Filtrer par genre
HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho
Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na Roho tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili. Kwa kweli, nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo. Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
- 13 - 1. Wokovu wa Wenye Dhambi Unafunuliwa Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-21)
Wigo wa mstahili wa ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa na dhiraa 100 kwa urefu. Katika Biblia, dhiraa moja ulikuwa ni urefu unaoanzia katika kiwiko cha mtu hadi katika ncha ya kidole, takribani sawa na sentimita 45 kwa vipimo vya kisasa. Kwa hiyo, wigo wa ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa ni dhiraa 100 maana yake ni kwamba ulikuwa na urefu wa mita 45, na kule kusema kwamba urefu wake ulikuwa ni dhiraa 50 maana yake ni kuwa upana wake ulikuwa takribani mita 22.5. Kwa hiyo, hivi vilikuwa ndivyo vipimo vya Nyumba ambayo Mungu aliishi kati ya watu wa Israeli katika kipindi cha Agano la Kale. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 1h 43min - 12 - 2. Nguzo za Ua wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-19)
Kifungu hiki kinaelezea juu ya nguzo, lango la pazia, mapazia ya kitani safi ya kusokotwa, mikanda, vishikizio, vikuku vya shaba, na vigingi vya shaba vya ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa ni mahali ambapo Mungu alikaa. Kipimo cha huo ua wa mstatili ulikuwa ni takribani mita 45 (kwa upande wake wa kaskazini na kusini) kwa mita 22.5 (katika upande wake wa mashariki na magharibi). Kimsingi, Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa na umbo dogo lililokuwa na paa la lililokunjwa mara nne. Kwa upande mwingine, ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa ni mpana kama uwanja wa wazi. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 1h 04min - 11 - 3. Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa Iliyotengenezwa Kwa Mti wa Mshita na Kufunikwa Kwa Shaba (Kutoka 38:1-7)
Ili mwenye dhambi yeyote kati ya watu wa Israeli aweze kuondolewa dhambi zake, basi ilimpasa kuleta mnyama wa sadaka ya kuteketezwa katika Hema Takatifu la Kukutania, na kisha kuzipitisha dhambi zake juu ya mnyama huyo wa sadaka kwa kuiweka mikono yake juu ya kichwa cha mwanasadaka huyo, na kisha kuikinga damu yake, na kisha kuikabidhi damu hii kwa kuhani. Kuhani aliye katika zamu yake aliiweka damu hii ya mwanasadaka katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, aliyaweka mafuta na nyama ya mwanasadaka huyo juu ya madhabahu, kisha akavichoma vitu hivyo kama manukato mazuri kwa Bwana Mungu. Hata Kuhani Mkuu, ili aweze kupokea ondoleo la dhambi zake, basi alipaswa kuiweka mikono yake juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kisha kuzipitisha dhambi zake kwa mnyama huyo mbele ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Hii ilikuwa ni sadaka ya upatanisho iliyokuwa ikitolewa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo ilitengenezwa kutokana na mti wa mshita na kisha kufunikwa kwa shaba, na sadaka hii ya ondoleo la dhambi ilitolewa baada ya tendo la kuiweka mikono juu ya mwanasadaka na kisha kuimwaga damu huyo mwanasadaka. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 45min - 10 - 4. Madhabahu ya Uvumba Ni Mahali Ambapo Mungu Anaitoa Neema Yake (Kutoka 30:1-10)
