Filtra per genere
Uhusiano Kati ya Huduma Ya YESU na Ile Ya YOHANA MBATIZAJI Kama Ilivyoandikwa Katika Injili Nne
Agano Jipya linaanza na Injili Nne ambazo ni Mathayo, Marko, Luka, na Yohana. Injili zote Nne zilishughulika na ziliandika kikamilifu kuhusu huduma ya Yohana Mbatizaji. Hii ni kwa sababu huduma yake ni ya muhimu sana. Hatuwezi kudai kuwa tunaifahamu huduma ya Yesu Kristo pasipo uelewa wa huduma ya Yohana Mbatizaji. Kama ndivyo, basi tunaweza kujiuliza, "Je, huduma ya Yohana Mbatizaji iliandikwa katika Injili Nne kwa umuhimu kiasi hicho?" Hali akimzungumzia Yohana Mbatizaji, Yesu alisema, "Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja" (Mathayo 11:14). Hivyo, Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtu aliyezaliwa katika dunia hii ili kuitekeleza huduma maalumu. Pia Yesu alisema, "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka" (Mathayo 11:12). Hii ni kweli kwa sababu Yohana Mbatizaji alizaliwa katika dunia hii, na wakati alipombatiza Yesu Kristo, dhambi za ulimwengu zilipitishwa kwenda kwa Yesu. Hivyo, Yesu aliweza kuzibeba dhambi za ulimwengu mara moja. Kwa kuruhusu jambo kuwa hivyo, Bwana amewaruhusu wale wanaoamini katika huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu kuingia Mbinguni kwa kupokea utakaso wa dhambi. Hii ndiyo maana iliyomo katika kifungu cha maandiko toka katika Injili ya Mathayo sura ya 11, aya ya 12-14. Je, unaamini kuwa injili ya maji na Roho ndiyo Ukweli? Ikiwa unaamini hivyo, basi hii ina maanisha kuwa unaifahamu huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu kikamilifu. Hata hivyo, Wakristo wengi ambao hawaifahamu huduma ya Yohana Mbatizaji hawaufahamu ukweli wa injili ya maji na Roho, na kwa sababu hiyo wanaishi maisha yao ya kiimani kwa jinsi ya matamanio ya miili yao. Pamoja na kuwa hawana ufahamu, watu wa jinsi hiyo hawajaribu hata kuifahamu huduma ya Yohana Mbatizaji iliyoandikwa katika Injili Nne. Kwa sababu hiyo, huduma ya Yohana Mbatizaji imekuwa haiheshimiwi kwa muda mrefu hata miongoni mwa Wakristo wanaodai kumwamini Yesu. Pengine kwa sababu hii, ninaona kuna watu wengi siku hizi ambao hawavutiwi na huduma ya Yohana Mbatizaji. Hivyo, watu wanakawaida ya kuwashangaa wale wanaovutiwa na mada hii. Hii ni kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiitazama kwa mbali huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu kiubishi kwa muda mrefu. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
- 12 - 1. Ni Lazima Uifahamu na Kuiamini Huduma ya Yohana Mbatizaji (Marko 1:1-2)
Marko 1:2 inasema, “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako.” Ndugu zangu waamini, unaweza kuipata haki ya Mungu ikiwa tu utatupilia mbali uelewa wa kale na kuifuata Biblia kadri Neno la Mungu linavyokuongoza. Hivyo, wakati unaposoma Neno la Mungu, ni lazima ulisome hali ukiwa umeyaacha mawazo na tamaa zako za mwili. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo unapoweza kutambua na kuamini katika mapenzi ya Mungu ambayo anataka kuyatimiza. Kanuni hiyo inatumika pia katika kifungu cha Maandiko cha leo. Ni pale tu utakapokuwa umeyaachilia mbali mawazo yako ya kimwili na kisha ukalifuata Neno la Mungu linapokuongoza ndipo unapoweza kufahamu kiusahihi huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 35min - 11 - 2. Yohana Mbatizaji Hakushindwa (Mathayo 11:1-14)
Ni huduma gani hasa ambayo Yohana Mbatizaji aliitimiza kabla ya Yesu? Wakristo wengi leo hii hawamfahamu vizuri Yohana Mbatizaji, hivyo wanatakiwa kupata mtazamo mpya kuhusu Yohana Mbatizaji ili waweze kumfahamu na kuikubali huduma yake kikamilifu. Sisi sote tunapaswa kuwa na ufahamu sahihi na kuukubali uhusiano kati ya huduma ya Yesu na ile ya Yohana Mbatizaji. Kwa kuufahamu uhusiano huu kikamilifu, basi unapaswa kwanza kulipokea ondoleo la dhambi kwa imani. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 1h 04min - 10 - 3. Yohana Mbatizaji, Aliyekuja Katika Njia ya Haki (Mathayo 17:1-13)
