Podcasts by Category

Changu Chako, Chako Changu

Changu Chako, Chako Changu

RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.

241 - Shindano la filamu kwa kutumia simu ya Mkononi na msanii kutoka Mombasa Rojo Mo
0:00 / 0:00
1x
  • 241 - Shindano la filamu kwa kutumia simu ya Mkononi na msanii kutoka Mombasa Rojo Mo

    Karibu katika makala changu chako chako changu Jumapili yaleo ambapo tutakijita zaidi kwenye matokeo ya shindano la kutengeneza filamu kwa kutumia simu ya mkononi liliooandaliwa na Alliance Francaise ya Nairobi nchini Kenya na kwenye Muziki tutakuwa naye msanii kutoka Mombasa Rojo Mo. Mimi ni Ali Bilali Bienvenue ama Karibu, restons ensemble mwanzo hadi tamati, yaani tubaki pamoja mwanzo hadi mwisho.

    Sat, 09 Nov 2024
  • 240 - Alliance Francaise ya Nairobi inavyoikuza sanaa ya uigizaji jukwaani sehemu ya kwanza.

    Katika Makala haya Ali Bilali amejielekeza Alliance Francaise ya Nairobi ambayo imeandaa Onyesho la Kwanza la tamthilia ya ‘Mgonjwa Mwitu’, utayarishaji wao wa kila mwaka wa maigizo yaliyotolewa na tamthilia za waandishi mashuhuri wa Ufaransa. Kwa maadhimisho ya miaka 75, chaguo ni 'Le Malade Imaginaire' na Molière. Hii ni comedy ya mwisho kuandikwa na Molière.

    Ingawa ilionyeshwa kwa mara ya kwanza mnamo 1673, kichekesho hiki cha kejeli, mojawapo ya bora zaidi za Moliere, hakijapoteza mvuto wake wa dhati na wa ulimwengu wote.

    Kumbuka pia kumfollow mtangazaji wako @billy_bilali kwenye mitandao ya kijamii @billy_bilali

    Mon, 04 Nov 2024
  • 239 - Fahamu hapa kuhusu liliokuwa soko la watumwa nchini DRC Oct 20 2024

    Karibu katika Makala Changu Chako Chako Changu, ambapo Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu ameungana na Denise Maheho kutoka Lubumbashi kuzungumzia kuhusu iliokuwa barabara ya watumwa zama za ukoloni.

    Kumbuka pia kutuachia comment na kumfollow mtangazaji wako asiependa makuu @billy_Bilali kwenye mitandao yake ya kijamii Instagram na facebook.

    Mon, 04 Nov 2024
  • 238 - Utamaduni wa ndoa kulingana na kabila la Wameru sehemu ya pili Oct 13 2024

    Ali Bilali ndio jina langu tunakutana tena Jumapili hii katika makala Changu Chako Chako Changu ambapo nakuletea sehemu ya pili ya Makala kuhusu Utamaduni w andoa kulingana na kabila la Wameru, kwenye le parler francophone nitakupa ratiba ya shughuli kwenye vituo vya Alliance Francaise ya Nairobi na Dar es salaam. Na kwenye Muziki tutamaliza na kibao Pambe chake Christian Bella kutoka huko nchini Tanzania, Karibu ama Bienvenue.

    Sun, 13 Oct 2024
  • 237 - Utamaduni wa watu wa Kabila la Wameru kutoka nchini Kenya

    Makala haya mtangazaji wako Ali Bilali anazungumzia kuhusu utamaduni wa watu wa kabila la Wameru kutoka nchini Kenya, wapo pia nchini Tanzania.

    Sun, 06 Oct 2024
Show More Episodes