Podcasts by Category
- 161 - Maaskofu wa kikatoliki nchini Kenya wakosoa utawala, Rwanda yamaliza Marbug
Maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya wameukosoa utawala wa Ruto, wataka kukomeshwa, utekaji nyara na ukiukaji wa haki za binadamu, wapinzani nchini DRC wajitokeza kupinga mpango wa kubadilisha katiba, Rwanda yafanikiwa katika mapambano yake dhidi ya ugoinjwa wa Murbag, kura ya maoni kuhusu katiba mpya kufanyika jumamosi nchini Gabon,Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa yaunga mkono ripoti kwamba Israel inatekeleza mauaji ya kimbari jijini Gaza
Sat, 16 Nov 2024 - 160 - Uchaguzi wa Marekani, mapigano DRC, kampeni za Raila kuwania uenyekiti wa tume ya AU
Donald Trump achaguliwa kuwa rais wa 47 wa Marekani, Ziara ya rais wa Kenya William Ruto huko Addis Ababa Ethiopia, na Sudan Kusini, na Raila Odinga kuzindua azma yake ya kuwania uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Februari mwaka 2025. Mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wazalendo mashariki mwa DRC, Umoja wa Mataifa wasema uamuzi wa kuahirishwa uchaguzi nchini Sudani Kusini haukubaliki, Duma Boko atawazwa rasmi kama rais mpya wa Botswana, Uhusiano wa Urusi na Marekani baada ya Trump kushinda uchaguzi
Sat, 09 Nov 2024 - 159 - Kithure Kindiki aapishwa kuwa makamu wa rais Kenya, ziara ya rais wa DRC nchini Uganda
Kuapishwa kwa makamu mpya wa rais wa Kenya Profesa Kithure Kindiki, ziara ya rais wa DRC Félix Tshisekedi Kampala Uganda huku mapigano kati ya waasi wa M23 na wazalendo yakiripotiwa mashariki mwa nchi yake, mkutano wa Comesa watamatika Jijini Bujumbura Burundi, Umoja wa mataifa wasema hali ya kibinadamu nchini Sudan yatia wasiwasi, upinzani washinda uchaguzi mkuu Botswana, kampeni za lala salama Marekani, lakini pia kauli ya Korea Kaskazini kuwa itasimama na Urusi hadi ushindi wake huko Ukraine.
Sat, 02 Nov 2024 - 158 - Rais Tshisekedi asema katiba ya Congo itarekebishwa, kesi ya naibu rais wa Kenya
Kauli ya rais wa DRC kuhusu marekebisho ya katiba yazua hisia mseto, kesi ya naibu wa Rais wa Kenya aliyeenguliwa madarakani Rigathi Gachagua yaendelea, umoja wa Ulaya kuendeleza shinikizo ilizoiwekea Burundi mwaka 2015 hadi mwaka 2025. Ziara ya mkuu wa UNHCR Fillipo Grandi nchini Uganda, mgombea wa chama tawala kule Msumbiji awa mshindi wa uchaguzi mkuu, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.
Sat, 26 Oct 2024 - 157 - Naibu rais wa Kenya Gachagua atimliwa, usalama wa mashariki ya DRC wajadiliwa Luanda
Kuondolewa madarakani kwa naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua na uteuzi wa profesa Kithure Kindiki, serikali ya Kinshasa yakaribisha makubaliano yaliyoafikiwa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa DRC na Rwanda kuhusu suala kulitokomeza kundi la FDLR na Rwanda kusema iko tayari kuwaondoa wanajeshi kwenye ardhi ya Congo, maandamano ya upinzani kule Msumbiji baada ya uchaguzi mkuu, kuuawa kwa kiongozi wa Hamas Yahya Sunwar, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.
Sat, 19 Oct 2024 - 156 - Mchakato wa kuondolewa madarakani naibu rais wa Kenya, mazishi ya waliokufa Goma
Wabunge 281 walipiga kura ya ndio kumwondoa naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua madarakani, mazishi ya watu waliokufamaji katika ajali ya Meli huko Goma DRC, ziara ya mkurugenzi wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika, Dr Jean Kaseya, nchini Rwanda kutathmini mikakati ya kupambana na mlipuko wa MPOX pamoja na marburg, mafuriko makubwa nchini Mali, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon, mchakato wa uchaguzi mkuu kule Marekani. Ungana na Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
Sat, 12 Oct 2024 - 155 - Mswada wa kumwondoa naibu rais wa Kenya Kachagua, watu zaidi 78 wafamaji DRC
Makala imeangazia mchakato wa kumwondoa madarakani naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua, makumi ya watu wafamaji katika ajali ya boti huko Goma mashariki mwa DRC, hali nchini Rwanda na ugonjwa wa murburg, Uganda na Sudan, siasa za Nigeria na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na yale ya Hezbollah nchini Israeli na mambo mengine.
Sat, 05 Oct 2024 - 154 - Lisu kuishitaki Tanzania kwa jaribio la kumuua, Kenya kupeleka polisi Haiti
Mwanasiasa wa upinzani kule Tanzania Tundu Lisu kuishitaki serikali na kampuni ya mawasiliano TIGO kwa jaribio la kumuua, rais wa Kenya William Ruto alisema polisi 2500 watapelekwa Haiti, wakati rais wa DRC Félix Tshisekedi atoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda kwa kuivamia nchi yake na kushirikiana na waasi wa M23, hali nchini Sudan, siasa za Senegal na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na mengineyo.
Sat, 28 Sep 2024 - 153 - Rais wa Tanzania Samia Suluhu na wanadiplomasia, msamaha kwa mkuu wa polisi Kenya
Makala hii imeangazia kauli ya rais wa Tanzania kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao ilivyozua gumzo katika uga wa kimataifa, msamaha wa mahakama kwa afisa mkuu wa polisi Kenya, ziara ya mjumbe wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu ulinzi wa amani Jean Pierre Lacroix huko DRC, UN kughadhabishwa na kuahirishwa uchaguzi wa sudan Kusini, jeshi Ia Israeli lashambulia Hezbollah kwa kulipua vifaa vyao vya mawasiliano na kwengineko duniani.
Sat, 21 Sep 2024 - 152 - Uchunguzi wa miili ya wanafunzi waliokufa Kenya, hali ngumu ya wakimbizi DRC na mengineyo
Ni wiki iliyoshuhudia matukio mengi miongoni ni pamoja na serikali ya Kenya kuendelea na uchunguzi wa mkasa wa moto uliowauwa wanafunzi, maandamano ya maelfu ya wakimbizi kwenye mji wa Goma mashariki mwa DRC wakiomba serikali iwarejeshe makwao na kumaliza vita, kule Senegal rais Bassirou alilivunja Bunge la taifa, na mdahalo wa kwanza wa televisheni kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na makamu wa rais Kamala Harris wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi wa Novemba na mengineyo.
Sat, 14 Sep 2024 - 151 - Mkutano wa 9 China na Afrika, miili200 yazikwa DRC, wanafunzi 17 wateketea Kenya.
Makala hii imeangazia mkutano wa tisa kati ya China na Afrika huko Beijing, wafungwa zaidi ya 100 waliuawa katika gereza la makala nchini DRC, Kenya na mkasa wa moto ulivyowaua wanafunzi Kaunti ya Nyeri, uchaguzi kufanyika nchini Tunisia, na nchini Ufaransa Michel Barnier aliteuliwa kuwa waziri Mkuu, miezi miwili baada ya mvutano wa kisiasa nchini Ufaransa, na mambo mengine kwengineko duniani.
Sat, 07 Sep 2024 - 150 - Kampeni ya Odinga kuwania uenyekiti tume ya AU, DRC yafungua kesi dhidi ya Rwanda
Uzinduzi wa kampeni ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, anayegombea unyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kongamano la 74 la WHO mjini Brazzaville, nchini Congo, DRC na Kampeni inayoitwa ICC Haki kwa DRC, hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini Sudan, shambulio la kigaidi Burkina Faso laua zaidi ya watu 300, hali nchini Israeli, na mchakato wa uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba
Sat, 31 Aug 2024 - 149 - DRC yaathirika na M-Pox, Raila asema siasa za Kenya, basi! na mengineyo
Tumeangazia katika makala ya wiki hii ni pamoja na ugonjwa wa Mpox ulitangazwa kuwa dharura ya kimataifa, DRC ikiathirika zaidi, nchini Kenya Raila Odinga kutojihusisha tena na siasa, jeshi la Uganda lilivamia na kuharibu kambi ya kundi la waasi la LRA huko Sudan pande hasimu zasusia mkutano wa Geneva, nchini Marekani, makamu wa rais Kamala Harris akubali uteuzi wa chama chake cha Democratic kuwa mgombea wa nafasi ya urais, na mengineyo
Sat, 24 Aug 2024 - 148 - Mpox yatangazwa janga la kimataifa la kiafya, mwanahabari wa Burundi Irangabiye aachiwa na mengineyo
Matukio ya dunia yaliyokithiri vichwa vya habari ni pamoja na virusi vya Mpox kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya huku bara la Afrika likiathiriwa zaidi, Burundi yamwachia mwanahabari aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10, tutaangazia siasa za Tanzania baada ya wanasiasa wa upinzani kukamatwa baadaye wakaachiwa, lakini pia hatua za mazungumzo kule Geneva kuhusu amani nchini Sudan.
Pia tutaangazia mgomo wa vyombo vya habari nchini Senegal kadhalika tutachambua wito wa Umoja wa Mataifa kutaka Afrika kupewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja huo
Kule Gaza, kundi la Hamas limekataa masharti 'mpya' ya upatanishi na Israeli na mazungumzo ya kupata mkataba wa kusitisha vita hivyo, kurejelewa tena wiki hii jijini Cairo, Misri.
Tue, 20 Aug 2024 - 147 - Tshisekedi amshutumu mtangulizi wake Kabila, serikali mpya Kenya na mengineyo
Makala ya Juma hili imeangazia hukumu iliyotolewa dhidi ya kiongozi wa chama cha waasi wa M23/AFC mashariki mwa DRC Corneille Nangaa, Rais wa Kenya aapisha baraza jipya la mawaziri miongoni mwao wanasiasa wa upinzani, mapigano ya nchini Sudan, maandamano nchini Nigeria na uongozi mpya wa mpito nchini Bangladesh baada ya kutoroka kwa waziri mkuu pia tumengazia yaliyojiri kwengineko duniani.
Sat, 10 Aug 2024 - 146 - Hamas yalaani mauaji ya kiongozi wake, mauaji ya kimbari DRC Genocost, na mengineyo
Makala hii imeangazia kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh nchini Iran, mazishi yake yalifanyika Doha, Urusi, mataifa ya Magharibi wabadilishana wafungwa, waziri mkuu wa DRC Judith Suminwa aongoza kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya wakongo maarufu, Genocost, yaliyojiri nchini Kenya, na mgomo wa wafanyabiashara wa Uganda, hukumu dhidi ya dikteta wa zamani wa nchini Guinea na kwengineko duniani.
Sat, 03 Aug 2024 - 145 - Michezo ya olimpiki yaanza Paris Ufaransa, Siasa za Kenya, DRC na kwengineko
Makala imeangazia hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Ijumaa ya wiki hii, huku miundombinu ya treni za umeme ikishambuliwa, rais William Ruto atangaza baraza la mawaziri akiwajumuisha wanasiasa wanne wa upinzani, kesi dhidi ya kiongozi wa muungano wa waasi Corneille Nangaa jijini Kinshasa nchini DRC, Maandamano na kukamatwa kwa vijana kule Uganda, siasa za Afrika Magharibi, na Kaskazini,Joe Biden ajijiondoa katika ki nyang’anyiro cha uchauguzi huku Kamala Harris akiteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Demokratic nchini Marekani.
Sat, 27 Jul 2024 - 144 - Ruto ateua mawaziri wapya, Paul Kagame ashinda uchaguzi, usalama bado mashariki DRC
Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto ya kuwateua mawaziri wapya baada ya mashinikizo, nchi yake ikishuhudia maandamano ya vijana, Kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji ya watu ambao miili yao ilikutwa jalalani Kware jijini Nairobi akiri kuwaua wanawake 42, rais wa Rwanda Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kishindo, Waasi wa M23 na jeshi la congo FARDC wakubali kusimamisha vita baada ya Marekani kutangaza kuongeza muda wa siku 15 kuruhusu misaada ya kibinadamu...na mengineyo..kwengineko duniani ambako watu wamestushwa ulimwenguni kuhusu hitilafu iliyojitokeza kiteknolojia..-
Sat, 20 Jul 2024 - 143 - Rais Ruto avunja baraza la mawaziri, uchaguzi huko Rwanda, usalama wazorota DRC
Makala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto kulivunja baraza lake la mawaziri, huku inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome akubali kujiuzulu, raia nchini Rwanda wajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini Rwanda jumatatu ya julai 15, pia hali ya mapigan yashuhudiwa nchini DRC licha ya wito wa Marekani wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu.Hali iliyojiri kwenye nchi za Afrika magharibi na kaskazini, Ufaransa, na Marekani.