Kifungu cha Maandiko cha leo kinatoka katika injili ya Mathayo 17:1-13. Kifungu hiki kinaeleza kuwa Yesu aliwachukua wanafunzi watatu, Petro, Yakobo, na Yohana na akawaongoza kwenda katika mlima mrefu sana. Jambo la kushangaza lilitokea kule mlimani. Musa na Eliya walishuka toka Mbinguni. Na mavazi ya Yesu yalibadilika yakang’aa na kuwa meupe na sura yake ikabadilika pia. Yesu alizungumza na Musa na Eliya. Petro alipoona hivyo, akazungumza katika hali kindoto, “Na tufanye vibanda vitabu: kimoja chako, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Tunapenda kujenga vibanda vitatu na kuishi pamoja nawe.” Kisha wingu likawafunika na sauti ikasema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye!” https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 47min - 9 - 4. Itazame Huduma ya Yohana Mbatizaji! (Luka 1:17-23)
Injili ya Luka katika sura ya 1 aya ile ya 17 inaeleza kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtu aliyekuja katika roho na nguvu ya Eliya na akaifanya kazi ya kuwarudisha watu kwa Mungu mbele ya uwepo wa Bwana. Yohana Mbatizaji alikuwa ni tofauti na watu wengine tangu alipozaliwa. Sisi watu wa kawaida tunaoana na kisha kuzaa watoto kwa kudhamiria au kutodhamiria kadri muda unavyozidi kwenda. Lakini Yohana Mbatizaji ni mtu ambaye kuzaliwa kwake kulikwisha tabiriwa na kuandaliwa katika Agano la Kale. Inasemwa kuwa Yohana Mbatizaji atakuja kwetu katika roho na nguvu ya Eliya. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Tue, 24 Jan 2023 - 58min - 8 - 5. Tuufurahie Utukufu wa Mungu Kwa Shukrani (Yohan 1:1-14)
Injili ya Yohana, Vitabu vitatu vya 1, 2, na 3 Yohana, na Kitabu cha Ufunuo ni Maandiko yaliyoandikwa na Mtume Yohana. Kwa kupitia Maandiko haya, basi tunaweza kuona jinsi imani ya Mtume Yohana ilivyokuwa, na pia jinsi imani ya wanafunzi wa Yesu ilivyokuwa. Mtume Yohana aliamini kuwa Yesu alikuwa ni Mungu halisi aliyeumba ulimwengu wote na sisi wanadamu, na kwamba Mungu alikuwa ni Mwokozi wake na Mwokozi wa wanadamu wote. Sisi sote tunapaswa kuwa na aina hii ya imani. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Mon, 23 Jan 2023 - 55min - 7 - 6. Je, Unazifahamu Huduma za Watumishi Wawili wa Mungu? (Yohana 1:30-36)
Kifungu cha maandiko cha leo kinatoka katika injili ya Yohana 1:30-36. Watumishi wa Mungu wanaoamini katika injili ya maji na Roho wanafahamu wote kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu na Mwokozi wa wenye dhambi. Vivyo hivyo, wale ambao wanamfahamu na kumwamini Mungu kwa kweli wanaweza kutambua kuwa Yohana Mbatizaji aliitimiza huduma muhimu na ya thamani akiwa kama mtumishi wa Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Mon, 23 Jan 2023 - 51min - 6 - 7. Kwa Nini Yesu Alipaswa Kuupokea Ubatizo? (Yohana 3:22-36)
Watu wengi hawafahamu ni kwa nini Yesu alikuja hapa ulimwenguni na akaupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji. Lakini ni lazima tufahamu vizuri kuhusu dhumuni la ubatizo ambao Yesu aliupokea, kuhusu Yohana Mbatizaji ambaye alimbatiza Yesu, na kuhusu uhusiano kati ya watu hao wawili. Kwa hiyo, kwanza kwa kutumia aya za Maandiko ninataka kuangalia habari za msingi na dhumuni la ubatizo wa Yesu uliotolewa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani. Na ili kufanya hivyo ni lazima tugeukie katika Injili ya Mathayo na kisha kumchunguza Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Mon, 23 Jan 2023 - 1h 01min - 5 - 8. Ieneze Injili ya Kweli na Tendo la Haki la Yesu (Mathayo 3:1-17)
Ni hakika kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtu muhimu sana katika Biblia. Yohana Mbatizaji aliwalilia watu wa Israeli ili wafanye toba. Ni lazima tuzikumbuke kikamilifu kazi za Yesu na Yohana Mbatizaji. Yesu, aliyekuja hapa duniani aliwaokoa wanadamu, akitii mapenzi ya Mungu wakiwa pamoja na Yohana Mbatizaji. Yohana Mbatizaji na Yesu walikuja hapa duniani na wakayakamilisha matendo ya haki. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Mon, 23 Jan 2023 - 23min - 4 - 9. Uhusiano Kati ya Kazi ya Yohana Mbatizaji na Injili ya Upatanisho wa Dhambi zetu (Mathayo 21:32)
Katika Injili ya Yohana sura ya 1 aya ya 6-7 imeandikwa hivi kumhusu Yohana Mbatizaji “Palitokea mtu ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Huyu alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.” Katika kifungu hiki, Mtume Yohana anashuhudia umuhimu wa ubatizo ambao Yohana Mbatizaji alimpatia Yesu huku akiuhusianisha na injili ya wokovu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Mon, 23 Jan 2023 - 1h 30min - 3 - 10. Yesu Aliyekuja Kuzitoweshea Mbali Dhambi Zako (Mathayo 3:13-17)
Hata Wakristo wa leo wanakiri kuwa wanamwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wao, lakini wengi wao hawafahamu kuwa Yesu ni Bwana aliyetukomboa toka katika dhambi zetu zote kwa kupitia injili ya maji na Roho. Hivyo ni muhimu sana kuwathibitisha kwa kutumia injili hii ya maji na Roho kuwa kwa hakika Yesu ni Mwokozi. Kwa kuwa wote wanazaliwa kama wenye dhambi, basi wote wanapaswa kuamini katika injili ya maji na Roho ili waweze kuoshwa dhambi zao. Kwa maneno mengine, ili waweze kuzaliwa tena upya, ni lazima waamini katika injili ya maji na Roho, na wanaweza kumwona Bwana mara watakapoamini hivyo tu. Kupokea ama kuto kupokea ondoleo la dhambi na kuzaliwa tena upya kunategemea ikiwa tunamwamini Yesu Kristo kiusahihi. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Mon, 23 Jan 2023 - 1h 16min - 2 - 11. “Tazama, Namtuma Mjumbe Wangu” (Marko 1:1-5)
Yohana Mbatizaji alikuwa akiuhuburi nyikani ubatizo wa toba wa ondoleo la dhambi. Si hilo tu, alikuwa ni mtu ambaye ataufanya ubatizo wa Yesu ambao utazihamishia dhambi za watu wote wa ulimwengu kwenda kwa Yesu. Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa ni nabii wa mwisho wa kipindi cha Agano la Kale na mtu aliyezaliwa katika nyumba ya Kuhani Mkuu, basi ndio maana alikuwa ni mtumishi ambaye atazihamishia dhambi zote za wanadamu kwenda kwa Yesu kwa kupitia ubatizo kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Mon, 23 Jan 2023 - 1h 51min - 1 - 12. Tumwamini Yesu Tukiwa na Ufahamu wa Yohana Mbatizaji (Luka 1:1-17)
Nilipita hapa na pale kukunua ili kukunua mashine ya kudurufu na nikaona watu wengi walikuwa wametingwa wakijaribu kutafuta kitu kitakacho waridhisha. Walikuwa ni watu maskini kiroho pamoja na kuwa walikuwa wakiishi katika wakati huu ambapo ulimwengu huu umejaa vitu na utajiri. Walionekana kama vile watu wanaozunguka jangwani wakitafuta njia ya kuwawezesha kupata bilauri ya maji kwa sababu ya kiu kali. Kwa kweli kimtazamo walikuwa ni watu matajiri, wa kimwili, na wa kidunia, lakini kwa kweli nilipoziangalia nafsi zao nilihisi wakionekana maskini na waliotengwa. Kwa kuwatazama kwa macho yangu, walikuwa ni watu waliokuwa wakipigana na kifo kwa sababu walikuwa wamepigwa na umaskini na njaa katika roho zao; walikuwa ni watu waliokuwa wakifa kwa sababu ya njaa kali ya kiroho. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Mon, 23 Jan 2023 - 1h 00min
Podcast simili a <nome>
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Espacio en blanco Radio Nacional
- Les Grosses Têtes RTL
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR