Filtrer par genre
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
- 241 - Shindano la filamu kwa kutumia simu ya Mkononi na msanii kutoka Mombasa Rojo Mo
Karibu katika makala changu chako chako changu Jumapili yaleo ambapo tutakijita zaidi kwenye matokeo ya shindano la kutengeneza filamu kwa kutumia simu ya mkononi liliooandaliwa na Alliance Francaise ya Nairobi nchini Kenya na kwenye Muziki tutakuwa naye msanii kutoka Mombasa Rojo Mo. Mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu, restons ensemble mwanzo hadi tamati, yaani tubaki pamoja mwanzo hadi mwisho.
Sat, 09 Nov 2024 - 240 - Alliance Francaise ya Nairobi inavyoikuza sanaa ya uigizaji jukwaani sehemu ya kwanza.
Katika Makala haya Ali Bilali amejielekeza Alliance Francaise ya Nairobi ambayo imeandaa Onyesho la Kwanza la tamthilia ya ‘Mgonjwa Mwitu’, utayarishaji wao wa kila mwaka wa maigizo yaliyotolewa na tamthilia za waandishi mashuhuri wa Ufaransa. Kwa maadhimisho ya miaka 75, chaguo ni 'Le Malade Imaginaire' na Molière. Hii ni comedy ya mwisho kuandikwa na Molière.
Ingawa ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mnamo 1673, kichekesho hiki cha kejeli, mojawapo ya bora zaidi za Moliere, hakijapoteza mvuto wake wa dhati na wa ulimwengu wote.
Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako @billy_bilali kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali
Mon, 04 Nov 2024 - 239 - Fahamu hapa kuhusu liliokuwa soko la watumwa nchini DRC Oct 20 2024
Karibu katika Makala Changu Chako Chako Changu, ambapo Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu ameungana na Denise Maheho kutoka Lubumbashi kuzungumzia kuhusu iliokuwa barabara ya watumwa zama za ukoloni.
Kumbuka pia kutuachia comment na kumfollow mtangazaji wako asiependa makuu @billy_Bilali kwenye mitandao yake ya kijamii Instagram na facebook.
Mon, 04 Nov 2024 - 238 - Utamaduni wa ndoa kulingana na kabila la Wameru sehemu ya pili Oct 13 2024
Ali Bilali ndio jina langu tunakutana tena Jumapili hii katika makala Changu Chako Chako Changu ambapo nakuletea sehemu ya pili ya Makala kuhusu Utamaduni w andoa kulingana na kabila la Wameru, kwenye le parler francophone nitakupa ratiba ya shughuli kwenye vituo vya Alliance Francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki tutamaliza na kibao Pambe chake Christian Bella kutoka huko nchini Tanzania, Karibu ama Bienvenue.
Sun, 13 Oct 2024 - 237 - Utamaduni wa watu wa Kabila la Wameru kutoka nchini KenyaSun, 06 Oct 2024
- 236 - Utamaduni wa ndoa kabila la wamakonde na wahangaza kutoka nchini Tanzania sehemu ya 2
karibu, Jumapili nyingine kuwa nami katika Makala Changu Chako Chako Changu Makala ambayo hukuletea Historia na utamaduni wa mambo mbalimbali, le Parler francophone na Muziki. Wiki iliopita nilikuletea Utamaduni wa ndoa kutoka makabila ya Wamakonde na wahangaza, ambapo leo nakuletea sehemu ya pili. Na kwenye le parler francophone nitakuletea ratiba za shughuli za kitamaduni kutoka Alliance francaise ya Nairobi na Dar es salaam, Tutamaliza na Wimbo wa Ibrah kutokz Tanzania
Sun, 29 Sep 2024 - 235 - Utamaduni wa watu wa makabila ya wahangaza na wamakonde kutoka nchini Tanzania
Katika makala haya, mtangazaji wako Ali Bilali amezungumza na Amua Rushita kutoka Mkoa wa Mtwara pamoja na Hilali Alexanda Ruhundwa kutoka Mkoa wa Kagera Wilaya ya Ngara nchini Tanzania kuzungumzia utamaduni wa ndoa kulingana na makabila hayo mawili. Kumbuka pia nawe unaweza kushiriki moja kwa moja studio au kwa njia ya simu. Wasiliana na mtangazaji wako asiependa makuu kufahamu zaidi.
Sun, 22 Sep 2024 - 234 - Toleo la 11 la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon kutolewa huko Benin
RFI inaandaa toleo la kumi na moja la Bourse Ghislaine Dupont na Claude Verlon, kwa heshima kwa waandishi wake wawili waliouawa kaskazini mwa Mali Novemba 2, 2013. Bourse hii, ambayo huwafunza waandishi wa habari vijana kumi wa redio na mafundi vijana kumi wa kuripoti kila mwaka, iko wazi. kwa wagombea kutoka nchi zote za Afrika zinazozungumza Kifaransa. Mafunzo hayo yatafanyika Cotonou. Maombi yamefunguliwa hadi Jumapili Agosti 25 saa sita usiku saa za Paris.
Mon, 26 Aug 2024 - 233 - Changu Chako Chako Changu: Utamaduni wa mahari kwa baadhi ya makabila barani AfrikaMon, 26 Aug 2024
- 232 - Changu chako chako changu Tasnia ya ulimbwende sehemu ya piliTue, 13 Aug 2024
- 231 - Changu Chako Chako Changu tasnia ya ulimbwende sehemu ya kwanza Agost 04 2024
Karibu katika makala changu chako chako changu, makala ambayo hukuletea mambo mbalimbali ya utamaduni, le parler francophone na Muziki, ambapo leo nakuletea sanaa ya Ulimbwende au Model, na kwenye la parler francophone nitakuletea shughuli zinazoendelea kwenye vituo vya Alliance francaise za ukanda kipindi hiki cha michuano ya Olympiki, mimi ni Ali Bilali Bienvenue.
Sun, 04 Aug 2024 - 230 - Historia ya kabila la Wabukusu pamoja na sanaa ya muziki kutokea kwa Bendi ya An Noor
Karibu kwenye makala ya changu chako ,chako changu juma hili ukiwa nami Florence Kiwuwa. Na kwenye kipengele cha historia hii leo tutaangazia historia ya kabila la Waluhya wanaofahamika kama wabukusu kisha kwenye kipengele chetu cha pili cha LeParle Francophone tutaangazia maonyesho ya Taarab yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Alliance France kisha tutamalizia na mwanamuziki wa Kenya almarufu kama Freshely Mwamburi.
Sun, 21 Jul 2024 - 229 - Matumizi ya lugha ya kiswahili katika enzi ya Kijiditali
Kiswahili kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 200 afrika mashariki na kwenye makala haya ya changu chako,chako changu ,Florence Kiwuwa amefanya majadiliano na wanafunzi katika chuo kikuu cha Multmedia ili kujua kuhusu mchango wa lugha hii katika kuendeleza utamaduni na utengamano na vilevile katika kipengele cha muziki amemuangazia mwanamuziki wa Tanzania Harmonize.
Tue, 16 Jul 2024 - 228 - Changu Chako Chako Changu maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 14 ya RFI Kiswahili
Karibu katika Makala Changu Chako Chako Changu jumapili ya leo ambapo nakulrtea Makala maalum kuhusu maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 14 tangu Ple RFI Kiswahili ilipoanza kupeperusha matangazo yake mubashara kutoka nchini Tanzania ambapo ilikuwa idhaa ya kwanza ya Kimataifa kutangaza ikiwa Afrika mashariki. Na kwenye Muziki nitakuletea Burudani ya Muziki wa Idd Aziz Kiswahili kitukuzwe wakati huu tukielekea kuadhimisha siku ya Kiswahili duniani. Mimi naitwa Ali Bilali, Bienvenue ama Karibu.
Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako Ali Bilali kwa kubonyeza hapa @billy_bilali
Sun, 07 Jul 2024 - 227 - Changu Chako Chako Changu, maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa DRCSat, 06 Jul 2024
- 226 - CHANGU CHAKO CHAKO CHANGU HISTORIA NA UTAMADUNI WA WATU WA KABILA LA WANUBI
Eid Mubaraka kwako mskilizaji wa RFI Kiswahili popopte pale ulipo ausubuhi hii. Karibu kuungana nami katika Makala haya Changu Chako Chako Changu. Leo nakuletea Historia ya watu wa Kabila la Wanubi, na kwenye Muziki nakupeleka nchini Burundi ambapo nazungumza na msanii wa kizazi kipya, Keypeacvaldiny. mimi ni Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu Karibu ama bienvenue.
Jina lake halisi ni Nzeyimana touré hamissi, anatumia jina la kisanii a @keypeac_valdyn amezaliwa April 8 mwaka 2002 jijini Bujumbura inchini burundi
Alianza muziki mwaka 2017, ila sababu ya harakati za masomo na familia alilazimika kuachana kabisa na muziki na kujikita zaidi na masomo. Baada ya kumaliza shule mwaka 2023 akaamuwa kurejea kwenye tasnia ya Muziki ambapo amekuja na EP yake iliowekwa hewani tangu April 15 mwaka 2024. EP yake hiyo ina nyimbo 3 ambazo ni:
Track n°1.carolina
Track n°2.sorry
Track n°3.mmmh
na songs hizo zote zipo kwenye platforms zake zote anapatikana kwa jina la @keypeac valdyn
yupo kwenye platforms zifwatazo kama : apple music, spotify, boomplay, youtube, rhapsody, deezer, amazon mp3, google play, shazam, tidal, tiktok, instagram, x , threads, na zingine.
Unaweza kumfollow mtangazaji wako Ali Bilali kwa kubonyeza hapa https://www.instagram.com/billy_bilali/
Sun, 16 Jun 2024 - 225 - Historia ya madaraka Day nchini Kenya na ziara ya Mistachampagne studio za RFI Kiswahili
Karibu katika makala ya leo changu chako chako changu ambapo leo nakuletea historia ya siku ya madaraka ambayo huadhimishwa kila Juni Mosi nchini Kenya. Na kwenye le parler francophone kama kawaida nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise za ukanda. Na Kwenye Muziki nitakuwa naye Mr Champagne msanii kutoka nchini Burundi ambaye yupo nchini Kenya kwa ajili ya kutangaza wimbo wake mpya Niko tu. Mimi ni Ali Bilali bienvenue ama karibu.
Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali
Tue, 04 Jun 2024 - 224 - Historia na utamaduni wa kabila la wanyakyusa sehemu ya piliThu, 30 May 2024
- 223 - Historia na Utamaduni wa wanyakyusa na muziki wa Kidum pamoja na Esther Nish
Furaha ilioje kukutana nawe Jumapili ya leo katika Makala Changu chako Chako Changu, ambayo hukuletea historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parler francophpone na Muziki ambapo leo nakuletea sehemu ya kwanza ya makala kuhusu historia ya Wanyakyusa, na kwenye Miuziki nitakuletea mwanamuziki Esthernish pamoja ni Kidum. Mimi ni Ali Bilali bienvenue. Ama Karibu.
Kumbuka pia kutufollow kwa Instagram @billy
Sun, 19 May 2024 - 222 - Sehemu ya makala kuhusu utamaduni wa waluo na waluhya hasa kwenye maswala ya ndoa
Karibu katika Makala haya changu chako chzako changu Jumapili ya leo ambapo nakuletea sehemu ya pili ya makala kuhusu tamaduni za wa Luhya na wa luo nchini Kenya ambapo sasa tutaangazia kuhusu tamadunbi za ndoa, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance francaise ya Nairobi na kwenye muziki nitakuletea mwanamuziki Mbosso kutoka nchini Tanzania. Mimi ni Ali Bilali Karibu.
Thu, 16 May 2024 - 221 - Utamaduni wa watu wa kabila la Waluo na Waluhya kutoka nchini KenyaSun, 05 May 2024
- 220 - Maoni ya washiriki katika kongamano la idhaa za kiswahili duniani sehemu ya mwisho
Ni jumapili nyingine tunakutana tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, utamaduni, le parler francophone na Muziki, na leo tunahitimisha mlolongo wa Makala kuhusu kongamano la idhaa za kiswahili duniani lililofanyika huko Mbeya, na kwenye le parler francophone nakuletea ratiba ya shughuli za kitamaduni kutoka Alliance Francaise ya Arusha na Nairobi, na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki King Kaka kutoka nchini Kenya.
Sun, 21 Apr 2024 - 219 - Sehemu ya tatu ya Makala kuhusu kongamano la nne la idhaa za Kiswahili duniani
Ni Jumapili nyingine tunakutana katika Makala Changu Chako Chako Changu, Makala ambayo hukuletea Historia ya mambo mbalimbali, Utamaduni, le parler francophone na Muziki, leo ninakuletea mazungumzo kuhusu ubidhaishaji wa lugha ya kiswahili, ikiwa ni kauli mbiu ya kongamano la nne za idhaa za Kiswahili Duniani lililofanyika mkoani Mbeya Mwezi Machi. Na kwenye le parler francophone nitakuletea mradi wa Creation Afrika unaonadaliwa na Allliance francaise ya Nairobi
Sun, 14 Apr 2024
Podcasts similaires à Changu Chako, Chako Changu
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- Tiempo de Juego COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Les Grosses Têtes RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR
Autres podcasts de Société et Culture
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- L'Heure Du Crime RTL
- Affaires sensibles France Inter
- Parlons-Nous RTL
- Les histoires incroyables de Pierre Bellemare RTL
- C dans l'air France Télévisions
- Au Cœur de l'Histoire Europe 1
- La libre antenne - Olivier Delacroix Europe 1
- Les Récits extraordinaires de Pierre Bellemare Europe 1 Archives
- LEGEND Guillaume Pley
- Les pieds sur terre France Culture
- Faites entrer l'accusé RMC Crime
- Choses à Savoir - Culture générale Choses à Savoir
- Héros RTL
- Libre antenne week-end - Valérie Darmon Europe 1
- CRIMES • Histoires Vraies Minuit
- Confidentiel RTL
- Choses à Savoir HISTOIRE Choses à Savoir
- Le Coin Du Crime La Fabrique Du Coin
- Hondelatte Raconte - Cote B Europe 1