mada ni Injilisha kwa haraka
Fri, 03 May 2024 - 57min - 493 - Fahamu juu ya muendelezo wa Uzao wa Adam na Hawa.
Karibu Uungane na Mtangazaji Happiness Mlewa katika Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, Mwezeshaji ni Frateri Ayuto Kogwa kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho – Jimbo kuu la Songea, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linahoji kabla ya Adam na Eva je, kulikuwa na watu wengine waliokuwa wakiishi Duniani?
Fri, 03 May 2024 - 29min - 492 - Ni, Kwanini Wakatoliki tunapokea Mwili wa Kristo katika Umbo la Mkate tuu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Peter Mjwauzi, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kwanini sisi Wakatoliki tunapokea mwili wa Kristo katika umbo la Mkate tuu na wakati wa Sala ya Ekaristi Padre anasema twaeni mnywe wote?
Mon, 29 Apr 2024 - 28min - 491 - Fahamu mambo unayotakiwa kufanya unapoingia Kanisani hadi inapoisha Misa Takatifu.
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea. Leo Frateri Elikana Nyagabona anajibu swali lililoulizwa, naomba kujua ninapoingia Kanisani ni mambo gani natakiwa kufanya hadi inapoisha Misa Takatifu?
Fri, 03 May 2024 - 27min - 490 - Je, Wafahamu Mashirika yanayotumia neno Bruda?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Faxon Polycarp Mpili, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali linalojibiwa linasema neno Bruda lina maana gani? ni mashirika gani wanatumia neno bruda, na kazi zao ni zipi katika kanisa.
Mon, 29 Apr 2024 - 19min - 489 - Je, Wafahamu vipindi vya Liturujia katika Kanisa Katoliki?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Baltazar Bao, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Tunaomba kuelezwa kuhusu vipindi vya kiliturujia katika Kanisa Katoliki maana tumekuwa tukisikia wanasema sasa ni kipindi cha Krismas, mara Majilio mara Pasaka, kiukweli hatuelewi maana yake pia mpangilio […]
Mon, 29 Apr 2024 - 26min - 488 - Je, Wafahamu Siri ya Miaka 28 ya Radio Maria Tanzania kwa Wanautume wake?
Uinjilishaji ni wajibu wa kila Mkristo Mbazitwa, Radio Maria Tanzania inarahisisha kazi hiyo ya Uinjilishaji kupitia vipindi vyake Mbalimbali Katika miaka 28 ya Radio Maria Tanzania, karibu uwasikilize Wanautume wa Radio Maria Tanzania wakielezea Utume huu Miaka 28 iliyopita kupitia Makala hii iliyotayarishwa na Agatha Kisimba.
Fri, 26 Apr 2024 - 54min - 487 - Miaka 28 ya Utume wa Radio Maria nchini Tanzania
Karibu usikilize Makala maalumu ya Miaka 28 ya Uinjilishaji wa Radio Maria Tanzania Katika makala hii , Rais wa Radio Maria Tanzania Ndugu Humphrey Julius Kira, amezungumzia Miaka 28 ya Radio Maria Tanzania tangu kuanzishwa kwake Aprili 26,1996 na pia ameelezea kwa undani namna Taasisi hii ilivyokuwa na kuenea kwa wigo wa Matangazo hapa nchini […]
Fri, 26 Apr 2024 - 58min - 486 - Fahamu dalili za wito wa maisha ya wakfu.
Ungana na Fredy William katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, ambapo Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, anazungumzia juu ya dalili za wito wa maisha ya wakfu.
Fri, 26 Apr 2024 - 53min - 485 - Fahamu dalili au cheche za wito.
Karibu Ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Maria Tanzania, Mada ni muendelezo wa dalili au cheche za wito.
Fri, 26 Apr 2024 - 56min - 484 - Je, ni kweli Makadinari wa Afrika hawachaguliwi kuwa Mapapa?
Karibu katika Kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu la Songea, Frateri Noah Mwamfupe anajibu swali lililoulizwa, Kwanini Makadinari wa Afrika hawachaguliwi kuwa Mapapa?
Wed, 24 Apr 2024 - 24min - 483 - Je, Wafahamu kwanini Wakristo husherekea Sikukuu ya Pasaka?
Karibu Uungane na Elizabeth Masanja katika Kipindi cha Utume wa Walei, Mada inayozungumziwa ni juu muendelezo kwanini tunasherekea Pasaka, Mwezeshaji Ndugu Luuteliko Ubelo kutoka kamati ya Uinjilishaji kutoka Utume wa Walei Jimbo kuu la Dar es salaam.
Wed, 24 Apr 2024 - 42min - 482 - Fahamu barua za kitume za Baba Mtakatifu Yohane Paulo II.
Ungana na Joyce Jonatus katika Kipindi cha Mtaguso Mkuu wa Vatcan, ambapo Padre Richard Matanda Tesha kutoka Jimbo Katoliki Moshi, anazungumzia juu ya Barua za kitume za Baba Mtakatifu Yohane Paulo II.
Wed, 24 Apr 2024 - 49min - 481 - Je, Wafahamu Utaratibu Wakusoma Masomo Kanisani?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateli Ezekieli Ngimba, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kwanini Masomo Kanisani katika maandiko matakatifu yanasomwa vipande vipande, Je yale yasiyosomwa hayafai?
Wed, 24 Apr 2024 - 24min
Podcasts similar to Radio Maria Tanzania
- Conversations ABC listen
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Affaires sensibles France Inter
- Dateline NBC NBC News
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- アンガールズのジャンピン[オールナイトニッポンPODCAST] ニッポン放送
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 吳淡如人生實用商學院 吳淡如
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR
Other Religion & Spirituality Podcasts
- Joel Osteen Podcast Joel Osteen, SiriusXM
- Joseph Prince Audio Podcast Joseph Prince
- Apostle Joshua Selman Apostle Joshua Selman
- Unter Pfarrerstöchtern ZEIT ONLINE
- Joyce Meyer Enjoying Everyday Life® Radio Podcast Joyce Meyer
- Andrew Wommack Conferences Andrew Wommack
- Sai Baba Fever FM - HT smartcast
- Laxmi Ji Ki Aarti Hubhopper
- Translation of the Quran in Swahili Unknown
- The Potter's Touch on Lightsource.com - Audio Bishop T.D. Jakes
- Hanuman Chalisa Hubhopper
- OM Shradha
- Joyce Meyer's Talk It Out Podcast Joyce Meyer
- Sai Baba Mantra Hubhopper
- Shri Hanuman Chalisa - Sandeep Khurana Sandeep Khurana
- Krishan Bhajan Hubhopper
- Pastor E. A. Adeboye Messages on DownloadSermon.com DownloadSermon Nigeria
- Faith Life Church with Keith Moore (Audio) Keith Moore
- Our Daily Bread Podcast | Our Daily Bread Our Daily Bread Ministries
- Koinonia Experience With Apostle Joshua Selman (ENI) Abraham Abiodun Ayinde