Sat, 13 Jul 2024 - 142 - DRC: Wanajeshi wanaodaiwa kutoroka adui kwenye mapambano wahukumiwaSat, 06 Jul 2024
- 141 - Ruto asema hatasaini mswada wa fedha 2024, M23 wauteka mji wa Kanyabayonga
Makala hii imeangazia maandamano nchini Kenya huku rais Ruto akisema hatasaini mswada wa fedha wa 2024 uliokuwa umeidhinishwa na wabunge walio wengi, waasi wa M23 huko DRC walifanikiwa kuuteka mji wa kimkakati wa Kanyabayonga wilayani Lubero mashariki mwa DRC, mgomo wa wafanyabiashara nchini Tanzania, na nini hatima yake, siasa za Afrika kusini lakini pia mdahalo kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na Joe Biden kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, yaliyojiri nchini Ufaransa na kwengineko Duniani.
Sat, 29 Jun 2024 - 140 - Maandamano nchini Kenya kupinga mswada wa fedha 2024, hali ya usalama DRC
Makala imeangazia hatua ya wabunge wa Kenya kuidhinisha mswada wa fedha wa 2024 kuingia katika hatua ya pili kabla ya kupitishwa licha ya maandamano makubwa nchini, ziara ya rais Felix Tshisekedi huko Lubumbashi, na kuendelea kwa mapigano kati ya FARDC na waasi wa M23, Uganda yawasamehe waasi wa zamani wa ADF, kuapishwa kwa rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa, hali huko Afrika Magharibi, na kwengineko duniani
Sat, 22 Jun 2024 - 139 - Nchi za Afrika mashariki zawasilisha bajeti, serikali mpya DRC yazinduliwa
Tunayoangazia ni pamoja na kutangazwa kwa badgeti ya mwaka 2024/2024 kwenye nchi za jumuia ya Afrika mashariki, serikali ya mwanamke wa kwanza aliyeteuliwa kuwa waziri mkuu mpya huko DRC ilizinduliwa wiki hii, mauaji ya ADF huko Lubero mashariki mwa nchi hiyo, kifo cha makamu rais wa Malawi katika ajali ya ndege, lakini tutaangazia yaliyojiri Afrika Magharibi, kabla ya kuelekea kwengineko duniani
Sat, 15 Jun 2024 - 138 - Mapigano Kanyabayonga DRC, katibu mkuu mpya wa EAC, na mengineyo
Makala hii imeangazia mkutano wa viongozi wa afrika huko Korea Kusini, hali ya wasiwasi kutanda kwenye mji wa Kanyabayonga, na mashirika kadhaa ya misaada kuanza kuhama, Burundi na kampeni ya kuvunja ndoa zisizorasmi, hotuba ya rais wa Uganda Yoweri M7, siasa za nchini Kenya, juhudi za kimataifa kuhusu amani ya Sudan, hali ya kisiasa Afrika kusini baada ya uchaguzi, hali ya usalama huko Gaza na siasa za Marekani
Sat, 08 Jun 2024
Podcasts similar to Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Espacio en blanco Radio Nacional
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR
Other News & Politics Podcasts
- Les Grosses Têtes RTL
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Entrez dans l'Histoire RTL
- C dans l'air France Télévisions
- Laurent Gerra RTL
- L'œil de Philippe Caverivière RTL
- LEGEND Guillaume Pley
- On marche sur la tête Europe1
- Les récits de Stéphane Bern Europe 1
- Hondelatte Raconte - Cote B Europe 1
- Bercoff dans tous ses états Sud Radio
- L’heure du crime : les archives de Jacques Pradel RTL
- Enquêtes criminelles RTL
- La dernière Radio Nova
- Global News Podcast BBC World Service
- TOCSIN PODCAST TOCSIN MÉDIA
- Culture médias - Thomas Isle Europe 1
- L'Heure des Pros CNEWS
- Pascal Praud et vous Europe 1
- C ce soir France Télévisions