Podcasts by Category
Mahubiri kupitia Wagalatia - KUTOKA TOHARA YA MWILI HADI MAFUNDISHO YA TOBA (II)
Mafundisho ya Toba Yanatosha Kukufanya Upate Ugonjwa wa Kiroho. Ulimwenguni kote watu wanaogopa virusi kama vile vya SARS kwa kuwa wanaweza kufa kutokana na kuambukizwa na virusi hivyo visivyoonekana. Vivyo hivyo, Wakristo wengi siku hizi ulimwenguni kote wanakufa kimwili na kiroho kutokana na kuathiriwa na mafundisho ya toba. Ni nani ambaye alifahamu jinsi mafundisho ya toba yalivyo potofu kiasi hicho? Unafahamu ni nani aliyewafanya Wakristo kuangukia katika mkanganyo wa kiroho? Ni Wakristo wenye dhambi wenyewe ambao wanaendelea kutoa sala za toba kila siku ili waweze kuzisafisha dhambi zao binafsi huku wakidai kuwa wanamwamini Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wao. Hivyo unapaswa kupokea ondoleo la dhambi zako kwa kuliamini Neno la injili ya maji na Roho ambalo kwa asili ndilo ambalo Mungu alitupatia. Haupaswi kuipoteza nafasi hii yenye baraka ya kuweza kuzaliwa tena upya. Sisi sote tunapaswa kukombolewa toka katika mkanganyo wa kiroho kwa kuuamini Ukweli wa injili ya maji na Roho. Tunapaswa kuiangalia nuru ya Ukweli ambayo ilikuja kupitia injili ya maji na Roho, na nuru hiyo ilikuja baada ya kuyatoroka mashimo ya mkanganyo wa kiroho. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
- 16 - SURA YA 4-1. Sisi Ndio Hatutaweza kuonja Mauti kamwe, Tutafurahia Maisha ya Milele (Wagalatia 4:1-11)
Mtume Paulo alisema katika Wagalatia 4:1,Sasa nasema kwamba mrithi,maadamu ni motto,hana tofauti kabisa na mtumwa, ingawa ni Bwana wa wote.Imeandikwa kuwa ikiwa sisi ni wana wa Mungu,basi sisi ni warithi wa urithi wake,Sisi ni warithi wa Mungu,inamaanisha kuwa Mungu ameturuhusu kupata uzima wa kweli kwa kutupatia ondoleo la dhambi zetu mileleTunapaswa sote kufahamu umuhimu mkubwa wa kile Mtume Paulo anasema hapa na kuamini kwa mioyo yetu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 27min - 15 - SURA YA 4-2. Je! Wewe na Mimi Tuna Imani Sawa na Ile ya Abraham? (Wagalatia 4:12-31)
Masharti kama vile kujitengenezea Wakristo au kanisa lenye watu watu wengi,linaloonekana kuwa maarufu sana,haswa miongoni mwa jamii za Wakaristo wa Dunia ya Tatu.Wanajaribu kubadilisha ukristo wa Magharibi kuwa aina moja ambayo inaambatana zaidi na tamaduni zao.Wanasisitiza sana kifungu cha pili cha uhasama wa jadi,Umoja katika mambo muhimu,uhuru katika vitu visivyo vya msingi na hisani katika mambo yote.Lakini jambo la bahati mbaya ni kwamba hawajua mambo muhimu ni yapi au ni nini.Walakini,injili ya maji na Roho iliyoenezwa na sisi haiwezi kudhihirishwa katika hali tofauti nay ale yaliyomo katika injili hii.Na hivyo haiwezi kubadilika kwa hali yoyote.Ninamshukuru Mungu kwa kweli maana ninaweza kuwahubiria injili ya maji na Roho ambayo inaweza kukuokoa kutoka katika dhambi zako zote chini ya hali yeyote.Kwa hviyo,niko tayari kufanya kazi hii ya haki mpaka siku ile Bwana wetu atakaporudi.Ninaamini kwamba roho nyingi zitaachiliwa kutoka katika dhambi zao zote kwa kuamini injili ya maji na Roho.Ninjua pia kitabu hiki kitakuwa na faida kwako kabisa. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 1h 06min - 14 - SURA YA 4-3. Usigeukie Tena Mambo Dhaifu na yenye Unyonge Ya Ulimwengu (Wagalatia 4:1-11)
