Podcasts by Category
- 160 - Wakaazi wa jimbo la Somaliland wapiga kura kumchagua rais na wabunge
Wakaazi wa jimbo la Somaliland, mojawapo wa êneo lililojitenga na Somalia zaidi ya miaka 30 iliyopita, tangu mwaka 2003 wamekuwa wakishiriki kwenye uchaguzi wa kumchagua rais na wabunge wao.
Fursa hiyo pia imekuja Novemba tarehe 13 mwaka 2024 ambapo wapiga kura Milioni 1 waliondikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Somaliland wanamchagua rais atakayewatumikia kwa miaka metano.
Wagombea watatu wanatafuta urais wa jimbo hilo, akiwemo kiongozi wa sasa Muse Bihi Abdi, anayetaka muhula wa pili, lakini mpinzani wake mkuu ni Abdirahman Mohamed Abdullahi, maarufu kwa jina la "Irro,”.
Kwenye Makala ya Wimbi la Siasa, tunajadili umuhimu wa uchaguzi wa jimbo la Somaliland na umuhimu wake, kwenye Jumuiya ya Kimataifa, wakati huu, êneo hilo linapotaka kujitawala.
Wed, 13 Nov 2024 - 159 - Msumbuji : Upinzani wakataa kutambua ushindi wa Daniel Chapo
Nchini Musumbuji maandamano yamekuwa yakishuhudiwa baada ya upinzani kukataa kutambua ushindi wa mgombea wa chama tawala Daniel Chapo.
Aliyekuwa mgombea wa upinzani Venancio Mondlane, amekuwa akisisitiza kwamba alipokonywa ushindi, katika makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Musumbiji.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa Lugete Mussa Lugete na Felix Arego wanafafanua hali nchini Msumbiji.
Tue, 05 Nov 2024 - 158 - Kenya : Bunge la Kenya lamuondoa naibu rais afisiniSat, 26 Oct 2024
- 157 - Mgogoro kati ya rais na naibu wake nchini Kenya ambao ni mzozo wa kihistoria
Hatma ya aliyekuwa naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua sasa utaamuliwa na mahakama baada ya mabunge yote mawili kumwondoa madarakani kwa njia ya hoja maalum
Hatua ya kuondolewa Gachagua ni dhihirisho ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya rais William Ruto na naibu wake Gachagua ,matukio ambayo si mageni nchini Kenya.
Wed, 23 Oct 2024 - 156 - Maadhimisho ya mwaka mmoja wa shambulio la Hamas huko Gaza Oktoba 7 2024
Makala wimbi la siasa inaangazia maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kundi la Hamas, litekeleze shambulio baya zaidi kuwahi kutekelezwa huko Israeli, tukio ambalo lilianzisha vita ambayo imesababisha vifo kwa maelfu ya raia wa Kipalestina na maandamano duniani kote kupinga vita hiyo, wakati huu mzozo huo ukihofiwa kuenea katika mashariki ya kati. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka na waalikwa wake
Wed, 09 Oct 2024 - 155 - Visa vya utekaji na mauaji ya wanasiasa wa upinzani Afrika Mashariki
Makala ya Wimbi la siasa inaangazia tukio la kutekwa na kuuawa, kwa wanasiasa wa upinzani kwenye nchi za Afrika mashariki,tukio la hivi punde likiwa ni kutekwa kwa mwanasiasa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema Ali Kibao, na baadaye alikutwa ameuawa, na matukio haya yanaripotiwa pia nchini Uganda na DRC. Ungana na Ruben Lukumbuka pamoja na waalikwa wake Jawadu Mohamed ni mchambuzi na mtaalamu wa siasa za Tanzania akiwa Daresalaam Tanzania, pia Frankline M wa CMD nchini Kenya.
Wed, 11 Sep 2024 - 154 - Mzozo wa Ethiopia na Somalia na mchango wa jumuiay aza kikanda kutuliza haliFri, 06 Sep 2024
- 153 - Amani ya Sudan bado kitendawili
Makala hii imeangazia hali ya kibinadamu inavyoendelea kuwa mbaya ndhini Sudan licha ya juhudi za kimataifa zinzoendelea.Nini kifanyike ili kufikia amani ya kudumu ya Sudan? kwa nini serikali imekataa kukaa meza moja na wapiganaji wa RSF? kuangazia hili, Ruben Lukumbuka anazungumza na Lugete Musa Lugete ni mchambuzi wa siasa za Kimataifa akiwa Tanzania, lakini pia Dismas Mokua mchambuzi wa masuala ya kisiasa akiwa Nairobi nchini Kenya
Wed, 28 Aug 2024 - 152 - Mchango wa Jumuiya ya nchi za SADC katika kutafuta suluhu ya mzozo wa DRC
Karibu katika Makala Wimbi la siasa ambapo tunazungumzia Mkutano wa 44 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika uliofanyika Harare, Zimbabwe ambapo viongozi walijadili changamoto zinazolikabili kanda hilo hususan usalama mashariki mwa DRC. Wachangiaji mada ni Alhaj Mali Ali akiwa Paris Ufaransa na Andulkarim Atiki akiwa Dar es salaam Tanzania.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekabidhiwa jukumu la Unyekiti wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.
Kumbuka kutufollow@billy_bilali
Thu, 22 Aug 2024 - 151 - Kauli ya rais Kagame kuhusu haja ya kuimarishwa kwa usalama wa kikandaWed, 14 Aug 2024
- 150 - Waasi wa M23 wauteka mji wa Ishasha licha ya sitisho la mapigano
Wiki hii askari wanaofikia 100 wa DRC, walikimbilia Uganda baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Ishasha ulioko mpakani na Uganda hali ambayo ilijiri wakati sitisho la mapigano lilikubaliwa kati ya DRC na Rwanda mjini Luanda Angola chini ya Upatanisho wa rais wa Angola Joao Laurenco. Kwa nini mapigano yanaendelea licha ya juhudi za kikanda na za kimataifa? Ruben Lukumbuka anazungumza na Francois Alwende, mchambuzi wa siasa za DRC akiwa Kenya, Jean Claude Bambaze, mwenyekiti wa mashirika ya kiraia wilayani Rutshuru akiwa Goma huko DRC.
Thu, 08 Aug 2024 - 149 - DRC : Yatangaza mpango wake wa kupunguza idadi ya wafungwa magerezaniSat, 03 Aug 2024
- 148 - Ufaransa : Macron afanikiwa kufungia mrengo wa kulia nje ya siasa za Ufaransa
Nchini Ufaransa licha ya mrengo wa kushoto kuibuka na ushindi kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge, duru ya pili ilikuwa kitendawili kwao baada ya vyama vya mrengo wa ksuhoto kushirikiana na kuzuia vyama vya mrengo wa kulia kupata ushindi.
Benson Wakoli anaangazia mbinu alaizotumia rais Emmanuel Macron kuvizuia vyama vya mrengo wa kulia kuibuka na ushindi.
Kumsaidia kuangazia hili anaye mchambuzi wa siasa za kimataifa Mali Ali , ambaye yupo Pari Ufaransa, pamoja na Lugete Mussa Lugete akiwa nchini Tanzania eneo la Mwanza.
Mon, 15 Jul 2024 - 147 - Kenya: Vijana watoa chanzo na suluhu ya ufisadi nchini mwao.Thu, 11 Jul 2024
- 146 - Uchaguzi wa wabunge nchini Ufaransa na mustakabali wa ulaya
Makala ya wimbi la siasa imeangazia uchaguzi wa wabunge nchini Ufaransa baada ya kufanyika kwa duru ya kwanza ya uchaguzi huo jumapili iliyopita na sasa duru ya pili imepangwa kufanyika julai 07.Uchaguzi huu unaweka wapi siasa za ufaransa, nini mustakabali wa kisiasa kwenye nchi hii, iwapo chama cha mrengo wa kulia cha National Rally kitaibuka mshindi?? Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi.
Wed, 03 Jul 2024 - 145 - Nini hatima ya maandamano yanayoendelea nchini Kenya ?
Siku ya Jumanne, Kenya ilishuhudia maandamano makubwa kupinga mswada tata wa sheria uliopitishwa na wabunge, kuongzeza kodi.
Waandamanaji wenye hasira, walivamia majengo ya Bunge jijini Nairobi na kusababisha uharibifu, huku polisi wakiwapiga risasi na kuwauwa waandamanaji.
Nini itakuwa suluhu ya mzozo huu ?
Tunachambua suala hili na Majeed Ali, mmoja wa vijana wanaounga mkono waandamanaji na Oponyo Akolo Eugene, kutoka Shirika la Wazalendo Movement Afrika, anayepinga maandamano.
Wed, 26 Jun 2024 - 144 - Kuapishwa kwa Cyril Ramaphona na mstakabali wa serikali mpya ya Afrika kusini
Makala hii inaangazia mchakato wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Afrika kusini, baada ya kuapishwa kwa rais Ramaphosa huku chama tawala ANC kikitangaza kufikia makubaliano na vyama vingine, kama DA. Kudadavua hili mwandishi wetu Ruben Lukumbuka anazungumza na Lugete Musa Lugete ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Jijini Daresalaam nchini Tanzania, pia Félix Nabel Arego, mtaalamu wa siasa wa siasa za Afrika kusini akiwa Nairobi Kenya
Fri, 21 Jun 2024 - 143 - Rwanda yaanza maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Julai 15 kumchagua rais na wabunge
Wananchi wa Rwanda wanajiandaa kupiga kura tarehe 15 mwezi Julai kumchagua rais na wabunge.
Wiki iiyopita, Tume ya Uchaguzi ilitangaza orodha ya awali ya wagombea urais ambao ni rais Paul Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1994, Frank Habineza kutoka chama cha Democratic Green na Philippe Mpayimana mgombea binafsi.
Mwanasiasa na mpinzani wa Kagame, Diane Rwigara, kutoka chama cha People Salvation Movement, ombi lake lilikataliwa.
Tunachambua maandalizi ya uchaguzi nchini Rwanda. Wachambuzi wetu ni Edwin Kegoli akiwa Nairobi na Mali Ali akiwa jijini Paris
Wed, 12 Jun 2024 - 142 - Chama tawala nchini Kenya, kwenye njia panda migawanyiko ikishuhudiwa
Nchini Kenya, malumbano ya kisiasa yameanza kushuhudiwa kati ya rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua, malumbano hayo yametokana na tofauti za kisiasa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027.
Kuna hofu kwamba wandani wa rais William Ruto wanawatumia wabunge vijana kutoka ngome ya naibu rais kumtatiza kisiasa hili likiibua malumbano makli ya kisiasa nchini Kenya.
Benson Wakoli hapa anachambua swala hili na mchambuzi wa siasa Felix Arego.
Fri, 31 May 2024 - 141 - Jaribio la mapinduzi nchini DRC lazua maswali mengi
Wimbi la siasa inaangazia kilichotokea Mei 19 jijini Kinshasa ambako vikosi vya jeshi la serikali (FARDC) viilidai kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya rais wa nchi hiyo.Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jumapili ya Mei 19, lakini sasa tukio hilo limeibua maswali mengi bila majibu. Kudadavua hili, utawasikia Georges Msamali, mtaalamu wa masuala ya kiusalama akiwa Nairobi nchini Kenya, Francois Alwende ni raia wa DRC na mtaalamu wa siasa za DRC.
Wed, 22 May 2024 - 140 - Wimbi la siasa: Madai ya Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu nchini Burundi
Kwenye Makala haya Ali Bilali akiwa pamoja na wachambuzi wa siasa Mali Ali kutoka Paris Ufaransa na Abdulkarim Atiki wanaangazi kuhusu tuhuma za Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu hususan uvurumishaji guruneti katika mji wa Bujumbura, tukio la hivi karibuni liligharimu maisha ya watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.
Fri, 17 May 2024 - 139 - Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi yaanza mazungumzo jijini Nairobi
Mazungumzo ya amani yanayohusisha makundi ya waasi nchini Sudan Kusini na serikali yameanza rasmi jijini Nairobi, wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi wa mwezi Disemba.
Makundi haya ni yale yaliosusia mkataba wa amani wa mwaka 2018, wakati rais Salva Kiiri na hasimu wa wake wa kisiasa ambaye sasa ni makamo rais wa Kwanza Reik Machar walisaini mkataba wa amani.
Soma piaKenya kuisaidia Sudan Kusini kupata suluhu ya utovu wa usalama wa miaka mingi
Katika makala haya Benson Wakoli na wachambuzi wa kisiasa Fracis Wambete, ambaye na mhadhiri wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda, pamoja na Abdulkarim Atiki, mchambuzi wa siasa za kimataifa kutoka nchini Tanzania wanajaribu kuangazia kufaulu kwa mazungumzo haya, skiza.
Fri, 10 May 2024 - 138 - Nini haki za wafanyakazi duniani ?
Kila tarehe 1, ni maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani. Wafanyakazi wanatumia siku hii kusherehekea mafanikio yao na kuendeleza mapambano ya haki zao. Je, siku hii ina umuhimu gani ? Wageni wetu ni Nice Mwansasu kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na mwanasheria wa masuala ya ajira kutoka Kenya Elvis Abenga
Wed, 01 May 2024 - 137 - Mwaka mmoja wa mapigano nchini Sudan kati ya jeshi la serikali na RSF
Wiki hii, ilikuwa ni mwaka mmoja wa vita nchini Sudan, kati ya jeshi la taifa chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa RSF wanaongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo.
Mwaka mmoja baadaye, vita vimeendelea na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, huku wengine Milioni 8.5 wakiyakimbia makaazi yao wakiwemo Milioni 1.8 waliokwenda kutafuta hifadhi katika nchi jirani kama Chad.
Wed, 17 Apr 2024
Podcasts similar to Wimbi la Siasa
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Espacio en blanco Radio Nacional
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR
Other News & Politics Podcasts
- Les Grosses Têtes RTL
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Entrez dans l'Histoire RTL
- C dans l'air France Télévisions
- Laurent Gerra RTL
- L'œil de Philippe Caverivière RTL
- LEGEND Guillaume Pley
- On marche sur la tête Europe1
- Les récits de Stéphane Bern Europe 1
- Hondelatte Raconte - Cote B Europe 1
- Enquêtes criminelles RTL
- L’heure du crime : les archives de Jacques Pradel RTL
- Bercoff dans tous ses états Sud Radio
- La dernière Radio Nova
- Global News Podcast BBC World Service
- TOCSIN PODCAST TOCSIN MÉDIA
- Culture médias - Thomas Isle Europe 1
- Pascal Praud et vous Europe 1
- L'Heure des Pros CNEWS
- C ce soir France Télévisions