Filtra per genere

Wimbi la Siasa

Wimbi la Siasa

RFI Kiswahili

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

160 - Wakaazi wa jimbo la Somaliland wapiga kura kumchagua rais na wabunge
0:00 / 0:00
1x
  • 160 - Wakaazi wa jimbo la Somaliland wapiga kura kumchagua rais na wabunge

    Wakaazi wa jimbo la Somaliland, mojawapo wa êneo lililojitenga na Somalia zaidi ya miaka 30 iliyopita, tangu mwaka 2003 wamekuwa wakishiriki kwenye uchaguzi wa kumchagua rais na wabunge wao.

    Fursa hiyo pia imekuja Novemba tarehe 13 mwaka 2024 ambapo wapiga kura Milioni 1 waliondikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Somaliland wanamchagua rais atakayewatumikia kwa miaka metano.

    Wagombea watatu wanatafuta urais wa jimbo hilo, akiwemo kiongozi wa sasa Muse Bihi Abdi, anayetaka muhula wa pili, lakini mpinzani wake mkuu ni Abdirahman Mohamed Abdullahi, maarufu kwa jina la  "Irro,”.

    Kwenye Makala ya Wimbi la Siasa, tunajadili umuhimu wa uchaguzi wa jimbo la Somaliland na umuhimu wake, kwenye Jumuiya ya Kimataifa, wakati huu, êneo hilo linapotaka kujitawala.

    Wed, 13 Nov 2024
  • 159 - Msumbuji : Upinzani wakataa kutambua ushindi wa Daniel Chapo

    Nchini Musumbuji maandamano yamekuwa yakishuhudiwa baada ya upinzani kukataa kutambua ushindi wa mgombea wa chama tawala Daniel Chapo.

    Aliyekuwa mgombea wa upinzani Venancio Mondlane, amekuwa akisisitiza kwamba alipokonywa ushindi, katika makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Musumbiji.

    Wachambuzi wa siasa za kimataifa Lugete Mussa Lugete na Felix Arego wanafafanua hali nchini Msumbiji.

    Tue, 05 Nov 2024
  • 158 - Kenya : Bunge la Kenya lamuondoa naibu rais afisini

    Nchini Kenya bunge la kitaifa na seneti limeidhinisha kuondolewa afisini kwa naibu rais Rigathi Gachagua, kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kueneza siasa za kikabila.

    Makala haya yaliandaliwa mapema.

    Sat, 26 Oct 2024
  • 157 - Mgogoro kati ya rais na naibu wake nchini Kenya ambao ni mzozo wa kihistoria

    Hatma ya aliyekuwa naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua sasa utaamuliwa na mahakama baada ya mabunge yote mawili kumwondoa madarakani kwa njia ya hoja maalum

    Hatua ya kuondolewa Gachagua ni dhihirisho ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya rais William Ruto na naibu wake Gachagua ,matukio ambayo si mageni nchini Kenya.

    Wed, 23 Oct 2024
  • 156 - Maadhimisho ya mwaka mmoja wa shambulio la Hamas huko Gaza Oktoba 7 2024

    Makala wimbi la siasa inaangazia maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kundi la Hamas, litekeleze shambulio baya zaidi kuwahi kutekelezwa huko Israeli, tukio ambalo lilianzisha vita ambayo imesababisha vifo kwa maelfu ya raia wa Kipalestina na maandamano duniani kote kupinga vita hiyo, wakati huu mzozo huo ukihofiwa kuenea katika mashariki ya kati. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka na waalikwa wake

    Wed, 09 Oct 2024
Mostra altri episodi