Paulo aliandika barua hii takriban miaka 2000 iliyopita. Mambo haya hurejea kanuni za msingi za Sheria, kuishi maisha ya kisheria ya imani kulingana na Sheria. Wayahudi walizoea kujifunza kila kitu kwa yeshiva. Mtume Paulo mwenyewe pia alifundishwa chini ya mwalimu maarufu aliyeitwa Gamalieli na kufundishwa kumcha Mungu kupitia Sheria. Ndio maana mtume Paulo aliita mambo kuwa bado yamefungwa na Sheria, kujifunza Sheria, na kufuata Sheria hata baada ya kuja kwa Yesu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 45min - 13 - SURA YA 4-4. Sisi ni Warithi wa Mungu (Wagalatia 4:1-11)
Mtume Paulo alisema kuwa ingawa watakatifu na wahudumu wote ni warithi wa Mungu ambao watarithi Ufalme wake, wakati wanaishi hapa duniani, sio tofauti na watumwa na wako chini ya wasimamizi kwa muda, na kwamba wanateseka chini ya mambo ya ulimwengu kwa muda mfupi. Alisema, "Ingawa tunaishi kama watumwa katika ulimwengu huu kwa muda mfupi, tusisahau kuwa sisi ni wana wa Mungu ambao tutarithi utajiri wote wa Mungu Baba." Ujumbe huu haukuzungumzwa tu kwa watumishi wa Mungu na watu wake wote wakati huo, lakini pia unasemwa kwetu pia leo. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 22min - 12 - SURA YA 5-1. Kaa Ndani Ya Kristo Ukitegemea Injili ya Maji na Roho (Wagalatia 5:1-16)
Mtume Paulo alisema katika Wagalatia 2:20, Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai;wala si mimi tena,bali Kristo yu hai ndani yangu. ikiwa tunaamini katika Neno hili, ya kwamba tumesulubiwa na Kristo na Yeye anaishi ndani yetu, basi tumekwisha kufa katika yeye, na Bwana wetu anakaa na anaishi ndani yetu. Kristo alichukua dhambi zote tunazotenda hapa duniani, kutoka katika dhambi zetu za zamani hadi dhambi hizi za sasa na za baadaye, kupitia Ubatizo aliopokea kutoka kwa Yohana Mbatizaji, na alikufa Msalabani na kufufuka kutoka kwa wafu tena. Sasa, kama Bwana wetu anaishi ndani yetu, kwa njia hiyo ametuwezesha kuimba zabuni na raha zake kila wakati. Bwana wetu ameishi mioyoni mwetu kama Roho Mtakatifu, na anatuongoza sote. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 42min - 11 - SURA YA 5-2. Athari ya Imani, Kufanya Kazi Kupitia Upendo (Wagalatia 5:1-6)
Katika Wagalatia sura 5 mtari wa 1, inasema, Kwa hiyo simameni,wala msinaswe tena chini ya konwa la utumwa. Kifungu hiki kinatuambia tusiipokee tohara ya mwili inayoturudisha kuwa watenda dhambi, kwa sababu Yesu Kristo alikuja kutuokoa kutoka katika dhambi. Bwana wetu ametufanya kuwa watoto wa Mungu kwa kutuokoa kutoka katika dhambi za ulimwengu huu kwa injili ya maji na Roho. Kwa kweli Bwana ametupa wokovu wa kweli na uhuru wa kweli kwa wale tunaoamini injili ya maji na Roho. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 46min - 10 - SURA YA 5-3. Kuishi Kwa Matakwa Ya Roho Mtakatifui (Wagalatia 5:7-26)
Kuna wakristo wengi wakati huu ambao bado hawajasamehewa dhambi zao, kwa kuwa hawajapokea injili ya ondoleo la dhambi ambayo imekuja na injili ya maji na Roho, na wanabaki wakikamatwa na mafundisho wakristo wa uwongo.Kwa hivyo, kupitia Kitabu hiki cha Wagalatia, napenda kuwaonya kwa kuwa wanakabiliwa na uharibifu wa kiroho kwa sababu ya fundisho la sala za toba ambalo wamekuwa wakifuata. Ninahisi hivyo isipokuwa nichukue fursa hii kuweka wazi jambo hili, hakutakuwa na fursa nyingine ya kusahihisha imani yao potofu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 47min - 9 - SURA YA 5-4. Matakwa ya Roho Mtakatifu na yale ya Mwilini (Wagalatia 5:13-26)
