Filtrar por género
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
- 145 - Uwekezaji katika sekta ya kilimo mkoani Arusha Kaskazini mwa Tanzania
Sekta ya Kilimo inaongoza kuwa na fursa nyingi za uwekezaji kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kwa mfano uzalishaji wa Ngano, mafuta ya kupikia, matunda na mboga mboga, mbolea, Viatilifu, mbegu bora, vifungashio, kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno na eneo la kilimo cha umwagiliaji.
Fri, 08 Nov 2024 - 144 - Tanzania: Kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya majimaji
Karibu katika Makala ya Afrika mashariki, hii leo tunatuwama nchini Tanzania katika Mkoa Lindi uliopo kusini mwa Tanzania mahali ilipo ibuka vita vya majimaji mara hii ikiwa ni kumbukizi ya miaka 119 tangu kuibuka kwa vita vya Majimaji.
Vita vya Majimaji vilipata mizizi yake katika eneo la Nandete Kipatimu, ambapo jamii za Matumbi zilijitokeza kwa ujasiri dhidi ya ukandamizaji wa kikoloni.
Roho hii ya upinzani ilichochea moto ulioenea hadi katika eneo la Ruvuma, ambapo watu wa huko, wakichochewa na ujasiri wa majirani zao, walianza kuungana katika mapambano yao wenyewe.
Wao pia waliharibu barabara walizolazimishwa kujenga, wakigeuza mandhari ya ukandamizaji kuwa uwanja wa vita kwa ajili ya uhuru.
Uasi huu wa pamoja ulionyesha azma inayokua miongoni mwa jamii za kupambana na ukweli mgumu wa utawala wa Kijerumani na kudai heshima yao.
Thu, 24 Oct 2024 - 143 - Wiki ya vijana ilivyoaadhimishwa mjini Mwanza nchini TanzaniaThu, 17 Oct 2024
- 142 - Tanzania: Mradi wa Jenga Kesho Bora ulivyoanza kutoa mazao kwa wafugaji wa samakiFri, 04 Oct 2024
- 141 - Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya lugha ya alamaFri, 27 Sep 2024
- 140 - EAC: Namna mafunzo ya ujasiriamali yanaweza kuwainua vijanaWed, 18 Sep 2024
- 139 - Maonesho ya awamu ya19 ya biashara katika nchi za Afrika MasharikiWed, 11 Sep 2024
- 138 - EAC: Fursa za uchumi wa samawati katika Ziwa VictoriaFri, 06 Sep 2024
- 137 - Maendeleo ya shughuli za uvuvi kwenye maziwa Tanganyika na Victoria
Hivi karibu serikali ya Tanzania iliitaka taasisi ya uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) kuandaa mkakati wa kulifunga ziwa hilo kwa kipindi kirefu. Kauli hiyo inakuja siku chache baada ya kufunguliwa kwa Ziwa Tanganyika lililofungwa kwa miezi mitatu kutoka Mei 15 hadi Agosti 15, 2024 kwa ajili ya kuruhusu samaki kuweza kuzaliana kwa wingi
Wed, 28 Aug 2024 - 136 - Hofu kwa wavuvi wa biashara ya samaki Ziwa Victoria nchini Tanzania
Serikali ya Tanzania imekuwa ikiteleza kanuni za mwaka 2009 juu ya kulifunga ziwa hilo kwa muda wa siku 10 utaratibu huu umekuwa endelevu hadi sasa ambapo kila mwezi wavuvi hawaruhusiwi kujishughulisha na shughuli za uvuvi kwa siku 10, ikiwa na maana kwamba katika kipindi cha mwaka mzima, Ziwa hilo linafungwa kwa siku 120, sawa na Robo mwaka yaani miezi minne
Wed, 28 Aug 2024 - 135 - Shughuli za uvuvi zarejelewa katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma
Shughuli za Uvuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma zilifungwa kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Mei 15 hadi Agosti 15, mwaka huu lengo likiwa ni kupumzisha ziwa hilo, ili kuchagiza ongezeko la Samaki
Kufungwa kwa ziwa hilo ni makubaliano yaliyoazimiwa katika kikao kilichofanyika mwaka 2022 kikihusisha nchi zinazozunguka ziwa hilo ambazo ni Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)
Fri, 23 Aug 2024 - 134 - Namna siku ya vijana ilivyoadhimishwa katika nchi za Afrika Mashariki
Siku ya Vijana Ulimwenguni, ambayo huadhimishwa tarehe 12 Agosti kila mwaka, ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka wa 1999 kupitia maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Lengo kuu la siku hii ni kutambua mchango wa vijana katika jamii, kuhamasisha ushirikiano na kuunga mkono haki za vijana, na kuonyesha jinsi vijana wanavyoweza kuchangia maendeleo endelevu na amani duniani
Wed, 14 Aug 2024 - 133 - Uchaguzi wa urais uliofanyika nchini Rwanda ambapo rais Kagame alitangazwa mshindiSat, 20 Jul 2024
- 132 - Harakati za kuelekea uchaguzi mkuu wa urais nchini Rwanda
Raia wa Rwanda ambao ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki, kwa sasa wapo katika kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu
Uchaguzi utakaofanyika Julai 15, 2024 kumchagua rais wao mpya Pamoja na wabunge
Rais anayemaliza muda wake Paul Kagame anawania kwa muhula wa nne akisaka ridhaa ya Wanyarwamda kusalia katika Ikulu ya Kigali
Taifa la Rwanda linalo kadilikuwa na jumla ya wakazi 14,410,469 kati yao ni Wanyarwanda takribani milioni 9 wameandikishwa katika daftari la mpiga kura kushiriki katika uchaguzi Urais, Jambo lenye sura mpya kwa sasa ni kwa mara ya kwanza uchaguzi huo utafanyika sambamba na ule wa bunge.
Wed, 03 Jul 2024 - 131 - Changamoto za raia wa Afrika Mashariki kupata maji kwa ukaribu
Makala ya Afrika mashariki ikiangazia juu ya namna wakazi wa Jumuiya ya Afrika mashariki wakiwa katika mkwamo wakupata katika huduma ya maji kwa ukaribu licha uwepo wa vyanzo vikumbwa vya maji.
Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Afrika mashariki, Maziwa makubwa yote mawili kwa maana ya ziwa Victoria na Tanganyika, na hatimaye, Mto White Nile hutegemea vyanzo vya maji vya kikanda vinavyojulikana kama Minara ya maji Water Towers ya eneo hilo.
Minara ya Maji ya Afrika mashariki ni mkusanyiko wa mazingira ya milimani na mabonde ya mito yanayohusiana.
Maeneo haya yana ushawishi mkubwa kwa hidrolojia ya kikanda na mizunguko ya hali ya hewa duniani.
Licha ya uwepo wa minara hii bado serikali za wanachama wa jumuiya hii zipo katika mkwamo wakufikisha huduma za maji kwa wananchi walio wengi.
Fri, 28 Jun 2024 - 130 - Tanzania: Kufungwa kwa muda kwa uvuvi ndani ya Ziwa VictoriaSat, 22 Jun 2024
- 129 - Mvutano kati ya Somalia na Ethiopia kuhusiana na suala la SomalilandSat, 08 Jun 2024
- 128 - Kumbukizi ya miaka 28 tangu kuzama kwa meli ya MV BukobaSat, 01 Jun 2024
- 127 - Tanzania: Jinsi raia wanaoishi na ulemavu wanapambana kujikimu kichumiFri, 24 May 2024
- 126 - Mafundisho potofu kutoka kwa baadhi ya viongozi wa dini Afrika MasharikiThu, 16 May 2024
- 125 - Juhudi za kupambana na ulawiti wa watoto katika nchi za Afrika mashariki
Ulawiti ni janga linaloendelea kuwakumba watoto si tu katika mataifa ya ukanda wa Afrika mashariki bali katika mataifa mbalimbali ulimwenguni.
Nchini Tanzania kumekuwa na takwimu za kupanda na kushuka huku baadhi ya wanaharkati wakisema kuwa swala la uzembe limekuwa likichangia kuongezeka kwa ubakaji na ulawiti kwa Watoto
Hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na kuibua wito wa kitaifa kwa wazazi kuongeza ulinzi na ufuatiliaji wa watoto wao.
Thu, 09 May 2024 - 124 - Ujumbe unaoandikwa kwenye vyombo vya usafiri katika mataifa ya AfrikaWed, 01 May 2024
- 123 - Tanzania:Juhudi za wabunifu katika kupunguza hewa ya ukaa kutunza mazingira
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Masuala na Utalii, katika taarifa ya misitu na ufugaji nyuki inabainisha kuwa mkaa ni chanzo kikubwa cha nishati ya kaya katika maeneo ya mijini kwa kupikia na kupasha joto, kwa kuwa inachukuliwa kuwa ya bei nafuu na inapatikanakwaurahisi.
Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya watu wote wa Tanzania kutegemea nishati ya majani. Nishati ya kupikia ndiyo inayoongoza kwa matumizi ya biomasi katika kaya ikilinganishwa na sekta nyingine kama vile ujenzi na kilimo sekta ya msingi.
Thu, 18 Apr 2024 - 122 - Fursa za uchumi wa buluu zilizopo katika Ziwa Victoria
Uchumi wa Buluu ni dhana pana yenye kubeba maana nzima ya kutumia kila rasilimali itokanayo na rasilimali maji kama Bahari, mito na maziwa.
Dhana hii ubeba shuguli mbalimbli ikiwemo utalii, uvuvi, kilimo cha mwani, bandari pamoja na mafuta na gesi zilizomo baharini au katika maziwa.
Kwa wakazi wa Jumuiya ya Afrika mashariki hasa katika mikoa inayo zunguka Ziwa.
Victoria kwa siku za usoni wanachangamkua fursa za uchumi wa buluu uliopo katika maeneo yao.
Dhana hii inatafsiriwa kwa kasi kwa siku za usoni na imekuwa ikitajwa kama ndio mharobaini wakuwanusua wananchi walio wengi kutoa katika mnyonyoro wa umasikini uliotopea.
Sat, 13 Apr 2024
Podcasts similares a Afrika Ya Mashariki
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- Tiempo de Juego COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR
Otros podcasts de Noticias y Politica
- Les Grosses Têtes RTL
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Entrez dans l'Histoire RTL
- C dans l'air France Télévisions
- Laurent Gerra RTL
- L'œil de Philippe Caverivière RTL
- LEGEND Guillaume Pley
- Les récits de Stéphane Bern Europe 1
- On marche sur la tête Europe1
- Hondelatte Raconte - Cote B Europe 1
- L’heure du crime : les archives de Jacques Pradel RTL
- Bercoff dans tous ses états Sud Radio
- Enquêtes criminelles RTL
- La dernière Radio Nova
- Global News Podcast BBC World Service
- TOCSIN PODCAST TOCSIN MÉDIA
- L'Heure des Pros CNEWS
- Culture médias - Thomas Isle Europe 1
- Pascal Praud et vous Europe 1
- C ce soir France Télévisions