Filtra per genere

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

RFI Kiswahili

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

161 - Maaskofu wa kikatoliki nchini Kenya wakosoa utawala, Rwanda yamaliza Marbug
0:00 / 0:00
1x
  • 161 - Maaskofu wa kikatoliki nchini Kenya wakosoa utawala, Rwanda yamaliza Marbug

    Maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya wameukosoa utawala wa Ruto, wataka kukomeshwa, utekaji nyara na ukiukaji wa haki za binadamu, wapinzani nchini DRC wajitokeza kupinga mpango wa kubadilisha katiba, Rwanda yafanikiwa katika mapambano yake dhidi ya ugoinjwa wa Murbag, kura ya maoni kuhusu katiba mpya kufanyika jumamosi nchini Gabon,Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa  yaunga mkono ripoti kwamba Israel inatekeleza mauaji ya kimbari jijini Gaza

    Sat, 16 Nov 2024
  • 160 - Uchaguzi wa Marekani, mapigano DRC, kampeni za Raila kuwania uenyekiti wa tume ya AU

    Donald Trump achaguliwa kuwa rais wa 47 wa Marekani, Ziara ya rais wa Kenya William Ruto huko Addis Ababa Ethiopia, na Sudan Kusini, na Raila Odinga kuzindua azma yake ya kuwania uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Februari mwaka 2025. Mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wazalendo mashariki mwa DRC, Umoja wa Mataifa wasema uamuzi wa kuahirishwa uchaguzi nchini Sudani Kusini haukubaliki, Duma Boko atawazwa rasmi kama rais mpya wa Botswana, Uhusiano wa Urusi na Marekani baada ya Trump kushinda uchaguzi

    Sat, 09 Nov 2024
  • 159 - Kithure Kindiki aapishwa kuwa makamu wa rais Kenya, ziara ya rais wa DRC nchini Uganda

    Kuapishwa kwa makamu mpya wa rais wa Kenya Profesa Kithure Kindiki, ziara ya rais wa DRC Félix Tshisekedi Kampala Uganda huku mapigano kati ya waasi wa M23 na wazalendo yakiripotiwa mashariki mwa nchi yake, mkutano wa Comesa watamatika Jijini Bujumbura Burundi, Umoja wa mataifa wasema hali ya kibinadamu nchini Sudan yatia wasiwasi, upinzani washinda uchaguzi mkuu Botswana, kampeni za lala salama Marekani, lakini pia kauli ya Korea Kaskazini kuwa itasimama na Urusi hadi ushindi wake huko Ukraine.

    Sat, 02 Nov 2024
  • 158 - Rais Tshisekedi asema katiba ya Congo itarekebishwa, kesi ya naibu rais wa Kenya

    Kauli ya rais wa DRC kuhusu marekebisho ya katiba yazua hisia mseto, kesi ya naibu wa Rais wa Kenya aliyeenguliwa madarakani Rigathi Gachagua yaendelea, umoja wa Ulaya kuendeleza shinikizo ilizoiwekea Burundi mwaka 2015 hadi mwaka 2025. Ziara ya mkuu wa UNHCR Fillipo Grandi nchini Uganda, mgombea wa chama tawala kule Msumbiji awa mshindi wa uchaguzi mkuu, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.

    Sat, 26 Oct 2024
  • 157 - Naibu rais wa Kenya Gachagua atimliwa, usalama wa mashariki ya DRC wajadiliwa Luanda

    Kuondolewa madarakani kwa naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua na uteuzi wa profesa Kithure Kindiki, serikali ya Kinshasa yakaribisha makubaliano yaliyoafikiwa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa DRC na Rwanda kuhusu suala kulitokomeza kundi la FDLR na Rwanda kusema iko tayari kuwaondoa wanajeshi kwenye ardhi ya Congo, maandamano ya upinzani kule Msumbiji baada ya uchaguzi mkuu, kuuawa kwa kiongozi wa Hamas Yahya Sunwar, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.

    Sat, 19 Oct 2024
Mostra altri episodi