Kama tungeliingia ndani ya Mahali Patakatifu, ambapo ni Nyumba ya Mungu, kitu cha kwanza ambacho tungelikiona ni kinara cha taa, meza ya mikate ya wonyesho, na madhabahu ya uvumba. Madhabahu ya uvumba iliwekwa mbele ya lango la kuingia Patakatifu pa Patakatifu, mahali ambapo kiti cha rehema kilikuwa kimewekwa, yaani baada ya kukipita kinara cha taa na meza ya mikate ya wonyesho. Urefu na upana wa madhabahu hii ya uvumba ulikuwa ni dhiraa moja, wakati kimo chake kilikuwa ni dhiraa mbili. Katika Biblia, dhiraa ni takribani sentimita 45-50 kwa vipimo vya hivi sasa. Hivyo, madhabahu ya uvumba ilikuwa na mraba mdogo wenye vipimo vya takribani sentimita 50 kwa urefu na upana na sentimita 100 kwa kimo. Kama ilivyokuwa kwa madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, madhabahu ya uvumba pia ilikuwa na pembe katika zake nne za juu. Hali ikiwa imetengenezwa kwa mti wa mshita, madhabahu ya uvumba ilikuwa imefunikwa yote kwa dhahabu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 47min - 9 - 5. Maana ya Kiroho ya Vikuku vya Fedha Vilivyotumika Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 26:15-30)
Mbao zote za Hema Takatifu la Kukutania mahali ambapo Mungu alikaa zilikuwa zimefunikwa kwa dhahabu. Mungu alimwambia Musa kutengeneza vikuku vya fedha ili kuushikiza ubao uweze uweze kusimama wima. Maana ya kiroho ya kuweka hivi vikuku vya fedha chini ya kila ubao ni kama ifuatayo. Katika Biblia, dhahabu ina maanisha ni imani ambayo haiwezi kubadilika kutokana na wakati. Kule kusema kwamba hivi vikuku vya kushikiza viliwekwa dhini ya ubato uliokuwa umefunikwa kwa dhahabu maana yake ni kwamba Mungu ametupatia karama mbili ambazo zinatuhakikishia wokovu wetu. Kwa maneno mengine, ina maanisha kwamba Yesu ameukamilisha wokovu wetu toka katika dhambi kwa kubatizwa na kuimwaga damu yake. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 1h 06min - 8 - 6. Kiti cha Rehema (Kutoka 25:10-22)
Ndani ya Hema Takatifu la Kukutania kulikuwa kumegawanyika katika sehemu kuu mbili: Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu. Kulikuwa na pazia kati ya sehemu hizo mbili, na Sanduku la Ushuhuda lilikuwa nyuma ya pazia hili na ndani ya Patakatifu pa Patakatifu. Mfuniko wa Sanduku la Ushuhuda unajulikana pia kwamba ni kiti cha rehema. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 43min - 7 - 7. Vikombe Vya Mapambo Kwa Injili ya Maji na Roho (Kutoka 25:31-40)
Kifungu hiki kinaelezea juu ya kinara cha taa cha Hema Takatifu la Kukutania. Leo nitapenda kuelezea juu ya maana ya kiroho ya vikombe hivi vya mapambo, maua na taa. Mungu alimwamuru Musa kutengeneza kwamba mhimili wa taa ili kutengeneza kinara cha taa cha dhahabu. Hivyo, kitu cha kwanza kilichofanyika ilikuwa ni kutengeneza huo mhimili, kisha baada ya huo mhimili yaliunganishwa matawi pembeni yake. Kila upande wa huo mhimili kulitengenezwa matawi matatu, kisha katika kila tawi kulikuwa na mabakuli matatu mfano wa ua la lozi, kisha vikombe vya mapambo na maua vilitengenezwa. Vivyo hivyo, taa saba ziliwekwa juu ya matawi hayo ili kuuangaza. Hivyo kinara cha taa kiliweza kuangaza vizuri kabisa ndani ya Patakatifu pa Patakatifu pamoja na vyombo vyake vya ndani. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 55min - 6 - 8. Maana za Kiroho Zilizofichika Katika Mavazi ya Kuhani Mkuu (Kutoka 28:1-43)
Leo tutakwenda kuangalia juu ya maana za kiroho zilizofichika katika mavazi ya Kuhani Mkuu. Haruni alipaswa kuyavaa mavazi haya pamoja na watoto wake. Kwa kupitia mavazi haya ya Kuhani Mkuu tutaweza kutambua kwa imani juu ya mpango wa Mungu ambao umetuokoa toka katika dhambi. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 55min - 5 - 9. Utakatifu Kwa Bwana (Kutoka 28:36-43)