Katika aya na maandiko ya leo, Mtume Paulo alisema, Tembea kwa Roho. Je! Inamaanisha nini kwetu kuzaliwa mara ya pili kwa kufuata matakwa ya Roho mbele za Mungu? Ni kuishi aina ya maisha yanayompendeza Mungu kama, kuhubiri injili ya maji na Roho kwa roho zingine ili waweze pia kupokea ondoleo la dhambi zao.Kinacholeta matakwa ya Roho ndani yetu na kutufanya tuishi kulingana na shauku hii ni imani yenyewe iliyowekwa katika injili ya maji na Roho. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 47min - 8 - SURA YA 5-5. Tembea Katika Matakwa Ya Roho (Wagalatia 5:16-26)
Katika kifungu cha maandiko cha leo, mtume Paulo anafafanua kazi za mwili na tunda la Roho Mtakatifu kwa kuzitofautisha dhidi ya kila mmoja. Kwanza kabisa, Paulo anasema kwamba kazi za mwili zinaonekana, halafu anaendelea kuorodhesha kama ifuatavyo: “Uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira , fitina,faraka,uzushi, wivu, husuda,ulevi, ulafi, na mambo yafananayo na hayo. "Kisha Paulo anafafanua matunda ya Roho, akisema, "Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema fadhili,uaminifu, upole,kiasi;Juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 37min - 7 - SURA YA 5-6. Matunda ya Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:15-26)
Katika kifungu cha maandiko cha leo, mtume Paulo alizungumza juu ya maisha ambayo humfuata Roho Mtakatifu, na maisha ambayo hufuata mwili. Tuna tabia hizi zote mbili, sawa? Walakini, kama wenye haki, kile tunachowaza na kutamani ni kuzaa matunda ya Roho Mtakatifu maishani mwetu. Imeandikwa, "Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, fadhili, utu wema, uaminifu, upole, kiasi. Juu ya mambo hayo hakuna sheria (Wagalatia 5: 22-23). Kuna matunda tisa ya Roho yaliyoorodheshwa hapa, na Bwana alituambia kuwa kila wakati tuzae matunda haya ya Roho katika maisha yetu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 22min - 6 - SURA YA 5-7. Usiishi kwa Utukufu Usio na Maana, Bali Tafuta Ufalme wa Mungu (Wagalatia 5:16-26)
Mara tu ukiangalia Wagalatia, tunaweza kuona kwamba kulikuwa na maeneo fulani ambayo mtume Paulo alipambana sana, akishawishiwa na imani ya waovu, kulikuwa na wengi katika makanisa ya Galatia ambao walidanganywa na mafundisho ya uwongo kwamba mtu alilazimika kumwamini Yesu Kristo kama Mwokozi kwa kupata tohara ili aokolewe. Alipata shida kwa sababu injili ya maji na Roho ingeweza kupotoshwa na waliotahiriwa ambao walikuwa wakifundisha kwamba kutahiriwa kwa mwili ndio kitu sahihi. Mtume Paulo alijitahidi sana kusahihisha imani ya wale waliopotoshwa. Kwa hivyo, aliwaonya wale waliotahiri kwa kusema, Msiwafundishe hivyo. Utalaaniwa na Mungu ikiwa unaamini na unashuhudia hivyo. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 48min - 5 - SURA YA 6-1. Shiriki Katika Kazi Zote Njema Za Mungu (Wagalatia 6:1-10)
Je! ulikuwa na chakula cha jioni kizuri? Hii ni mara ya kwanza kwamba hatujafanya sherehe zozote za michezo wakati wa kufanya mikutano yetu ya uamsho. Wahudumu wetu na mimi walikuwa wamechoka sana na walichoka sana mara tu baada ya kuingia kwenye vyumba vyetu, tulianguka na tukalala. Labda sote tulichoshwa sana na tulihisi uchovu sana katika miili na roho siku hizi kutokana na kufanya bidii sana kutumikia Injili. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 59min - 4 - SURA YA 6-2. Lazima Tutupilie, Mbali Imani Ya Sala za Toba na Kutambua Kuwa Ni Uwongo (Wagalatia 6:1-10)
