Filtrar por género

Meza Huru

Meza Huru

Meza Huru

Tanzanian music, from Genesis to currently status told by Stake holders.

23 - Mezani na LUCCI #22
0:00 / 0:00
1x
  • 23 - Mezani na LUCCI #22

    Marehemu CPWAA anatajwa kama mmoja wa wasanii wa kwanza kufanya muziki wa Crank (KING OF BONGO FLEVA CRANK) kupitia ngoma ya PWAA iliyotayarishwa na LUCCI chini ya Mawingu Studio. Hii inamaanisha kuwa Lucci ni mmoja wa waandaaji wa kwanza kwa muziki wa Bongo Fleva wenye mahadhi ya Crank. Mbali na kutayarisha muziki vilevile Lucci anasimama kama msanii baada ya kushiriki kwenye nyimbo kadhaa mfano Kaka na Dada aliyoshirikishwa na Jokate ambae kwasasa ni Katibu Mkuu wa UWT kupitia chama cha CCM.

    Fri, 01 Nov 2024 - 1h 53min
  • 22 - Mezani na DARK MASTER #21

    Bado kiwanda cha Bongo Fleva kinaendelea kukumbuka mchango mkubwa wa vijana walioiwakilisha Dodoma mwanzoni mwa mwaka 2001 kupitia ngoma zao kadhaa ambazo zinachezwa na kusikilizwa mpaka hivi sasa.


    Wanaitwa Chemba Squad, ambapo ndani yake majina kama Noorah aka Baba stylz, Dark Master, Albert Mangwea na Mez B wa area C yalitajwa kuunda kundi hilo.


    Ngoma kama Ice Cream, Ghetto langu na Kama Vipi zinatajwa kama ngoma bora za muda wote kutoka kwa wakali hao ambapo hivi sasa wamebaki wawili tu (Noorah yupo zake Shy Town na Dark Master akiwa Dar es salaam) huku bahati mbaya Ngwea na Mez B wakiwa ni marehemu (RIP).


    Leo tunakusogezea historia kamili na mengi usiyoyajua kuhusu Dark Master aka MwanaChemba.

    Fri, 20 Sep 2024 - 1h 30min
  • 21 - Mezani na FEROOZ #20

    Je Unamfahamu FERUZI MRISHO? Gwiji na moja wa waanzilishi na NUNDA mkuu wa DAZ NUNDAZ. Mwenyewe akitambulika zaidi kama Kamanda kabla Kamanda haijawa THE ANTHEM it is now. Leo tuko nae mezani akitusimulia safari yake yote ya mziki, toka anaandikiwa mashairi na dada yake Achane mpaka anatunga tungo matata kama Starehe, Kamanda, Nitafanya Nini, Jirushe, Elimu dunia N.K. Karibu Mezani.

    Fri, 02 Aug 2024 - 1h 35min
  • 20 - Mezani na MARLON LINJE #19

    Je, Unamfahamu producer ambaye, dare I say it, bila yeye labda kwaya au bendi yako maarufu usingeisikia kama ulivyoisikia? Producer ambaye amefanya zaidi ya 80% ya production ya mziki wote wa bendi na kwaya Tanzania kwa miaka 30. Marlon Linje, bonge la mshika dau, leo yupo nawe mezani, karibu.

    Thu, 18 Jul 2024 - 2h 58min
  • 19 - Mezani na MANDOJO NA DOMOKAYA #18

    Usichofahamu ni majina yao halisi Joseph Francis Michael Ong'oso na Precious Juma Mkoma maarufu kama Man'Dojo na Domokaya. Wanamuziki mashuhuri sana wa kizazi cha jana na leo.  nani asiyepende kusikia sauti nzuri na za kuvutia zikisindikizwa na Guitar lao(wenyewe wanaliita Banjo)?  Nani asiyetambua uwezo wa miamba hawa wa muziki katika kuweka viitikio na vionjo makini katika nyimbo mbalimbali za Muziki wa Kibongo? Hawa ni marafiki waliogeuka ndugu, wenyewe wanadai wamepitia mpaka kuvaa nguo sare 😁 Meza Huru imekaa nao na kupata simulizi ya maisha yao ya muziki na amini kwamba, inavutia sana.  Jumuika nasi mezani kuwasililiza 😊, Karibu  #MezaniNaMandojoNaDomokaya  #MezaHuru

    Fri, 25 Nov 2022 - 2h 30min
Mostrar más episodios