Nach Genre filtern

Afrika Ya Mashariki

Afrika Ya Mashariki

RFI Kiswahili

Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.

145 - Uwekezaji katika sekta ya kilimo mkoani Arusha Kaskazini mwa Tanzania
0:00 / 0:00
1x
  • 145 - Uwekezaji katika sekta ya kilimo mkoani Arusha Kaskazini mwa Tanzania

    Sekta ya Kilimo inaongoza kuwa na fursa nyingi za uwekezaji kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kwa mfano uzalishaji wa Ngano, mafuta ya kupikia, matunda na mboga mboga, mbolea, Viatilifu, mbegu bora, vifungashio, kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno na eneo la kilimo cha umwagiliaji.  
     

    Fri, 08 Nov 2024
  • 144 - Tanzania: Kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya majimaji

    Karibu katika Makala ya Afrika mashariki, hii leo tunatuwama nchini Tanzania katika Mkoa Lindi uliopo kusini mwa Tanzania mahali ilipo ibuka vita vya majimaji mara hii ikiwa ni kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya Majimaji.

    Vita vya Majimaji vilipata mizizi yake katika eneo la Nandete Kipatimu, ambapo jamii za Matumbi zilijitokeza kwa ujasiri dhidi ya ukandamizaji wa kikoloni.

    Roho hii ya upinzani ilichochea moto ulioenea hadi katika eneo la Ruvuma, ambapo watu wa huko, wakichochewa na ujasiri wa majirani zao, walianza kuungana katika mapambano yao wenyewe.

    Wao pia waliharibu barabara walizolazimishwa kujenga, wakigeuza mandhari ya ukandamizaji kuwa uwanja wa vita kwa ajili ya uhuru.

    Uasi huu wa pamoja ulionyesha azma inayokua miongoni mwa jamii za kupambana na ukweli mgumu wa utawala wa Kijerumani na kudai heshima yao. 

    Thu, 24 Oct 2024
  • 143 - Wiki ya vijana ilivyoaadhimishwa mjini Mwanza nchini Tanzania

    Tunaangazia jinsi vijana wanavyoweza kutumia fursa za kidijitali katika kukuza na kuimarisha shughuli zao za kiuchumi mjini Mwanza nchini Tanzania. 

    Thu, 17 Oct 2024
  • 142 - Tanzania: Mradi wa Jenga Kesho Bora ulivyoanza kutoa mazao kwa wafugaji wa samaki

    Namna Mradi wa Jenga Kesho Bora (BBT), unaosimamiwa na Wizara ya Kilimo nchini Tanzania ulivyoanza kutoa mazao kwa wafugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ndani ya Ziwa Victoria. 

    Fri, 04 Oct 2024
  • 141 - Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya lugha ya alama

    Jamii imetakiwa kujifunza lugha ya alama ilikuweza kuwasiliana vyema na watu wanaoishi na ulemavu wa kusikia.

    Fri, 27 Sep 2024
Weitere Folgen anzeigen