Nimeshughulikia maswala kadhaa katika Wagalatia hadi sasa, lakini kushughulikia Kitabu cha Wagalatia kwa undani zaidi, bado ninahitaji kutoa mahubiri zaidi. Ni kwa sababu Neno katika Wagalatia lina mengi sana na masomo ya kiroho ambayo lazima yashughulikiwe. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 51min - 3 - SURA YA 6-3. Hebu Tumtumikie Mungu Kwa Kubebeana Mizigo Yetu Kila Mmoja (Wagalatia 6:1-10)
Kifungu cha Maandiko cha leo kinasema Ndugu zangu,mtu akighafilika katika kosa lolote,ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole,Mtu ameghafilika kwa kosa lolote, tunapaswa kurejesha watu kama hao kwa roho ya upole, na tukajichunguze. Kwanza lazima tuchunguze imani yetu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 44min - 2 - SURA YA 6-4. Bwana Ametuokoa Sio Kwa Damu Yake tu Msalabani, bali Kupitia Injili Ya Maji na Roho (Wagalatia 6:11-18)
Jioni hii, katika Neno la Mungu kutoka Wagalatia 6: 11-18, ningependa kushiriki neema za Bwana nanyi. Kama tulivyoona hivi sasa katika Neno, na vile vile katika kifungu hiki, tunaweza kuona tena jinsi waasi walivyolitupa Kanisa la Mungu katika machafuko makubwa ya kiroho, na jinsi mtume Paulo alivyopata shida kubwa mikononi mwa walanguzi aliokuwa nao. Tuje kwenye haya makanisa ya Galatia,Ndio maana Paulo alikasirika.Mtume Paulo kwanza aliwaonyesha watu wa tohara nia na siri. Sababu zilizowafanya kutetea tohara ya mwili zilikuwa ni tatu: Kwanza, ni kupitishwa na Wayahudi; pili, kuzuia kuteswa na watu wao; na ya tatu, kujivunia imani yao. Ndio sababu Paulo alisema katika Wagalatia 6: 12-13, "Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili,ndio wanaowashurutisha kutahiriwa;makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo,hilo tu.Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria;bali wanataka ninyi mtahiriwe,wapate kuona fahari katika miili yenu. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 1h 00min - 1 - SURA YA 6-5. Hebu na Tuhubiri Injili ya Maji na Roho Kwa Ufahamu Sahihi (Wagalatia 6:17-18)
Katika sehemu ya mwisho ya Wagalatia, mtume Paulo alisema haswa, Tangu sasa mtu asinitaabishe;kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu. (Wagalatia 6:17). Alichomaanisha Paulo hapa ni kwamba watu hawapaswi kujaribu kupokea ondoleo la dhambi kupitia imani yao batili, wala kudai kuwa hawana dhambi. Alisema kwamba hakuna mtu anayepaswa kumsumbua tena, haswa kwani alielezea vya kutosha jinsi ilivyo imani potofu kwa walanguzi kujaribu kuwa watu wa Mungu kwa kutahiriwa. Kwa maneno mengine, Paulo aliwaambia wasimpe uzito au kumtoa nguvu kwa imani hizo mbaya. https://www.bjnewlife.org/https://youtube.com/@TheNewLifeMissionhttps://www.facebook.com/shin.john.35
Sun, 15 Jan 2023 - 39min
Podcasts similar to Mahubiri kupitia Wagalatia - KUTOKA TOHARA YA MWILI HADI MAFUNDISHO YA TOBA (II)
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Espacio en blanco Radio Nacional
- Les Grosses Têtes RTL
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR