Podcasts by Category

MAISHA: Toleo la Kiswahili

MAISHA: Toleo la Kiswahili

Koleman Thompson

Karibu kwenye podcast yangu, MAISHA: Swahili Edition! Dhumuni la podcast hii ni kuzungumzia safari zetu za maisha na mambo ambayo tumepitia na kujifunza. Kwa majina naitwa Koleman Thompson. Nililelewa katika jingo la Utah, Marekani. Nilijifunza Kiswahili nilipotumikia kama Mmisionari kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Pia, nina podcast nyingine inayoitwa “MAISHA: English Edition”. Ukitaka kusikiliza kuhusu maisha ya watu waongeao Kiingereza, utafute hiyo podcast. Asante sana kwa kusikiliza!

7 - Lizbeth Leonard | Maisha ya Vijana wa Tanzania
0:00 / 0:00
1x
  • 7 - Lizbeth Leonard | Maisha ya Vijana wa Tanzania

    Lizbeth Leonard ni mtu mzuri sana ambaye anampenda Mungu na familia yake sana. Nilibarikiwa sana kuishi na yeye na familia yake wakati ambao nilikuwa Tanzania. Aliboresha maisha yangu sana kwa mfano na maneno yake. Kwenye kipindi hiki, tulizungumza sana kuhusu maisha ya vijana wa Tanzania (ikijumuisha umuhimu wao, changamoto zao, na utatuzi kwa changamoto zao). Natumaini kwamba wengine watafaidika kutokana na mazungumzo haya.

    Sun, 25 Aug 2024 - 53min
  • 6 - Mwalimu Vinold John | Utamaduni na Lugha ya Waswahili

    Vinold John ni mwalimu bora kabisa na nimefurahi kujifunza kutoka kwake mara kwa mara kwenye progamu hii hapa Tanzania. Anapenda sana kufundisha kuhusu utamaduni na lugha ya Waswahili. Katika kipindi hiki, tulizungumza mawili matatu kuhusu mada hizo, pamoja na umuhimu wa subira katika maisha yetu. Furahie! Ukitamani kujifunza kutoka kwa mwalimu Vinold, unaweza kumkuta kwa njia zifuatazo: Email - vinoldjohn@gmail.com Whatsapp - +255 756 704 834 Podcast - Bonga Language School Instagram - bonga_language_school

    Thu, 15 Aug 2024 - 56min
  • 5 - Erick Mwasha | Kuishi Maisha ya Furaha

    Jiunge na mimi na Rafiki yangu Erick tukizungumzia masuala makubwa ya maisha kama vile umuhimu wa kuwasaidia watu wengine, changamoto za maisha katika Tanzania, na kuishi vizuri na wengine!

    Thu, 08 Aug 2024 - 1h 22min
  • 4 - Fredrick Charles | Maana ya Maisha na Umuhimu wa Amri za Mungu na Mpango Wake

    Katika kipindi hiki, Fredi na mimi tulizungumzia maana ya maisha kidini na kijamii. Fredi ni rafiki yangu mpya hapa Tanzania. Yeye ni mtu mwema sana na ana mawazo mazuri mengi kushiriki. Anapenda Mungu sana na pia anafuatilia mambo ya siasa na mpira. Tuliongea kuhusu mpango wa Mungu na umuhimu wa kupenda wengine katika maisha yetu. Alisimulia matokeo machache ya maisha yake pia. Mfurahie!

    Fri, 19 Jul 2024 - 1h 18min
  • 3 - Grace Neema Lubango | Majaribu Magumu ya Maisha na Tofauti Kati ya Maisha ya Tanzania na Marekani

    Grace Neema Lubango ni rafiki yangu mwema. Alilelewa Tanzania na akahamia Marekani miaka kadhaa iliyopita. Katika kipindi hiki tulizungumzia sana tofauti kati ya maisha yake Tanzania na maisha yake Marekani. Aliweza kutoa ushauri mzuri sana. Pia, aligusia sana majaribu magumu ambayo amepitia maishani mwake na jinsi alivyoweza kumkaribia Mungu katika majaribu hayo. Nafiriki mtafaidika sana kwa kusikiliza. Na pia, Grace anapanga kuanzisha podcast mwenyewe ambayo itaitwa “Conversations with Miss Grace.” Napendekeza sana mtafute hiyo podcast baadaye ili kusikiliza mazungumzo mengine ambayo atakuwa nayo. Asante

    Wed, 12 Jun 2024 - 1h 02min
Show More Episodes