Mungu anatuonyesha nini kupitia kilemba hiki cha Kuhani Mkuu? Kilemba na yale mapambo yake vina maanisha kwamba Yesu Kristo alizichukua dhambi zetu zote kwa kupitia ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji na kwa sababu hiyo amezisafishilia mbali dhambi zetu zote. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 53min - 4 - 10. Kifuko cha Kifuani cha Hukumu (Kutoka 28:15-30)
Hebu sasa tukiangalie kifuko cha kifuani ambacho Kuhani Mkuu alikitumia katika kuwahukumu watu wa Israeli. Kifungu cha maandiko hapo juu kinatueleza kuwa kifuko cha kifuani cha hukumu kilitengenezwa kwa kitambaa kilichokuwa na mraba unaolingana kwa vipimo kwa urefu na upana wake. Kitambaa hiki kilikuwa kimefumwa kiujuzi kwa nyuzi za dhahabu, za bluu, za zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Vito kumi na mbili vya thamani viliwekwa katika kitambaa hiki huku kila mstari ukiwa na vito vitatu na hivyo kufanya jumla ya mistari minne. Pia Mungu alimwambia Musa kuweka Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu. Urimu na Thumimu zina maanisha ni ‘mwanga na ukamilifu.’ https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 1h 01min - 3 - 11. Sadaka ya Dhambi Ili Kumsimika Kuhani Mkuu (Kutoka 29:1-14)
Leo hii hebu tuangalie katika kumsimika Kuhani Mkuu. Hapa tunaona kwamba Mungu alimwamuru Musa jinsi yay kumsimika Haruni na wanawe kwa kina. Neno “kusimika” ambalo linaonekana kimaana katika aya ya 9 maana yake hi kufanya kitu kuwa kitakatifu, kuandaa, kuweka wakfu, kumheshimu, na kumchukulia mtu au kitu kama kitakatifu. Kwa maneno mengine, kusimikwa maana yake ni kutakaswa na kuwekwa wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hivyo, “kusimikwa kama Kuhani Mkuu” maana yake ni “kuwekwa kando ili kupewa mamlaka na majukumu ya Kuhani Mkuu.” Mungu alimpatia Haruni pamoja na wanawe haki ya kuwa Kuhani Mkuu na ukuhani ambao ulimwezesha kuwapatia watu wake ondoleo la dhambi. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 50min - 2 - 12. Kuhani Mkuu Aliyetoa Sadaka Siku ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 16:1-34)
Ni Kuhani Mkuu ndiye aliyetoa sadaka katika Siku ya Upatanisho kwa ajili ya watu wa Israeli. Sadaka hii ilitolewa mara moja kwa mwaka siku ya kumi ya mwezi wa saba katika kalenda ya Kiisraeli. Katika siku hii, wakati Kuhani Mkuu Haruni alipotoa sadaka kwa niaba ya watu wa Israeli kwa ajili yao, basi maovu yao yote yalipitishwa kwenda kwa mwanasadaka huyu wa sadaka ya kuteketezwa na kisha kusafishiliwa mbali. Hivyo, Siku ya Upatanisho ilikuwa ni sikukuu kubwa kwa watu wa Israeli. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 1h 35min - 1 - 13. Vifaa Vilivyotumika Katika Mavazi ya Kuhani Mkuu (Kutoka 28:1-14)
Hebu sasa tuangalie vifaa vilivyotumika katika kutengenezea mavazi ya Kuhani Mkuu. Naivera ilikuwa ni kifaa cha ajabu katika mavazi yaliyovaliwa na Kuhani Mkuu. Hii naivera ilikuwa imefumwa kwa nyuzi za dhahabu, bluu, zambarau, na nyekundu na kitani safi ya kusokotwa. Hili vazi takatifu la Kuhani Mkuu lilitengenezwa na fundi stadi aliyezifuma na kuzitarizi hizo nyuzi tano. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 1h 00min
Podcasts similaires à HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Espacio en blanco Radio Nacional
- Les Grosses Têtes RTL
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR