Nach Genre filtern
- 12088 - 03 DESEMBA 2024
- Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe mahususi kwa siku hii, ameueleza ulimwengu kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanawakumbusha kwamba ulimwengu unahitaji uongozi wa watu wenye ulemavu zaidi kuliko hapo awali. Guterres ameeleza kuwa Watu wenye ulemavu tayari wanabeba mzigo mkubwa wa majanga yanayoumiza ulimwengu lakini mara nyingi wananyimwa haki yao ya kuchangia katika suluhu za majanga haya.Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Syria hii leo imezitaka pande zinazopigana nchini Syria zifuate kikamilifu sheria za kimataifa na kuwalinda raia. Hii inatokana na ongezeko kubwa la mapigano tangu tarehe 27 mwezi uliopita ambayo yanatishia kuenea katika maeneo mengine ya nchi.Mkutano wa mwaka 2024 wa Taaluma kuhusu Afrika umeanza leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Mada ya mkutano huo wa siku tatu ni "Nguvu, Haki, na Watu: Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria kwa Mabadiliko ya Afrika." Mkutano huo wa kila mwaka unalenga kuongeza uwakilishi wa Waafrika katika ufadhili wa kimaendeleo wa kimataifa, ili kuchagiza mustakabali bora wa Afrika.Na mashinani leo ikiwa ni siku ya watu wenye ulemavu duniani tunakupeleka Timor-Leste, kusini-mashariki mwa Asia kuona jinsi mradi uliofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP umemwezesha Antonio Ornai mwenye ulemavu wa kutoona kushiriki zoezi la kuitikia maonyo ya taarifa za majanga kwenye taifa hilo ambalo hugubikwa na majanga ya asili mara kwa mara kama vimbunga na mafuriko.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Tue, 03 Dec 2024 - 12087 - Kiswahili kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali duniani
Kuendeleza utamaduni wa jamii mbalimbali ni moja ya masuala yanayopigiwa chepuo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa dhamira ya kuhakikisha utambulisho wa jamii unarithishwa kutoka kizazi hadi kizazi. Mkoa wa Tanga uliopo Kaskazini mwa Tanzania umekuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha hilo kupitia vifaa mbalimbali vya kitamaduni ambavyo vimekuwa vikitumika enzi na enzi katika jamii na sio tu kukuza lugha ya Kiswahili bali kuhakikisha inaendelea kwa vizazi na vizazi . Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wanawake wanaohakikisha utamaduni huo haupotei, ungana nao katika makala hii kupata undani.
Mon, 02 Dec 2024 - 12086 - Mashauriano ya mkataba wa kutokomeza plastiki yaahirishwa hadi mwakani, rasimu mpya yawasilishwa
Vuta nikuvute kwenye mashauriano huko Busan, Korea Kusini kuhusu mkataba wenye nguvu za kisheria dhidi ya uchafuzi utokanao na matumizi ya plastiki na kulinda mazingira ya baharini imefikia ukingoni kwa mkutano kuahirishwa na wawakilishi wa nchi zilizokuwa zinashiriki kuridhia rasimu mpya yenye ibara 32 itakayojadiliwa mwakani. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Mon, 02 Dec 2024 - 12085 - 02 DESEMBA 2024
- Vuta nikuvute kwenye mashauriano huko Busan, Korea Kusini kuhusu mkataba wenye nguvu za kisheria dhidi ya uchafuzi utokanao na matumizi ya plastiki na kulinda mazingira ya baharini imefikia ukingoni kwa mkutano kuahirishwa na wawakilishi wa nchi zilizokuwa zinashiriki kuridhia rasimu mpya yenye ibara 32 itakayojadiliwa mwakani.Wakati jana Desemba Mosi Ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya UKIMWI kwa kuhamasisha haki za binadamu ili kufanikisha vita dhidi ya ugonjwa huu hatari, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) inajivunia miaka 25 ya kujiunga na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) katika kushughulikia janga la Virusi Vya UKIMWI (VVU) miongoni mwa watu wanaotumia dawa za kulevya na miaka 20 ya kazi ya kupambana na UKIMWI magerezani.Makala leo inamulika jinsi bidhaa za kitamaduni zinavyotumika kukuza na kuendeleza mila na desturi za Kiswahili mkoani Tanga Kaskazini mwa Tanzania. Je ni bidhaa zipi hizo na zinatumika vipi? Tuungane na Flora Nducha aliyeyabaini hayo hivi karibuni alipokuwa Havana Cuba kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili.Na mashinani tunasikiliza manufaa ya ufadhili wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD kwa wakulima kutoka kwake Sharon Kirui kutoka Kaunti ya Nakuru nchini Kenya ambaye ni mnufaika wa vocha za kielektroniki za ununuzi kutoka kwa IFAD na ameweza kupanua biashara yake ya kilimo.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mon, 02 Dec 2024 - 12084 - UNODC yajivunia miaka 20 ya kupambana na UKIMWI magerezani
Wakati jana Desemba Mosi Ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya UKIMWI kwa kuhamasisha haki za binadamu ili kufanikisha vita dhidi ya ugonjwa huu hatari, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) inajivunia miaka 25 ya kujiunga na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) katika kushughulikia janga la Virusi Vya UKIMWI (VVU) miongoni mwa watu wanaotumia dawa za kulevya na miaka 20 ya kazi ya kupambana na UKIMWI magerezani. Anold Kayana na taarifa zaidi.
Mon, 02 Dec 2024 - 12083 - Mradi wa IFAD wasaidia vijana Senegal kusalia nchini mwao, kulikoni?
Mradi wa uitwao Agri-Jeunes uliozinduliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD ili kusaidia raia wa Senegal kuondokana na umaskini, na janga la njaa, umewapatia vijana wa kiume na wa kike matumaini ya kusalia nchini mwao badala ya kuhamia ughaibuni. Mradi huu umewasaidia vijana hao kwa mafunzo ya kilimo, ufugaji kuku, uvuvi na stadi za kuendesha biashara ndogondogo.
Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2024, makumi ya maelfu ya watu waligeukia wasafirishaji haramu wa binadamu kwa njia ya bahari ya Atlantiki kuelekea visiwa vya Kanari, lakini zaidi ya watu 5000 wamekufa wakijaribu kufika huko. Haya yote yakisababishwa na ukosefu wa ajira na kipato duni. Kupitia video iliyoandaliwa na IFAD, Bosco Cosmas amefuatilia Maisha ya vijana hao, na kutuandalia makala hii
Fri, 29 Nov 2024 - 12082 - Fahamu mbinu itumiwayo Afrika Kusini kukabili Virusi Vya Ukimwi
Kuelekea ya Siku ya Kimataifa ya UKIMWI itakayoadhimishwa Jumapili hii, ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) iliyotolewa juzi Jumatano imeeleza kuwa dunia inaweza kufikia lengo lililokubaliwa la kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030 lakini kwa sharti kwamba viongozi ni lazima walinde haki za binadamu za kila mtu anayeishi na Virusi Vya UKIMWI, VVU au aliyeko hatarini kuambukizwa. Anold Kayanda ameangazia mfano mzuri wa Afrika Kusini unaofahamika kama “Takuwani Riime”.
Fri, 29 Nov 2024 - 12081 - Gaza yanafanishwa na 'jehanamu'
Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ofisi ya eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, Ajith Sungay amesema miezi 13 ya vita imeufanya Ukanda wa Gaza kuwa kama jehanamu, kwani kuna uharibifu usio na kifani, njaa isiyoelezeka magonjwa na kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu yanayotawanya raia kila uchao. Flora Nducha na taarifa zaidi.
Fri, 29 Nov 2024 - 12080 - 29 NOVEMBA 2024
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika adha zinazokumba raia kwenye eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli; hakari za kukabili UKIMWI Afrika Kusini; IFAD ilivyonusuru vijana na safari za kwenda Ulaya zinazohatarisha maisha yao; Mkimbizi wa ndani Gaza anayezungumzia harakati za kusaka mkate ili kulisha familia yake.
- Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ofisi ya eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, Ajith Sungay amesema miezi 13 ya vita imeufanya Ukanda wa Gaza kuwa kama jehanamu, kwani kuna uharibifu usio na kifani, njaa isiyoelezeka magonjwa na kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu yanayotawanya raia kila uchao. Flora Nducha na taarifa zaidi.Kuelekea ya Siku ya Kimataifa ya UKIMWI itakayoadhimishwa Jumapili hii, ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) iliyotolewa juzi Jumatano imeeleza kuwa dunia inaweza kufikia lengo lililokubaliwa la kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030 lakini kwa sharti kwamba viongozi ni lazima walinde haki za binadamu za kila mtu anayeishi na Virusi Vya UKIMWI, VVU au aliyeko hatarini kuambukizwa. Anold Kayanda ameangazia mfano mzuri wa Afrika Kusini unaofahamika kama “Takuwani Riime”.Mkala inayokupeleka nchini Senegal kusikia jinsi mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo IFAD umewezesha vijana kuondokana na mawazo ya kuweka rehani maisha yao wakisaka maisha bora Ulaya. Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas.Mashinani fursa ni yake nampisha Abu Muhammad, mkimbizi wa ndani huko Deir Al Balah, Ukanda wa Gaza akielezea umuhimu wa mgao wa mikate kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula, WFP, kwa wakimbizi hao wakati huu ambapo vita inaendelea eneo hilo.
Fri, 29 Nov 2024 - 12079 - Jukwaa la UN la Muungano wa Ustaarabu limetufungua macho - Dativa Mahanyu na Mariam Mintanga
Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Ustaarabu limekunja jamvi leo huko Cascais, Ureno ambako sambamba na jukwaa hilo, pia vijana kutoka makundi 150 duniani walikusanyika katika Jukwaa lao. Katika vijana hao walikuwemo watengeneza filamu chipukizi ambao kupitia filamu wanaeleza mambo kadha ya ulimwengu kama uhamiaji, ujumuishaji, kupambana na ubaguzi na mengine mengi. Miongoni mwa vijana hao waliohudhuria ni Dativa Mahanyu na Mariam Mintanga kutoka Tanzania. Kwanza tumsikilize Mariam Mintanga akieleza alivyojisikia kuhudhuria mkutano huu kisha tutamsikia Dativa Mahanyu akieleza kuhusu filamu ya Fid ya ambayo kupitia taasisi ya Tai Tanzania imepata tuzo ya PLURAL+
Wed, 27 Nov 2024 - 12078 - Dkt. Tedros: Kifo cha ghafla cha Dkt. Faustine Ndungulile kimenishtua na kunisikitishaWed, 27 Nov 2024
- 12077 - 27 NOVEMBA 2024
- Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO, amesema amestushwa na kusikitishwa na kifo cha aliyetarajiwa kushika wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Engelbert Ndungulile kutoka nchini Tanzania.Awamu ya pili ya mradi wa kuboresha lishe, SUN II nchini Zambia umewezesha wakulima kupanda mazao yanayohimili ukame na vile vile kukabiliana na viwavi jeshi kwa kutumia mbinu za asili, mradi uliotekelezwa na shirika la Umoja la kuhudumia watoto, UNICEF ili wakulima wasikumbwe na njaa wakati huu ambapo ukame umetikisa nchi za kusini mwa Afrika.Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Ustaarabu limekunja jamvi leo huko Cascais, Ureno ambako sambamba na jukwaa hilo, pia vijana kutoka makundi 150 duniani walikusanyika katika jukwaa lao wakiwemo watengeneza filamu chipukizi ambao kupitia filamu wanaeleza mambo kadha ya ulimwengu kama uhamiaji, ujumuishaji, kupambana na ubaguzi na mengine mengi. Miongoni mwa vijana hao ni Dativa Mahanyu na Mariam Mintanga kutoka Tanzania. Kwanza tumsikilize Mariam Mintanga akieleza alivyojisikia kuhudhuria mkutano huu kisha tutamsikia Dativa Mahanyu akieleza kuhusu filamu ya Fid ya ambayo kupitia taasisi ya Tai Tanzania imepata tuzo ya PLURAL+.Na mashinani fursa ni yake Shaza Ahmed, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la wanawake Nada El Azha linalotoa msaada kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia nchini Sudana akitoa wito kwa viongozi wa kimataifa wa kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Wed, 27 Nov 2024 - 12076 - UNICEF yawapatia wakulima nchini Zambia tumaini la kupata chakula
Awamu ya pili ya mradi wa kuboresha lishe, SUN II nchini Zambia umewezesha wakulima kupanda mazao yanayohimili ukame na vile vile kukabiliana na viwavi jeshi kwa kutumia mbinu za asili, mradi uliotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, ili wakulima wasikumbwe na njaa wakati huu ambapo ukame umetikisa nchi za kusini mwa Afrika. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Wed, 27 Nov 2024 - 12075 - Namayombo Mgonela: Utamaduni wa Kiswahili umeniinua kiuchumi
Lengo namba 5 la Maendeleo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, ya Umoja wa Mataifa ni usawa wa kijinsia ambao ni pamoja na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa. Akiwa Havana Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la kimataifa la Kiswahili Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili, alikutana na kuzungumza na Namayombo Nyanzala Mgonela, mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vilivyoko Karibea St. Kitts na Nevis ambaye anatumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe katika jitihada za kutimiza lengo hilo. Kwa kina zaidi tuungane na Flora Nducha.
Tue, 26 Nov 2024 - 12074 - 26 NOVEMBA 2024Tue, 26 Nov 2024
- 12073 - Tanzania: FAO yawezesha ufugaji kuku bila kutumia dawa ili kuepusha UVIDA
Nchini Tanzania wanufaika wa mradi wa kudhibiti usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, (AMR) au kwa lugha ya Kiswahili, (UVIDA) unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamezungumzia manufaa ya ufugaji wa kuku bila kutumia dawa. Unaweza kujiuliza wanafuga vipi kuku bila kutumia dawa. Na je ni kwa nini wanafanya hivi. Je hawatumii dawa kabisa au wanafanya nini?
Katika makala hii, mwandishi wa habari wa Redio washirika wetu Tanzania Kids Time ya mkoani Morogoro,mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, Hamad Rashid, amezungumza na wanufaika hao ambao pia walipata nafasi ya kuonesha shamba darasa la ufugaji kuku bila ya kutumia dawa kupitia hafla iliyoratibiwa na FAO katika shule ya sekondari Kihonda, Manispaa ya Morogoro, ikienda sambamba na Wiki ya utoaji elimu kuhusu UVIDA ambayo hufanyika duniani kote kila ifikapo tarehe 18 hadi 24 mwezi Novemba. Kwako Hamad.
Mon, 25 Nov 2024 - 12072 - MONUSCO yaitikia ombi la Meya wa Beni, Kivu Kaskazini DRC
Kiu cha Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, cha kuona daraja linalounganisha barabara muhimu linakarabatiwa kilipata jawabu baada ya ombi lake kwa Ujumbe wa Umoja wa MAtaifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kuchukua hatua ambayo pia inawezesha doria za ulinzi wa raia mjini humo. Maelezo kamili anayo George Musubao kutoka Beni, katika taarifa hii tuliyoitoa kwenye ukurasa wa Xwa MONUSCO.
Mon, 25 Nov 2024 - 12071 - 25 NOVEMBA 2024
- Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, Je wajua kwamba wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa wapenzi wao au ndugu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja anauawa katika kila dakika 10. Na zaidi ya yote bara la Afrika linaongoza?Kiu cha Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, cha kuona daraja linalounganisha barabara muhimu linakarabatiwa kilipata jawabu baada ya ombi lake kwa Ujumbe wa Umoja wa MAtaifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kuchukua hatua ambayo pia inawezesha doria za ulinzi wa raia mjini humo.Makala inatupeleka Tanzania kwake Hamad Rashid wa redio washirika Kidstime FM ya mkoani Morogoro, mashariki mwa taifa hilo akizungumza na wanufaia wa mafunzo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO la ufugaji kuku bila kutumia dawa.Na mashinani tunakwenda Kenya kusikia harakati za viongozi wa dini ya kiislamu kukabiliana na ukatili wa kijinsia.
Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Mon, 25 Nov 2024 - 12070 - UN: Mwanamke au msichana mmoja aliuawa kila baada ya dakika 10 na mwenzi au ndugu 2023
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, Je wajua kwamba wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa wapenzi wao au ndugu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja anauawa katika kila dakika 10. Na zaidi ya yote bara la Afrika linaongoza?
Maudhui ya siku hii yanasema “Hakuna kisingizio” cha ukatili dhidi ya wanawake lama alioushuhudia Ester manusura kutoka Uganda, ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifanyiwa ukatili na mpenzi wake anaema “Nilikuwa na umri wa miaka 15 aliponioa naye alikuwa na miaka 28wakati mwingine alikuwa akinivua nguo zote na kunilazimisha kukaa kwenye varandana nilikuwa nikichelewa kurudi ananitandika nje nyumba kila mtu kushuhudia Nilikuwa katika hali mbaya ya uchungu Mkubwa na kuvuja damu.”
maadhimisho ya mwaka huu yanaambatana na ripoti iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la masuala ya wanawake, UN Women na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kudhibiti Dawa za kulevya na Uhalifu, (UNODC), inaangazia mwanga wa janga la mauaji ya wanawake na kutoa wito kwa hatua za dharura ili kukabili janga hilo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ujumbe wake wa siku hii inayoadhimishwa tarehe 25 mwezi Novemba kila mwaka, ikiashiria pia kuanza kwa siku 16 za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, zikiwa na kilele chake tarehe 10 mwezi Desemba, siku ya Haki za Binadamu duniani amesema “Janga la ukatili dhidi ya wanawake na wasichana linaaibisha ubindamu, dunia lazima iitikie wito huu. Tunahitaji hatua za dharura kwa ajili ya haki na uwajibikaji, na kusaidia uchechemuzi.”
Mkurugenzi mtendaji wa UN Women Sima Bahous amesisitiza kuwa “Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana si kwamba hauepukiki, unaweza kuzuilika. Tunahitaji sheria thabiti, ukusanyaji bora wa takwimu, uwajibikaji zaidi wa serikali, utamaduni wa kutovumilia, na kuongezeka kwa ufadhili kwa mashirika ya kupigania haki za wanawake na taasisi. Tunapokaribia kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji mwaka 2025, ni wakati wa viongozi wa dunia kuungana na kuchukua hatua kwa haraka, kujitolea na kuelekeza rasilimali zinazohitajika kumaliza mgogoro huu mara moja na kwa wote”
Mauaji ya wanawake yanavuka mipaka, hali ya kiuchumi na kijamii, utamaduni. Hata hivyo kiwango au ukubwa wake unatofautiana.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, bara la Afrika lilivunja rekodi ya kuwa na viwango vya juu vya wanawake kuuawa na wapenzi wao au mwanafamilia. Wanawake 21,700 waliuawa Afrika mwaka huo wa 2023, ikifuatiwa na bara la Amerika na kisha Oshenia.
Mashirika ya UN Women na…
Mon, 25 Nov 2024 - 12069 - Vijana wajumuishwe kwenye majadiliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi - Nasra
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania umewajumuisha watoto kwenye harakati za kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Huko Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 tunamsikia Nasra Abdallah, mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania akizungumzia kilichompeleka, anachoondoka nacho na ujumbe wake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Fri, 22 Nov 2024 - 12068 - Kuna mkwamo kwenye mkutano wa COP29 huku mapendekezo mapya yakitaka nchi tajiri kuzilipa masikini dola bilioni 250 kwa mwaka
Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea.
Hakika vuta nikuvute bado inaendelea hata sasa washiriki wako mezani kwakikuna vichwa na kujadili mapendekezo mapya. Mkwamo huo umetokana na kushindwa kuafikiana katika masuala kadhaa kubwa likiwa ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi na hususasn kuhusu ni kiasi gani cha fedha nchi zinazoendelea zinapaswa kupokea kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 na wapi fedha hizo za ufadhili zitatoka.
Nchi zinazoendelea zinataka kulipwa dola trilioni 1.3 kwa mwaka lakini hilo halijaafikiwa na mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na raia wa mkataba huo wa UNFCCC yanaonyesha tofauti kubwa na safari ndefu ya kufikia muafaka.
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya yaliyowasilishwa leo mezani na Rais wa COP29 Mukhtar Babayev yanataka nchi zinazoendelea kupokea dola bilioni 250 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2035 kwa ajili ya kuchukua hatua didi ya mabadiliko ya tabianchi.
Na maesema “Fedha hizi zitatoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo sekta za umma na za binafsi, na kitaifa na kimataiifa ikiwemo vyanzo mbadala”.
Wakati pia COP29 ikitoa wito wa kufikia lengo la ufadhili wa dola trilioni 1.3 ifikapo mwaka 2035 pia imezikaribisha nchi zinazoendelea kutoa michango ya ziada.
Kiwango kilichopendekezwa cha ufadhili kinatarajiwa kuzusha vuta ni kuvute katika majadiliano hayo kwa siku nzima ya leo huenda hadi kesho ingawa mkutano huo unahisi ahuweni kwamba kuna kiwango kilichowasilishwa na unataka hitimisho la mkutano haraka iwezekanavyo. Je nchi zinazoendelea zitapokea vipi pendekezo hili jawabu bado halijulikani. Wapenzi wa UN News Kiswahili endeleeni kufuatilia kwenye kurasa zetu kufahamu hatma ya mkutano huo.
Fri, 22 Nov 2024 - 12067 - 22 NOVEMBA 2024
- Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea.Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto.Makala inakupeleka Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 kumsikia kijana kutoka Tanzania akizungumzia kilichompeleka, anachoondoka nacho na ujumbe wake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.Na katika mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, tunasikia kauli ya Willem Westhuizen, mkulima kutoka Namibia, akielezea changamoto zinazotokana na ukame unaoathiri maisha yao kila siku”.
Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Fri, 22 Nov 2024 - 12066 - Mafunzo ya walinda amani kutoka Tanzania huko Beni yajengea uwezo walimu kusaidiana na watoto
Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto.
Video ya MONUSCO ikianza na walinda amani wakijongea kwa jamii, Kapteni Noella Nyaisanga kiongozi wa kikundi hicho cha wanawake cha kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania kwenye MONUSCO, TANZBATT-11 anaeleza jinsi kikundi chao kinavyosogea kwa jamii na hasa watoto ili kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi kwenye eneo hili la Beni, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. Anafafanua zaidi lengo lao.
Lengo ni kujenga uaminifu kwa raia ambao tunawalinda. Kwa hiyo tukaamua kuandaa masomo shuleni, ambayo yataweza kuwaimarisha wao, kuwasaidia tatizo la kuwa wameathirika kisaikolojia.
Zavadi Mbambu ni miongoni mwa walimu waliopatiwa mafunzo ya kusaidia watoto walioathiriwa na changamoto lukuki ikiwemo mapigano. Akisema stress, anamaanisha msongo.
“Unakuwa na wanafunzi wanaokuwa na msongo wa mawazo kutokana na jambo ambalo wanaishi, na hata mauaji. Kuna wale ambao hata wameua wazazi wao , hata familia yao yote. Na kwa hao wanafunzi wanapoingia shuleni , wanakuwa kama hawako ndani, fikra zao zinakuwa mbali . Lakini kupitia mafunzo nimewaelewa , na tumejua namna gani ya kuishi nao. Na tayari mabadiliko yameanza kuonekana.”
Pacifique Kyakimwa, mmoja wa wanafunzi anasimulia mkasa mmoja.
“Kuna mwenzetu aliyekuwa na tatizo, yaani tukiwa ndani ya shule, alikuwa anacheka, yaani anatusumbua hadi hatumwelewi mwalimu. Lakini tangu wameanza kufundisha hili somo, wameanza kuelewa . Ameanza kuwa na akili inayotumika vizuri. Mafunzo haya yamefika wakati tunahitaji , na imetusaidia sana.”
Fri, 22 Nov 2024 - 12065 - Jinsi usawa wa kijinsia na rika katika umiliki wa ardhi unavyochochea ukulima na uhakika wa chakula Kenya
Mpango wa Usimamizi wa Ardhi uliopatiwa jina "Kusaidia kufikia Ajenda 2030 kupitia mageuzi chanya ya ugatuzi wa ardhi katika maeneo ya ardhi za jamii nchini Kenya" umeboresha uhakika wa kupatikana kwa chakula na lishe kupitia upatikanaji wa ardhi kwa wote nchini Kenya. Programu hii imezinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya (EU) katika kaunti 9 ikilenga kuimarisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi. Kupitia video iliyoandaliwa na FAO, Cecily Kariuki anaeleza matokeo yake.
Thu, 21 Nov 2024 - 12064 - 21 NOVEMBA 2024
- Hague kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ICC ambayo leo imetoa kibali cha kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wa zamani wa ulinzi Yoav Galant na kiongozi wa kundi la kipalestina la Hamas Mohamed Diab Ibrahim al-Masri alimaarufu kama kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhaifu wa vita ulitendeka wakati wa vita inayoendelea baina ya Israel na Hamas.Mjini Baku nchini Azerbaijan mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachanama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabainchi COP29 unaelekea ukingoni na leo ukijikita na masuala ya kijinsia na mabadiliko ya tabianchi. Miongoni mwa waliozungumzia changamoto ya tabianchi kwa wanawake ni Jemimah Njuki, mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wa kiuchumi katika shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women.“Raia wanaoshtakiwa katika mahakama za kijeshi nchini Uganda hukosa dhamana sawa ya mchakato wa kisheria kama wale wanaoshtakiwa katika mahakama za kiraia,” amesema Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu hii leo kufuatia tukio la kutekwa kwa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kiiza Besigye akiwa nchini Kenya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno MHARABU”.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Thu, 21 Nov 2024 - 12063 - COP29 Georgina Magesa: Watoto wana haki ya kuishi katika mazingira salama
Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 unaoendelea huko Baku Azerbaijan umeleta pia watoto na vijana wanaharakati wa mazingiria kutoka kote ulimwenguni na kuwapatia fursa kuketi katika meza moja na viongozi ili kuhakikisha mustakabali wao umewekwa katika ajenda ya mkataba huo.
Jukumu lao kama wachechemuzi wa mabadiliko chanya na hitaji la mazungumzo na ushirikiano kati ya vizazi lilitambuliwa rasmi katika matokeo ya Mkutano wa Zama Zijazo, SOTF mnamo Septemba 2024.
Georgina Magesa, msichana mwenye umri wa miaka tisa na mwanaharakati wa mazingira, ambaye amewakilisha watoto wenzake kutoka Tanzania katika Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan. Anatoa ujumbe mahsusi akianza kwa kusistiza kuwa watoto pia wana mchango katika kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
“Watoto wenzangu duniani kote, nyie pia mnaweza kuleta mabadiliko chanya. Anza na hatua ndogo pia muwe na ndoto kubwa. Panda miti. Hifadhi maji. Jifunze kuhusu mazingira yetu. Kwa Pamoja vitendo vyetu vidogo vitageuka mabadiliko makubwa”
Katika mwaka huu wa 2024 ambao viwango vya joto duniani vimevunja rekodi duniani, watoto na vijana wanaendelea kupaza sauti zao wakihimiza viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka zinazohitajika ili kushughulikia janga la mabadiliko ya tabianchi. Georgina anasema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF liko mstari wa mbele, lakini sasa ni wakati wa mshikamano kwa ajili ya mazingira bora kwa watoto wa leo, na wa zama zijazo..
“Kwa viongozi wa dunia walioko hapa leo, hii si kazi ya UNICEF pekee. UNICEF inafanya kazi nzuri na sisi watoto, lakini tunahitaji msaada wako ili kujenga ulimwengu wa kesho ambapo hakuna mtoto anayepaswa kuchagua kati ya afya na elimu yake; ambapo hakuna mtoto anayekunywa maji yasiyo salama; hakuna mtoto anayekosa shule kwa sababu ya masuala yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi; na ambapo kila mtoto ana nafasi ya kuwa na afya bora na elimu bora.”
Georgina anatamatisha kwa kusisitiza kuwa janga la mabadiliko ya tabianchi limenyima watoto haki zao hivyo kwa kila mtu...
“Kumbuka unapolinda mazingira unalinda afya, elimu na ndoto za watoto. Mtoto mwenye afya bora na elimu bora anaweza kubadilisha ulimwengu.”
Ama kweli watoto wana haki ya kuishi katika mazingira salama!
Wed, 20 Nov 2024 - 12062 - 20 NOVEMBA 2024
- Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao.Kama ulivyosikia katika taarifa yetu ya kwanza leo ni siku ya watoto duniani ikirejelea tarehe 20 Novemba mwaka 1954 kwa mara ya kwanza kabisa ilipoanzishwa na Umoja wa Mataifa kusongesha umoja na kujitambua miongoni mwa watoto duniani..Makala ikiwa leo ni siku ya watoto duniani, tunakupeleka Baku Azerbaijan katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29, ambako Selina Jerobon amefuatilia mkutano wa watoto na vijana inayomulika mchango wao katika kuhakikisha mazingira bora.Mashinani katika kuadhimisha siku ya watoto duniani tunabisha hodi msitu wa Amazoni nchini Peru kwa mtoto Susan akitoa wito kwa dunia kuchukua hatua dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kulinda msitu huo kunusuru kizazi cha watoto wa sasa na wa vizazi vijavyo katika taifa hilo.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Wed, 20 Nov 2024 - 12061 - UNICEF - Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mtoto duniani yafanyika Denmark
Leo ikiwa ni siku ya watoto duniani ikirejelea tarehe 20 Novemba mwaka 1954 kwa mara ya kwanza kabisa ilipoanzishwa na Umoja wa Mataifa ili kusongesha umoja na kujitambua miongoni mwa watoto duniani. Kisha siku hii ikaongezwa nguvu na Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto duniani mwaka 1959 na hatimaye mwaka 1989 Baraza hilo lililopitisha Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto, CRC. Mkataba unatambua haki kuu nne za msingi za mtoto: Kuishi, Kuendelezwa, Kulindwa na Kushirikishwa. Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limefanya maadhimisho ya kimataifa huko Copenhagen Denmark, na Madina Jubilate, Mchechemu wa UNICEF Tanzania kwa Tabianchi anaelezea alivyoshiriki.
Wed, 20 Nov 2024 - 12060 - Waraka kutoka kwa watoto: Kwenu watu wazima, kwa nini mnauruhusu mustakbali wetu kuwekwa rehani?
Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao.
Hao ni baadhi tu ya makumi ya watoto walioandika barua , hawa ni kutoka Gaza, Tanzania na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC ambao walishika kalamu na karatasi kufikisha ujumbe wao kwa watu wazima wa dunia ya sasa iliyoghubikwa na changamoto lukuki zinazoweka rehani mustakbali wao.
Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNICEF ya “Hali ya watoto duniani mwaka 2024: Mustakabali wa Utoto katika Ulimwengu Unaobadilika,” iliyotolewa leo sanjari na maadhimisho ya siku hii kuna masuala matatu makubwa ya kimataifa yatakatoathiri maisha ya watoto ifikapo 2050 na kuendelea. Mosi ni mabadiliko katika idadi ya watu, pili janga la mabadiliko ya tabianchi na migogoro na tatu teknolojia
UNICEF inasema yote haya ni changamoto na fursa ambazo watoto wanaweza kukabiliana nazo katika zama zijazo.
Rafif mtoto mkimbizi wa ndani ameandika barua kutoka Palestina ambako vita imetamalaki, anasema
“Ninatoka mjini Gaza na sasa nimefurushwa hadi Kusini mwa Gaza. kama watoto Ni haki yetu kuishi kwa usalama na kujenga mustakbali bora”
Kutoka mashariki ya Kati hadi Afrika Mashariki kwa Steven akimulika afya
“Na nianaandika kwenu kutoka Tanzania. Kwenye jamii yangu watoto wanaugua kila wakati , kwa nini? Huu ndio mustakbali wangu je unasikiliza?”
Nako Congo DRC mitihani ni mingi, Andrea anasema
“Nataka kushuhudia dunia ambayo kila mtoto anapendwa, dunia ambayo amani inashamiri ni raha na faraja. Napenda kuona hasira zinageuka na kuwa mazungumzo”
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiunga mkono suti hizo za watoto katika ujumbe wake amesema Katika Siku ya Watoto Duniani tunasherehekea washiriki wachanga zaidi wa familia yetu ya kibinadamu. Lakini leo pia ni wakati wa kutambua changamoto kubwa zinazowakabili watoto katika ulimwengu wetu uliogawanyika sana, wenye misukosuko na mara nyingi ulioshamiri ukatili.”
Ripoti ya UNICEF imetoa wito wa kuwekeza katika elimu, miji endelevu na yenye mnepo kwa watoto, miundombinu inayohimili mabadiliko ya tabianchi, teknolojia, huduma muhimu na mifumo ya msaada wa kijamii na pia teknolojia iliyo salama kwa watoto ili kupambana na mzigo wa changamoto zinazowakabili.
Wed, 20 Nov 2024 - 12059 - 19 NOVEMBA 2024
- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewasihi viongozi wa kundi la nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, G20 wanaokutana huko Rio De Janeiro, Brazil kuwaagiza mawaziri na washawishi wao huko COP29 wahakikishe wanakubaliana juu ya lengo jipya na kubwa la mwaka huu la ufadhili kwa tabianchi nchi. Guterres amesema sambamba na hilo ni vema kukabiliana na taarifa potofu kuhusu tabianchi.Huko Kusini mwa Lebanon, walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha Mpito nchini humo, UNIFIL, wameshuhudia uharibifu mkubwa wa kutisha kwenye vijiji vilivyoko sambamba na eneo la kati ya Israeli na Lebanon lisilopaswa kuwa na mapigano, huku hali ya watoto nchini humo ikizidi kuwa mbaya.Hii leo ni siku ya choo duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema licha ya choo kuwa ni msingi wa kusongesha afya ya binadamu na kusaidia watoto wa kike na wanawake kuishi maisha ya utu, bado wakazi wengi wa dunia hususan kwenye mizozo na majanga wanaishi bila huduma hiyo ya msingi.Mashinani tunasalia huko huko Baku, kwenye COP29 ambapo nampisha msichana mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania, akieleza ni nini anafanya na nini atakachoondoka nacho kwenye mkutano huo.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Tue, 19 Nov 2024 - 12058 - Uganda inaendelea na mapambano ya kutunza wakimbizi licha ya changamoto za kifedha
Kwa miongo kadhaa sasa mfumo wa Uganda wa kuwaweka wakimbizi kwenye makazi badala ya kambi, umesaidia kujengea mnepo wakimbizi na hivyo wanaweza kujitegemea. Wakimbizi wanapata huduma za msingi kama vile hata ardhi ya kulima na kufugia mifugo ili kujipatia kipato. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Selina Jerobon amefuatilia hadithi ya mama mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye baada ya kupitia machungu na kukimbilia nchini Uganda sasa ameanza kuwa na matumaini ingawa ukata unatishia huduma kama alivyojionea mwenyewe Fillipo Grandi, Kamishna Mkuu wa shirika hilo.
Mon, 18 Nov 2024 - 12057 - Vijana wafurahia stadi za kuondokana na umaskini Sudan Kusini
Vijana katika mji wa Tambura ulioko jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanageuza mafunzo ya ufundi stadi kuwa nguvu ya amani na ustawi, mafunzo ambayo yalifanikishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.
Shamrashamra zilitawala wakati vijana 61, wakiwemo wasichana 41 na wavulana 20 walipohitimu mafunzo ya ufundi stadi yenye lengo la kuwaondoa katika umaskini na pia kuwaepusha kutumikishwa katika mzozo unaoendelea nchini humo tangu Desemba 2013.
Walifundishwa urembo wa nywele, kutengeneza sabuni, halikadhalika ushoni, mafunzo yaliyofadhiliwa na UNMISS na kutolewa na shirika la kiraia Star Trust Organization, linalohusika na kupunguza ghasia kwenye jamii kwa kuwajegena vijana uwezo.
Miongoni mwao ni Suzan James, mama wa watoto wawili aliyejifunza urembo wa nywele na akiwa anamhudumia mteja wakati wa mafunzo anasema.
“Ninashukuru mno, kwa sababu nimejifunza mambo mengi ambayo awali sikuyafahamu, lakini sasa ninaweza kufanya. Inanisaidia sana, na ninajivunia na nina furaha. Baada ya hili, nitaenda kufungua sehemu yangu mwenyewe ya urembo wa nywele ili kusaidia jamii.”
Huyu ni Justin Alex yeye amejifunza ushoni na akiwa kwenye chereheni yake anasema.. “iwapo nitapekela hii cherehani nyumbani, nitaweza kufanya kazi na kusaidia familia yangu. Kama kijana tusikae nyumbani au tusifanye uhalifu mjini na kusababisha vifo kwa jamii zetu kwa sababu si jambo zuri. Kuanzia sasa tunahitajika kushiriki kwenye shughuli za kusaidia jamii, kama kupeleka hii cherehani nyumbani ili nisaidie jamii yangu.”
Wahitimu wamepatiwa vifaa vya kuanzia kufanyie kile walichojifunza. Katika hafla ya utoaji wa vyeti UNMISS iliwakilishwa na afisa wake wa masuala ya ulinzi na ujumuishaji kwenye jamii Ibrahim Tahiru ambaye amesema..
“Mradi huu unaweza kuleta amani, lakini pia mradi huu huu unahitaji amani ili uweze kuendelea. Bila amani hivi vitu vitakuwa bure. Kwa sababu wahitimu wanahitaji mazingira yenye amani ili waweze kutumia stadi zao kwa ajili ya kuboresha maisha yao na ya jamii zao. Mradi huu ni ishara ya nia yetu ya kuendelea kushirikiana na Sudan Kusini na kusaidia kufikia amani ya kudumu na kuondokana na umaskini.”
Mamlaka za Tambura zina Imani kubwa na mradi huu kama asemavyo Kaimu Kamishna wa Tambura Moses Masisere.
“Hakika, Tambura tumekuwa tukililia amani. Kwa hiyo kwa msaada huu tunaamini kuwa mafunzo kwa vijana zaidi kutawasaidia washiriki kwenye harakati za kiuchumi na kupunguza mauaji na uhalifu mwingine Tambura.”
Mon, 18 Nov 2024 - 12056 - 18 NOVEMBA 2024
- Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.Vijana katika mji wa Tambura ulioko jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanageuza mafunzo ya ufundi stadi kuwa nguvu ya amani na ustawi, mafunzo ambayo yalifanikishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.Katika makala Selina Jerobon kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi anakupeleka Uganda kuona harakati za wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kujikwamua kiuchumi baada ya machungu waliyopitia nyumbani kwao.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani jamii katika maeneo kame wanakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mwenyeji wako ni Bosco Cosma, karibu!
Mon, 18 Nov 2024 - 12055 - IOM: Zaidi ya watu 20,000 wamefuriushwa ndani ya siku 4 Haiti kutokana na machafuko ya magenge ya uhalifu
Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince (POTOPRINSI) limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo na IOM nmini Port-au-Prince asilimia kubwa ya watu hawa waliofurushwa makwao wametawanywa zaidi ya mara moja wakilazimika kukimbia na kuacha kila kitu walichokuwa nacho na shirikika hilo linasema kiwango hiki cha watu kutawanywa hakijashuhudiwa Haiti tangu Agost 2023.
Shirika hilo linasema kufungwa kwa usafiri wa anga kufuatia shambulizi lililolenga ndege tatu za kibiashara mjini Port-au-Prince, kuzuia ufikiaji wa bandari kuu ya nchi hiyo, na barabara zisizo salama zinazodhibitiwa na makundi yenye silaha kumeliacha eneo la Katikati ya mji mkuu taabani na kutengwa bila msaada na hivyo kuzidisha mateso kwa watu ambao tayari wako hatarini.
Mkuu wa IOM nchini Haiti Grégoire Goodstein ameonya kwamba "Kutengwa kwa Port-au-Prince kunaongeza janga la ibinadamu. Uwezo wetu wa kutoa misaada umewekwa njiapanda na bila msaada wa haraka wa kimataifa, mateso yataongezeka sana kwa raia wa Haiti huku kukiwa na asilimia 20 pekee ya mji wa Port-au-Prince inayofikika, wakati wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kufikia watu walioathirika.”
Kulingana na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, vikundi vya uhalifu katika mji mkuu wa Hati vinaendelea kupanuka wigo vikichukua udhibiti wa vitongoji vya ziada na kutenganisha zaidi jamii.
Hadi sasa ofisi hiyo inasema ghasia zinazohusiana na magenge zimesababisha karibu vifo 4,000 mwaka 2024, unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono unaotumiwa kama silaha ya ugaidi, umefikia viwango vya kutisha.
Pia imesema wanawake na watoto wameathiriwa kupita kiasi, huku asilimia 94 ya wanawake na wasichana waliokimbia makazi yao wakiwa katika hatari kubwa ya kudhulumiwa kingono.
Licha ya changamoto hizi, IOM na washirika wake wameahidi kuendelea kutoa msaada wa kuokoa maisha.
IOM pia inatoa wito wa kuongeza haraka ufadhili kwa shughuli za kibinadamu Haiti kwani hadi kufikia mwezi huu wa Novemba, ombi la dola milioni 674 la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Haiti limefadhiliwa kwa asilimia 42 pekee, na kuwaacha mamilioni ya watu bila msaada wanaohitaji.
Mon, 18 Nov 2024 - 12054 - Esneda kutoka jamii ya Yukpa asema haogopi vitisho kutetea eneo la jamii yao ya asili nchini Colombia
Jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia imevumilia miongo kadhaa ya migogoro na watu kutawanywa inayosababishwa sio tu na mabadiliko ya tabianchi mila kandamizi bali pia kupotea kwa viumbe hai na hivyo kutishia maisha yao.
Esneda Saveedra, Kiongozi wa jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia akiwa anazungumza akiketi ndani ya msitu na kando ya mto Maracas., anasema hana hofu ya kutetea ardhi hii.
Ardhi anayozungumzia ni eneo hilo la mto Maracas anayotetea dhidi ya vitisho kutoka kwa waharibifu wa mazingira kufuatia yale yaliyojadiliwa katika mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa bayonuai, COP16 uliomalizika Ijumaa iliyopita huko mjini Cali nchini Colombia.
"Sina hofu ya kutetea ardhi hii. Yale niliyopitia kama mtoto, changamoto zote hizo, yalinipa nguvu, yalinipa ujasiri, na yakaondoa hofu yangu."
Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR inatupatia taswira ya juu ya eneo la makazi ya jamii ya Yukpa, msitu mnene na kisha kwenye mto Maracas, shughuli zinaendelea, wengine wakiogelea, wengine wakivua samaki, mama mmoja akisafisha kuku aliyemaliza kumchuna.
Esneda anaeleza umuhimu wa mto huu kwa maisha ya jamii yake na anaendelea kujitahidi ili kulinda mazingira hayo.
"Huu ni mto Maracas, ambapo watu wetu, mababu zangu, walivua samaki kwa ajili ya chakula kila siku. Waliharibu mazingira kwa kukata miti yote, na matokeo yake, mto ulianza kukauka. Leo, mto Maracas hauna mtiririko wa maji kama ulivyokuwa zaidi ya miaka 20 iliyopita."
Katika juhudi zake, Esneda ameanzisha mazungumzo na maafisa wa serikali katika manispaa ya Becerril, akijaribu kuleta mabadiliko na uelewa juu ya umuhimu wa kuhifadhi ardhi na utamaduni wa watu wa Yukpa.
"Kumekuwa na uratibu, kazi ya pamoja, na jambo muhimu zaidi kwangu kama mwanamke wa Yukpa imekuwa kuleta ufahamu kuhusu watu wa Yukpa na ardhi yetu. Mabadiliko ya tabianchi yametufikisha kwenye tatizo kubwa zaidi, ambalo ni upotevu wa mazao na ukosefu wa chakula. Leo hatuna chakula cha kutosha katika jamii zetu. Tunaendelea kupambana, lakini pia tuko hapa kusaidia dunia nzima kuendelea kupambana na kulinda mazingira, ardhi, na hewa. Na kusema: 'Tupo hapa kuchangia kwa ajili ya ubinadamu, kwa ulimwengu mzima.’"
Harakati zake zimekumbwa na vitisho.
“Walinitishia hapa kwa kuzungumza, na kwa kusema ukweli. Mama yangu alikuwa kiongozi thabiti—na bado ni kiongozi thabiti. Na nilipokuwa mdogo, nilimsindikiza kwenye michakato yake yote ya harakati, mipango na uongozi. Niliendeleza njia hiyo ya uongozi kwa sababu niliona ni muhimu. Ilikuwa ni wajibu wangu. Nilijiambia, ‘mimi ni mwanamke ambaye nimezaliwa kutetea eneo hili.”
Kwa Esneda, kulinda ardhi ya Yukpa ni zaidi ya wajibu; ni dhamira ya kuhifadhi urithi wa mababu zake. Katika changamoto za kila siku, Esneda anabaki imara kwa matumaini kuwa jamii yake na mchango wao katika kuhifadhi mazingira utatambuliwa ulimwenguni.
Fri, 15 Nov 2024 - 12053 - Anne Tek: COP29 isiwape kisogo wanawake wanaokabiliiwa na athari za mabadiliko ya tabianchi Afrika
Mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP29 ukianza wiki ya piili mjini Baku Azerbaijan leo, wito umetolewa kwa wanawake amba oni waathirika wakubwa wa janga la mabadiliko ya tabianchi kutopewa kisogo.
Anne Cheruto Tek ambaye amebeba bendera ya wanawake waathitika wa mabadiliko ya tabianchi kutoka Afrika ameiambia UN News anachokifanya COP29..
“Sana sana kufuatilia haya madhara ya mabadiliko ya tabianchi hasa kwa wanawake na vijana barani Afrika. Sana sana utakuwa wanawake ndio wanaoshughulikia masuala ya maji, masuala ya kuni, masuala ya chakula , lakini mara nyingi kukiwa na janga la mabadiliko ya tabianchi kama ukame, mafuriko, wanawake ndio wanaangamia zaidi, kwa sababu wanawke ndio wanakuwa na jukumu la kuendesha nyumba na hivyo hawana nafasi ya kutafuta fedhha ambaz zinaweza kuwasaidia wakati wa majanga hayo.”
Na kutokana na hayo anasema wanawake hukabiliwa na changamoto kubwa
“Wengi hupata magonjwa , wengi huathhirika sana wakati wa majanga ikiwemo vifo, ukosefu wa fedha na pia ukatili wa kijinsia wakati wa shida za mabadiliko ya tabianchi.”
Na nini ombi lake katika mkutano huo?
Kuhakikisha kuwa hizi changamoto zinaangaziwa hasa kwa masuala ya fedha, kuhakikisha kuwa fedha zinawafikia wanawake vijijini , kuhakikisha kuwa wanaweza kuelewa masuala ya mabadiliko ya tabianchi na pia waweze kuelezea hadithi zao jinsi wanavyoathirika na tunaomba hii COP kuangazia haya majanga hasa kwa wanawake, wasichana na watu wasiojiweza kama wenye ulemavu.”
Fri, 15 Nov 2024 - 12052 - 15 NOVEMBA 2024
- Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 u unaofanyika Baku Azerbaijan, leo umejikita na ongezeko la gesi chafuzi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inatokana na shughuli za binadamu ikiwemo ufugaji wa ng’ombe, na sasa nini kifanyike ili kuidhibiti.Tunasalia huko huko Baku, Azerbaijan. Wito umetolewa kwa wanawake ambao ni waathirika wakubwa wa janga la mabadiliko ya tabianchi wasipewe kisogo katika harakati za kuhimili na kukabili madhara ya janga hilo.Katika makala Bosco Cosmas anatupeleka Amerika ya Kusini kusikia harakati za mwanamke wa jamii ya asili za kulinda eneo lao.Mashinani leo Fathimath, kijana kutoka Maldives anatoa kauli kwa ajili ya hatua za dharura kupambana na mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa COP29.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Fri, 15 Nov 2024 - 12051 - UNEP: Licha ya taarifa za ongezeko la gesi ya methane hatua zinazochukuliwa ni kidogo
Mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP29 unaofanyika Baku Aberbaijana leo umejikita na ongezeko la gesi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na shughuli za binadamu na nini kifanyike kuidhibiti. F
Kulingana na ripoti iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa wa mazingira UNEP katika mkutano huo, mfumo wa teknolojia ya hali ya juu ambao unatambua uvujaji mkubwa wa gesi ya methane umewasilisha tarifa 1,200 kwa serikali na makampuni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, lakini ni asilimia moja tu ya taarifa hizo ndizo zilizofanyiwa kazi.
Ripoti hiyo mpya iliyopewa jina “Jicho kwenye methane: Haionekani lakini inashuhudiwa” inasema licha ya ahadi zilizotolewa chini ya makubaliano ya ahadi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi ya methane kwa asilimia 30 ifikapo 2030 hatua zinazochukuliwa hazitoshelezi kupunguza gesi hiyo.
Ripoti imeangazia tahadhari za methane kutoka kwenye Mfumo wa Tahadhari na hatua dhidi ya Methane MARS, ambayo ni sehemu ya UNEP ya uangalizi wa kimataifa wa uzalishaji wa methane IMEO ambayo unawakilisha fursa ambazo haijatumiwa kwa hatua za haraka dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Akizindua ripoti hiyo Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, amesema ili kuwa na nafasi yoyote ya kudhibiti ongezeko la joto duniani, uzalishaji wa methane lazima ushuke, na ushuke haraka.
"Tunapozingatia kuwa ni asilimia 1 tu ya taarifa 1200 ambazo tulitoa ndizo zilisababisha hatua kuchukuliwa, basi hauitaji kuwa mtaalamu wa hesabu ili kuhesabu ushindi mkubwa unaowezekana hapa. Tuna mifumo iliyothibitishwa ya kutambua uvujaji Mkubwa wa gesi ya methane ili uweze kukomeshwa haraka, mara nyingi kwa ukarabati rahisi na wakati mwingine tunazungumza juu ya kukaza mipira au kubadilisha vichungi.”
Ameongeza, kuwa "Serikali na makampuni ya mafuta na gesi ambayo sehemu kubwa ya uchumi wa dunia bado inawategemea lazima waache kupiga domo kwa changamoto hii wakati majawabu yanawatazama usoni. Badala yake, wanapaswa kutambua fursa muhimu ambayo mfumo huu unatoa na kuanza kuchukua hatua kutokana na taarifa kwa kuziba uvujaji ambao unamwaga gesi ya methane ya joto kwenye angahewa.”
Amehitimisha kwa kusema, "Serikali na sekta binafsi lazima zizuie uzalishaji wa methane, na lazima zifanye hivyo sasa."
Gesi ya Methane kwenye angahewa ni kichocheo cha pili kikubwa cha ongezeko la joto duniani baada ya hewa ya ukaa au CO2 na ina nguvu zaidi ya mara 80 kuliko hewa ya ukaa katika kusambaa kwa muda mfupi.
UNEP imesisitiza kuwa utoaji wa gesi ya methane duniani lazima upunguzwe kwa asilimia 40 hadi 45 ifikapo 2030 ili kufikia njia za gharama nafuu zinazopunguza ongezeko la joto duniani hadi kufikia nyuzi joto 1.5°C.
Bado taarifa za sayansi za hivi karibuni zinaonyesha viwango vya angahewa vya methane vimepanda kwa kasi iliyovunja rekodi katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.
Fri, 15 Nov 2024 - 12050 - Jifunze Kiswahili - Ufafanuzi wa maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”Thu, 14 Nov 2024
- 12049 - 14 NOVEMBA 2024
- Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa kisukari, shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limesema idadi ya watu wazima wanaoishi na Kkisukari duniani ni zaidi ya milioni 8000 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 4 tangu mwaka 1990.Baku Azerbaijan ambako mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 leo umejikita na na lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres ameainisha jukumu muhimu ambalo miji, mikoa, biashara na taasisi za kifedha lazima zitekeleze katika kuendesha juhudi za dunia nzima kufikia lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa katikati ya karne hii.Nchini Sudan shirika la Umojja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharida OCHA limesema ghasia za kutumia silaha na mashambulizi katika Jimbo la Aj Jazirah zinadhihirisha ukatili wa karibu miezi 19 ya vita nchini Sudan,huku kukiwa na ripoti za ubakaji, mauaji ya halaiki na uporaji mkubwa. Katika chini ya wiki mbili, OCHA inasema uhasama huko Aj Jazirah umefurusha zaidi ya watu 135,000 kutoka makwao, wengi wao walikimbilia majimbo jirani ya Gedaref na Kassala.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Thu, 14 Nov 2024 - 12048 - Wananchi tufahamishwe kwa kina majukumu ya MONUSCO ili kukabili habari potofu DRC
Umoja wa Mataifa unatambua ni kwa kiasi gani habari potofu na habari za uongo kuwa ni mojawapo ya vikwazo vikuu vinavyokabili operesheni zake za kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Hii imesababisha Umoja huo kuhaha kila wakati kuona ni kwa vipi itakabiliana na habari hizo, iwe ni kupitia mafunzo kwa wanahabari, au kusaidia ujenzi wa vyombo vya habari, na hata kuzungumza na wananchi. Hivi karibuni Umoja Wa Mataifa kupitia Idara yake ya Ulinzi wa Amani, kitengo cha uadilifu wa habari, ulituma Tume yake Mashariki mwa DRC kukutana na wakazi ili kujua ni nini Umoja wa Mataifa unapaswa kufanya ili kupambana na habari potofu na za uongo nchini humo. Mwandishi wetu wa Mashariki mwa DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini, George Musubao alishuhudia ziara hiyo na ametuletea makala hii.
Wed, 13 Nov 2024 - 12047 - Patricia Kombo COP29: Ufadhili wa fedha utakuwa jawabu mujarabu kudhibiti mabadiliko ya tabianchi Afrika
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 leo ukiingia siku ya nne mjini Baku Azerbaijan vijana kutoka Afrika wataka ufadhili uongezwe kutoka mataifa makubwa hususan yanayochangia zaidi hewa ukaa ili kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mataifa yanayoendelea ambapomiongoni mwa waathirika wakubwa ni vijana.
Asante Bosco na mmoja wa washiriki hao ni Patricial Kombo Mumbua kutoka Kenya akiwasilisha matakwa ya vijana katika mkutano huo, na akizungumza na UN News kuhusu ujumbe wake kwa COP29 amesema
“Kwangu kama kiongozi wa vijana jambo la kwanza ni kuweza kupata zile fedha au kuzikusanya ili ziweze kusaidia mataifa ambayo yanapambana na kukabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi . Pili ni kuhakikisha kuwa viongozi kutoka mataifa ambayo yanazalisha zaidi hewa ukaa yanawajibika ili kuyafanya matifa ambayo yanaendelea kuweza kujilinda , kunufaika , kujiinua dhidi ya janga hilo na pia kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika jamii zao.”
Na nini anachokitarajia katika mkutano huo wa COP29?
“Ni kuweza kuona kuwa hili kongamano litaweza kuhamasisha upatikanaji wa hizo hela kwa mataifa ambayo yanakabiliwa na hizi changamoto za mabadiliko ya tabianchi, Na pia wakati ambapo mataifa yanaendelea kurekebisha michango yao ya kitaifa ya mabadiliko ya tabianchi au NDCs, waweze kuleta michango ambayo inaaambatana na zile changamoto ambazo mataifa yao yanazidi kuathiirika nazo za mabadiliko ya tabianchi.”
Mbali ya masuala ya ufadhil mada zingine zinazotamalaki kwenye mijadala ya leo COP29 ni masuala ya nishani safi , mifumo ya tahadhari za mapemba na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa matifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea.
Wed, 13 Nov 2024 - 12046 - 13 NOVEMBA 2024
- Kuongeza kiwango cha fedha kwenye ufadhili wa miradi ya kukabili na kuhimili tabianchi nchi ikiwa ni moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan, leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bila kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi, na kuimarisha miradi ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kila uchumi duniani utakumbwa na madhara makubwa.Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuriko ya msimu yanayokumba eneo hilo mara kwa mara, eneo ambalo ardhi yake ina rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara.Katika Makala George Musubao, mwandishi wetu huko Jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akimulika mkutano ulioandaliwa na watendaji wa Umoja wa Mataifa ya eneo hilo kuangalia jinsi ya kukabiliana na habari potofu na za uongo.Na mashinani tutakuwa Sudan Kusini, ambako shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linasaidia jamii zilizoathiriwa na mafuriko kupata suluhisho la kudumu.
Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Wed, 13 Nov 2024 - 12045 - UNHCR Sudan Kusini yachukua hatua kupunguza madhara ya mafuriko katika sekta ya kilimo
Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ,UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuriko ya msimu yanayokumba eneo hilo mara kwa mara, eneo ambalo ardhi yake ina rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara.
Hapa shambani jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini, wakulima wakiwemo wenyeji na wakimbizi wakiwa shambani wakiimba. Awad Usman mwenyeji wa hapa anasema kuimba kunatuliza fikra zangu. Nyimbo hazisaidii kupanda mazao, lakini zinaweza kupunguza msongo wa mawazo.
Msongo wa mawazo unatokana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi yaletayo mvua kubwa na mafuriko kwenye mashamba yao.
Awad anasema nakumbuka mafuriko ya mwaka 2019, yalisomba kila kitu. Ufuta wote ulisombwa. Mtama pekee ulisalia. Tulikaa ndani ya nyumba kwa siku tano, na tulipotoka tulikuta shamba zima limetwama kwenye maji.
Alex Noel Kilong, afisa wa UNHCR anasema mafuriko yanaongeza machungu kwa shida ambazo tayari jamii inakumbana nazo. Mafuriko yanazidi kuongezeka na kusoma barabara, mifugo, mashamba na vituo vya afya hivyo anasema..
“Tunahitaji kujenga mbinu za kujipatia kipato. Maban ina fursa kubwa sana, udongo una rutuba, tunatakiwa pia kujenga mapipa ya kuhifadhi maji juu ya ardhi, na maji haya yanaweza kutumiwa wakati wa ukame, ili kilimo kiwe shughuli inayoweza kufanyika mwaka mzima. Kwa njia hiyo tutaweza kupunguza njaa. Tutapunguza ukosefu wa uhakika wa chakula miongoni mwa wenyeji na pia kwa wakimbizi.
UNHCR pia imepatia wakulima kama Awad mbegu ya ufuta mweupe, ambayo anasema ni bora na hivyo atakavyovuna , kiasi atauza na nyingine atahifadhi kwa matumizi ya kula nyumbani na pia kama mbegu.
Wed, 13 Nov 2024 - 12044 - 12 NOVEMBA 2024
- Kuongeza kiwango cha fedha kwenye ufadhili wa miradi ya kukabili na kuhimili tabianchi nchi ikiwa ni moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan, leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bila kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi, na kuimarisha miradi ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kila uchumi duniani utakumbwa na madhara makubwa.Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyotolewa leo huko COP29 inaonesha ni kwa jinsi gani watu wanaokimbia vita, ghasia na mateso wanazidi kujikuta kwenye mazingira yaliyokumbwa na janga la tabianchi, janga ambalo linawaweka kwenye mchanganyiko wa vitisho, lakini bila fedha wala msaada wa kukabiliana navyo.Na mamia ya wakimbizi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu sasa watafanya bure mitihani ya kuonesha umahiri wao wa lugha ya kiingereza, au IELTS. Hii inafuatia makubaliano ya ushirikiano kati ya UNHCR na mfumo wa kimataifa wa lugha ya kiingereza, IELTS.Na mashinani COP29 ukiendelea huko Baku Azerbaijan, tunabisha hodi nchini Zimbabwe ambako Umoja wa Mataifa unawasaidia wakulima kakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Tue, 12 Nov 2024 - 12043 - Kozi za Kiswahili ziongezwe ili watu wengi zaidi wajifunze duniani kote- 'Bongo Zozo'
Kongamano la kimataifa la Kiswahili limefunga pazia mwishoni mwa wiki mjini Havana Cuba ambako washiriki takriban 400 kutoka barani Afrika, Ulaya, Asia na Aamerika wamejadiliana mada mbalimbali za kukuza na kupanua wigo wa lugha hiyo ya Kiswahili duniani. Hata hivyo wapenzi wa lujifunza lugha hiyo wanataka kozi za kujifunza Kiswahili kwa wageni ziongezwe katika sehemu nyingi zaidi ili kutoa fursa kubwa kwa wanaotaka kujifunza kama alivyobaini Flora Nducha alipozungumza na mmoja wa wachechemuzi wa lugha hiyo ya Kiswahili Nick Reynold au Bongo Zozo. Ungana nao katika Makala hii
Mon, 11 Nov 2024 - 12042 - Stiell: Lazima tuweke malengo ya juu ya ufadhili ili kukabili mabadiliko ya tabianchi
Kufuatia mwaka mwingine wa viwango vya juu vya joto kali na matukio ya kupitiliza ya hali ya hewa, Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi Simon Stiell amewaeleza washiriki wa mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 , kwamba malengo mapya ya ufadhili kwa tabianchi ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa mataifa, yakiwemo yale tajiri na yenye uthabiti.
Katika hotuba yake mbele ya washiriki wa mkutano huo ulioanza leo huko Baku, mji mkuu wa Azerbaijan hadi tarehe 22 mwezi huu wa Novemba, Bwana Stiell amesema kwa kadri madhara ya mabadiliko ya tabianchi yalivyo dhahiri ni lazima kukubaliana mwelekeo mpya wa ufadhili kwa miradi ya kukabili na kuhimili.
Amehoji, mnataka bei za vyakula na nishati iongezeke zaidi? Je mnataka nchi zenu ziendele kushindwa kushindana kiuchumi? Je mnataka dunia yetu iendelee kukosa utulivu na kugharimu maisha adhimu?
Amekumbusha kuwa janga la tabianchi linaathiri kila mkazi wa dunia kwa njia moja au nyingine.
Bwana Stiell amesema nimekanganyikiwa kama mtu mwigine yeyote kwamba mkutano mmoja wa COP hauwezi kuleta marekebisho abayo kila taifa linahitaki. Lakini iwapo majibu yenu kwenye maswali hayo ni HAPANA, basi ni hapa pande zote zinahitaji kukubaliana jinsi ya kuondokana na zahma hii.
Hivyo amesema, “katika nyakati ngumu, kukiwa na majukumu mazito, sitegemei matumaini na ndoto. Kinachonihamasisha ni stadi na azma ya binadamu. Uwezo wetu wa kuanguka na kuinuka tena na tena, hadi tunapotimiza malengo yetu.”
Amekumbusha kuwa mkataba wa tabianchi ndio mchakato pekee ambapo wanaweza kupatia majawabu janga la tabianchi na kuwajibishana kwa wale wanaokwenda kinyume.
Ametaka washirika kuonesha stadi zao kwenye COP29 na pande zote zishinikize makubaliano ya ufadhili kwa tabianchi la sivyo kila nchi itagharimika.
Mon, 11 Nov 2024 - 12041 - 11 NOVEMBA 2024
- Kufuatia mwaka mwingine wa viwango vya juu vya joto kali na matukio ya kupitiliza ya hali ya hewa, Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi Simon Stiell amewaeleza washiriki wa mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29, kwamba malengo mapya ya ufadhili kwa tabianchi ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa mataifa, yakiwemo yale tajiri na yenye uthabiti.Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuchagiza kaya kulima bustani za mboga za majani pamoja na ufugaji wa kuku huko jimbo la Afar, kaskazini mashariki mwa Ethiopia umesaidia familia za vijijini kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto.Makala inatupeleka Havana Cuba ambako kongamano la kimataifa ka Kiswahilii limekunja jamvi mwishoni mwa wiki na shuhuda wetu huo Flora Nducha amezungumza na watu mbalimbali akiwemo mchechemuzi wa Kiswahili hususan kwenye mitandaao ya kijamii Nick Reynold ali maarufu Bongo Zozo, ambaye ni raia wa Uingereza.Na mashinani fursa ni yake Profesa msaidizi Xiaoxi Zhang raia wa China ambaye ni mshirika wa kimataifa au (Global Fellow) na mhadhiri wa masuala ya fasihi linganishi katika chuo kikuu cha Habib kilichopo Sindhi Karachi nchini Pakistan mmoja wa waliohudhuria kongamano la Kiswahili lililomalizika mwishoni mwa wiki akitoa ujumbe kuhusu changamoto ya kujifunza Kiswhili.
Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Mon, 11 Nov 2024 - 12040 - Mradi wa UNICEF wa kuboresha lishe waleta tabasamu kwa wazazi na watoto Afar Ethiopia
Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kuchagiza kaya kulima bustani za mboga za majani pamoja na ufugaji wa kuku huko jimbo la Afar, kaskazini mashariki mwa Ethiopia umesaidia familia za vijijini kukabiliana na utapiamlo miongoni mwa watoto.
Video ya UNICEF Ethiopia inaanza ikimuonesha mtoto akitabasamu, na kisha akiwa na mama yake wakielekea kwenye kituo cha afya. Mama huyu anaitwa Fatuma Kebir na mwanae huyu aliyembeba anaitwa Abdu. Fatuma anasema..
“Nilihofia kuwa angeendelea kuwa na utapiamlo. Kwa hiyo nilimpeleka kituo cha afya na mhudumu wa afya akanieleza kuwa mwanangu amepoteza uzito, kama ambavyo nilihisi. Akaniambia nimlishe zaidi, hasa uji uliochanganywa na mayai, maziwa, na mboga.”
Video ikimuonesha Fatuma akiandaa uji akichanganya na mayai, mtaalam wa lishe wa UNICEF, Yetayesh Maru, anasema,
“Kama sehemu ya mtambuka wa hatua na uratibu dhidi ya utapiamlo kwenye jamii, Fatuma ametambuliwa kuwa ni kaya iliyo hatarini, hivyo amenufaika na mradi wa kisekta wa kuboresha lishe kwa watoto.”
Sasa Fatuma na mtoto wake Abdu wanapata tabasamu upya.
“Nilimlisha kwa mwezi mmoja kama walivyoshauri na kisha nikarudi kituo cha afya. Mtoa huduma alisema kwamba sasa ana afya na amerudia uzito wake. Nilifurahi sana alipoanza kuongezeka uzito.”
Tabasamu lao ni dhahiri hata kwa mtoa huduma Yetayesh, akisema “Sasa Abdul anakua vizuri, na nguvu kamilifu, huku akicheka na mama yake.”
Mon, 11 Nov 2024 - 12039 - Tutahakikisha Kiswahili kinasambaa duniani na kusongesha ajenda za UN: Dkt. Ndumbaro
Kongamano la kimataifa la Kiswahili leo limeng’oa nanga jijini Havana Cuba likiwaleta pamoja takribani washiriki 400 kutoka Afrika, Asia, Amerika na Ulaya ili kujadili ajenda mbalimbali za kupanua wigo wa luugha hiyo na kuitumia kuleta tija ikiwemo kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa kama amani na maendeleo endelevu. Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa wakati wa Kongamano hilo Waziri wa utamaduni, sanaa na michezo wa Tanzania Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amesema hili ni kongamano la kimataifa la Kiswahili na ajenda yake kuu ni kukifanya Kiswahili kivuke mipaka.
Fri, 08 Nov 2024 - 12038 - 08 NOVEMBA 2024
Miongoni mwa habari kubwa Umoja wa Mataifa hii leo ni uwajibikaji unasakwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wapalestina na waisraeli, na pia shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limeweka bayana gharama za kiuchumi na hata kiafya zilizofichika zitokanazo na mifumo ya uzalishaji, usafirishaji na ulaji wa chakula. Lakini kubwa zaidi nakupeleka Havana, Cuba kupata kwa mahtasari mazungumzo ya Flora Nducha na mmoja wa washiriki.
Mashinani tunasalia huko huko Havana Cuba na fursa ni yake Profesa Juan (Huani) Jacomino (Hakumino) raia wa Cuba ambaye ni Mwalimu wa Kiswahii katia chuo kikuu cha Havana Cuba anayeshiriki Kongamano la Kiswahili lililofunguliwa leo akitoa wito kwa raia wa Cuba na wa nchi zingine kuhusu umuhimu wa kukumbatia Kiswahili.
Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu!
Fri, 08 Nov 2024 - 12037 - Fahamu kuhusu faida za kidiplomasia na kiuchumi zilizoletwa na lugha ya Kiswahii kisiwani Zanzibar
Huko Havana Cuba mambo yanaendelea kuiva kwenye Kongamano la kimataifa la Kiswahili huku wageni wakitoka katika kila pembe ya dunia kushiriki. Miongoni mwao ni Waziri Tabia Maulid Mwita kutoka Zanzibar ambaye amezungumza na shuhuda wetu katika kongamano hilo Flora Nducha kuhusu faida za kiplomasia na kiuchumi zilizoletwa na lugha ya Kiswahii Kisiwani Zanzibar.
Thu, 07 Nov 2024 - 12036 - 07 NOVEMBA 2024
- Fedha kwa ajili ya mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ni jambo lililopatiwa kipaumbele katika ripoti mpya ya leo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP wakati huu ambapo kiwango cha joto kinazidi kuongezeka kila uchao na kuleta zahma duniani kote.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema hii leo watoto 6 wa kipalestina, wamesafirishwa kutoka Gaza kwenye Romania kwa matibabu mahsusi ; watatu wakiwa wanaugua saratani, wawili magonjwa ya damu na mmoja majeraha. Wameambatana na jumla ya waangalizi 15.Na huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umezindua mfumo wa uthibitishaji, kama sehemu ya mchakato wa Luanda wenye lengo la kufuatilia makubaliano ya sitisho la mapigano kati ya Rwanda na DRC yaliyoanza kutekelezwa tarehe 4 mwezi Agosti mwaka huu mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunasalia huko huko Havana Cuba, kwenye kongamano la Kiswahili la Kimataifa ambako Dkt. Kisembo Ronex Tendo mshiriki kutoka taasisi ya vijana ya Afrika Mashriki Fest Uganda anaeleza cha kufanya kusongesha Kiswahili nchini Uganda.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Thu, 07 Nov 2024 - 12035 - Uganda imechukua hatua kuhakikisha Kiswahili kinazungumzwa shuleni hadi bungeni: Dkt. Tendo
Kwa kutambua thamani na mchango Mkubwa wa lugha ya Kiswahili katika Kanda ya Afrika Mashariki na kimataifa, sasa serikali ya Uganda imeivalia njuga lugha hiyo kwa kuweka mikakati maalum ya kuhakikisha inafundishwa na kuzungumzwa kuanzia shuleni hadi Bungeni. Flora Nduha wa Idhaa hii aliyeko mjini Havana Cuba kutujuza yanayojiri katika kongamano la kimataifa la Kiswahili amebainni hayo alipozunggumza na mmoja wa washiriki kutoka nchini Uganda.
Wed, 06 Nov 2024 - 12034 - Guterres ampongeza Donald J. Trump kwa kuchaguliwa Rais wa Marekani
Kufuatia Donald J Trump kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Jumanne Novemba 5, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa salamu za pongezi.
Taarifa iliyotolewa Jumatano asubuhi jijini New York, Marekani na msemaji wa Umoja wa Mataifa, imemnukuu Guterres akisema napongeza wananchi wa Marekani kwa ushiriki wao katika mchakato wa demokorasia.
Kisha akasema nampongeza Rais Mteule Donald J. Trump na ninarejelea imani yangu kwamba ushirikiano kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa ni nguzo muhimu ya uhusiano wa kimataifa.
Guterres amesema Umoja wa Mataiifa uko tayari kufanya kazi kwa kina na serikali ijayo ya Marekani il ikutatua changamoto kubwa zinazokabili dunia hivi sasa.
Trump ambaye anawakilisha chama cha Repablikani, anakuwa Rais wa 47 wa Marekani.
Amemshinda Makamu wa Rais Kamala Harris ambaye alikuwa anagombea kiti cha urais kupitia chama cha Demokrati.
Hii ni mara ya pili Trump ataongoza Marekani kwani alikuwa Rais wa 45 wa Marekani kuanzia Januari 20, 2017 hadi Januari 20, 2021 baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2016.
Wed, 06 Nov 2024 - 12033 - 06 NOVEMBA 2024
- Kufuatia Donald J. Trump kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Jumanne Novemba 5, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa salamu za pongezi.Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC za kunasua watoto na vijana wanaotumikishwa vitani zinaendelea na tukio la hivi karibuni zaidi ni la kijana..Makala leo inatupeleka Havana Cuba ikiwa imesalia siku moja tu kabla ya kuanza kwa kongamano la kimataifa la Kiswahili lililobeba maudhui “Kiswahii na teknolojia, na Kiswahili kama nyenzo ya kudumisha amani na maendeleo”.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kwa mwanamke mwandishi wa habari akitueleza jinsi wanavyochochea haki za binadamu.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Wed, 06 Nov 2024 - 12032 - Simulizi ya Ombeni baada ya kutoroka waasi na kurejea uraiani huko DRC
Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC za kunasua watoto na vijana wanaotumikishwa vitani zinaendelea na tukio la hivi karibuni zaidi ni la kijana.
Katika video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ombeni anasimulia jinsi waasi wa FDLR mashariki mwa DRC walivyowakamata msituni.
"Tulikuwa vijana watanoFDLR walitukamata na kutupeleka msituni. Maisha ilikuwa ngumu sana na hatukuweza kutoroka"
Kazi wanatumikishwa bila mshahara na zaidi ya yote.
"Kila saa ni mateso, kazi mingi bila malipo."
Alitumikishwa msituni kwa miaka minane, akionesha makovu ya vipigo alivyopatiwa.
"Tuliteseka sana, tulitumikishwa kwa muda wa miaka minane, tukachapwa viboko, tuliumizwa sana na kubaki na majeraha"
Lakini siku moj aliweza kutoroka. Akiwa Kibirizi akamweleza mkubwa wake ya kwamba..
" Siku moja nikamwambia mkubwa wangu naenda kusalamia rafiki yangu, wakati huo tukapata nafasi ya kutoroka."
Katika harakati hizo akakutana na MONUSCO. Anasema kwamba, "Njiani nikakutana na wanajeshi wa MONUSCO, nikainua bunduki juu na kujisalimisha, nikisindikizwa na mkubwa wao nikaeleza kile tulichopitia"
Sasa Ombeni anashiriki programu za kumjumuisha tena kwenye jamii, DDR-S inayondeshwa na MONUSCO huko Beni, jimboni Kivu Kaskazini.
Wed, 06 Nov 2024 - 12031 - 05 NOVEMBA 2024
- Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Miji Duniani, WUF12 umeingia siku ya pili hii leo huko Cairo, Misri, ambako Ming Zing ambaye ni Mkurugenzi wa Miji, Mnepo na Ardhi kutoka Benki ya Dunia amezungumzia umuhimu wa kujumuisha wanawake na vijana katika mipango miji.Sudan imekuwa nchi ya 16 barani Afrika na ya kwanza katika Ukanda wa WHO wa Mashariki na Mediterania kuanzisha chanjo dhidi ya Malaria kwa watoto wasiozidi umri wa miezi 12. Chanjo imeanza kutolewa jana katika majimbo ya Gedaref na Blue Nile ambapo WHO na wadau wamesema mwaka 2025 na 2026 chanjo itapelekwa katika maeneo 129 nchini kote Sudan.Na leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu tsunami, ambayo ni mawimbi makubwa ya maji yatokanayo na tetemeko chini ya bahari. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake anasema pamoja na kukumbuka waliopoteza maisha kwa tsunami miaka 20 iliyopita, tunaahidi tena kulinda zaidi ya watu milioni 700 duniani kote walio hatarini kukumbwa na Tsunami.Mashinani tutaelekea Sudan kusini kuangazia harakati za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS za kuimarisha ulinzi wa wanawake katika migogoro na majanga.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Tue, 05 Nov 2024 - 12030 - Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wasaidia watoto yatima huko Beni, DRC
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mapigano kati ya jeshi la serikali, FARDC na vikundi vilivyojihami, yamesababisha vifo na hata watu kufurushwa makwao. Watoto wamesalia yatima na hawana walezi. Vituo vya kulea watoto yatima vimebeba jukumu la kuwatunza, lakini navyo viko taabani. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa, kutoka Tanzania, TANZBATT-11 wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO waliguswa na kuamua kujiongeza na kuwasilisha msaada kwa watoto hao. Afisa Habari wa TANZBATT-11 Kapteni Fadhillah Nayopa anasimulia kile walichofanya.
Mon, 04 Nov 2024 - 12029 - UN: Baada ya janga la njaa, sasa kipindupindu na homa ya kidingapopo yaikumba Sudan
Nchini Sudan ambako vita na njanga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani.
Asante Assumpta kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA na lile la afya duniani WHO, hali inazidi kuwa mbaya Sudan ambako katikati ya vita majanga mingine ya kiafya yanazuka.
OCHA imeripoti zaidi ya wagonjwa 28,000 wa kipindupindu na vifo vimefikia 836 katika majimbo 11 kati ya 22 Julai na 28 Oktoba mwaka huu huku likihofia kwamba idadi kamili ya wagonjwa huenda ni kubwa zaidi.
Pia shirika hilo limeonya juu ya kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa homa ya kidingapopo na mvua zinazonyesha na kusababisha mafuriko makubwa zimeongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa hayo.
Nalo shirika la WHO linasema milipuko hii imezuka wakati mfumo wa huduma ya afya nchini Sudan umzidiwa uwezo, huku hospitali nyingi hazifanyi kazi au zimefungwa kabisa kutokana na usambazaji mdogo wa vifaa na uhaba wa mafuta. Shirika hilo linasema hadi asilimia 80 ya vituo vya afya katika maeneo yenye migogoro ikiwa ni pamoja na Al Jazirah, Kordofan, Darfur na Khartoum aidha havifanyi kazi au vimefungwa.
Na linaonya kwamba "Kuporomoka huku kwa mfumo wa afya kunazuia mipango ya chanjo ya watoto, kuongeza kasi ya kuenea kwa magonjwa yanayozuilika, na kuzua wasiwasi kuhusu uwezekano wa milipuko mikubwa zaidi ya magonjwa."
Kwa sasa mashirika hayo yamesema majimbo yaliyoathirika zaidi na kipindupindu ni Kassala Gedaref, Al Jazirah, na Northern wakati homa ya kidingapopo imeghubika zaidi majimbo ya Kassala na Khartoum.
Pia changamoto nyingine kubwa ya kutoa huduma za afya katikati ya milipuko hii mashirika hayo yanasema ni mashambulizi dhidi ya vituo vya afya ambayo tangu kuanza kwa vita 15 Aprili mwaka jana yamefikia 116 na kusababisha vifo 188 na majeruhi 140.
Mon, 04 Nov 2024 - 12028 - 04 NOVEMBA 2024
- Nchini Sudan ambako vita na janga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani.Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika.Makala inakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako Kapteni Fadhillah Nayopa, Afisa habari wa kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania, TANZBATT-11 katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO anazungumzia usaidizi waliopatia watoto yatima.Mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula, tunakutana na Geoffrey Nawet, Mwanafunzi katika shule ya Kakuma nchini Kenya akitueleza jinsi ambavyo programu ya Mlo shuleni ya lishe bora umewawezesha wanafunzi kumakinika shuleni na kupata motisha ya kuendelea na masomo.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Mon, 04 Nov 2024 - 12027 - UNICEF na wadau Somalia wafanikisha mradi wa maji kwa wakazi wa Galmudug
Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika.
Tuko Adale, mji wa ndani zaidi wa jimbo la kati mwa Somalia, Galmudug. Hapa zaidi ya kaya 2,000 sasa zina huduma ya maji safi na salama, kufuatia ukarabati wa kisima cha maji.
Salada Mohammed Omar, yeye ni mfugaji na ni shuhuda wa mradi huu uliotekelezwa na serikali ya jimbo la Galmudug kwa ufadhili wa shirika la Marekani la Misaada ya kimaendeleo USAID na UNICEF.
“Tulisafiri muda mrefu kuteka maji, lakini sasa kisima kiko karibu na makazi yetu, tunapata kwa urahisi maji ya kupikia, kufulia na kufanyia usafi.”
Video ya UNICEF inaonesha raia na ngamia wakiwa kisimani. Mohammed Yusuf Dirshe ambaye ni kiongozi wa kijamii hapa Adale anasema “awali hakukuwa na tanki la maji wala pampu. Kwa hiyo ilikuwa vigumu kupata maji kwa ajili ya mifugo. Lakini sasa unaona hawa ngamia wanatoka umbali wa hadi wa kilometa 35.”
Issack Mohammed, kutoka Kituo cha Amani na Demokrasia mdau wa mradi huu anaeleza kilichofanyika.
“Ukarabati ulihusisha kujengea juu matanki, kuweka pampu inayotumia nishati ya jua, na kioski cha maji ili wavulana, wasichana na wanawake waweze kuteka maji kwa urahisi.
UNICEF inasema mradi huu unarejesha uhai hapa Adale, kwa kuhakikisha watoto wanakua wakiwa na afya njema, jamii zinastawi na mbinu za kujipatia kipato zinakuwa endelevu.
Mon, 04 Nov 2024 - 12026 - Asante WFP kwa msaada wa pesa taslim uliotuwezesha kiuchumi - Esther Josephine
Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Chakula Duniani WFP, ungali unaendelea kuwasaidia wakimbizi wa ndani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kurejesha tabasamu la waliopoteza makazi yao kutokana na hali ya ukosefu wa usalama nchini humo. Chakula na pesa taslimu zilitolewa kwa wale wanaohitaji jimboni Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC. Mwandishi wetu George Musubao amekutana na Esther Josephine, mama wa watoto 3 aliyekimbia kutoka Kitsanga kwa sababu ya mapigano kati ya jeshi la serekali ya DRC (FARDC) na waasi wa M23, na anatueleza jinsi mama huyu amewezakujikwamua kiuchumi katika makala hii.
Fri, 01 Nov 2024 - 12025 - UNICEF Kenya wafanikisha mapambano dhidi ya kipundupindu Lamu
Serikali ya Kaunti ya Lamu katika pwani ya kaskazini ya Kenya, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanaendesha shughuli ya kuwafikia wanajamii ili kubadilishana taarifa kuhusu jinsi watu wanaweza kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kutoa huduma za maji, vifaa vya kujisafi na usafi kwa jamii zilizoathirika. Kutoka katika video iliyoandaliwa na UNICEF.
Wamekaa chini ya mti, wanawake kwa wanaume. Nyuma ni nyumba ya makuti na matumbawe, Lamu, Pwani ya Kenya. Muelimishaji wa masuala ya afya anawaeleza namna ya kuweka mazingira safi ili kupambana na kipindupindu. Mwanajuma Kahidi yamewahi kumkuta. Anaposema Cholera anamaanisha hiyo hiyo kipindupindu iliyokuwa imetishia Uhai wake na familia yake.
“Nilipopata maambukizi ya Kipindupindu nilihisi siko sawa kwa sababu nilikosa nguvu na nikakosa raha na nikapoteza nuru ya macho ndio nikakimbilia hospitali. Huo ugonjwa ulipitia kwenye maji na chakula. Mimi na watoto wangu tulipatwa na kipindupindu. Mimi nilichukua siku tatu. Watoto wangu wote mmoja baada ya mwingine walichukua siku nane nane. Madaktari wanajibidiisha sana juu yetu. Baada ya siku kadhaa wanajitokeza na kutuuliza, je mnafanya juhudi tulizowaambia?”
Leila Abrar ni Mshauri katika UNICEF anayehusika na mabadiliko ya tabia katika jamii anasema, "kiwango cha ufahamu ni cha juu zaidi kuliko tulipokuwa tunaanza uelimishaji. Na pia tunaambiwa kuwa kiwango cha unawaji mikono kimeongezeka. Mabadiliko ya kijamii na tabia kwa kweli yanahusu kushirikisha jamii, kuwezesha jamii.
Fri, 01 Nov 2024 - 12024 - 01 NOVEMBA 2024
- Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza inazidi kuzorota huku raia na hata wafanyakazi wa kutoa misaada wakisalia wamepigwa butwaa kwani mashambulizi kutoka Israeli yanaendelea kila uchao.Serikali ya Kaunti ya Lamu katika pwani ya kaskazini ya Kenya, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanaendesha shughuli ya kuwafikia wanajamii ili kubadilishana taarifa kuhusu jinsi watu wanaweza kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kutoa huduma za maji, vifaa vya kujisafi na usafi kwa jamii zilizoathirika. Kutoka katika video iliyoandaliwa na UNICEF.Makala George Musubao, mwandishi wetu wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC anazungumza na mkimbizi Esther Josephine aliyeko kambi ya Bulengo nje kidogo ya mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini ambaye amenufaika na msaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.Mashinani tutakuwa Lebanon, kumsikia mama aliyenusurika kifo na wanawe kutokana na makombora ya Israel.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Fri, 01 Nov 2024 - 12023 - Raia na hata wahudumu wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza wamekata tamaa
Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza inazidi kuzorota huku raia na hata wafanyakazi wa kutoa misaada wakisalia wamepigwa butwaa kwani mashambulizi kutoka Israeli yanaendelea kila uchao.
Naanzia ndani ya hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza, mtoto aliyejeruhiwa amebebwa akilia kwa uchungu. Kwingineko mgonjwa mwingine anatolewa kwenye gari la wagonjwa! Ni taswira iliyozoeleka sasa Gaza.
Louise Wateridge ambaye ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Dharura katika shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kutoka Gaza Kati amesema hali si hali.
Anasema, “mambo kwa kweli yanazidi kuwa mabaya hapa. Kukata tamaa ni kila mahali. Namaanisha, watu unaozungumza nao, na wafanyakazi wenzangu niliozungumza nao hawajui sasa wafanye nini. Hawafahamu waende wapi. Unaweza kusikia nyuma yangu milio ya makombora ikiendelea.”
Bi. Wateridge akaendelea kusema kuwa, “kutokuwa na matumaini ndio neno pekee lililosalia Gaza. Unafahamu watu milioni 2.2. Inabidi umkumbushe kila mtu kwamba wamenasa. Hakuna njia ya kutoka nje ya Ukanda wa Gaza na mashambulio ya mabomu yanaendelea mchana kutwa na usiku kucha.”
Hali ikiendelea hivyo hii leo huko katikati mwa Gaza, hapo jana jeshi la Israeli lilishambulia na kuharibu kwa kiasi kikubwa ofisi ya UNRWA iliyoko Ukingo wa Magharibi, ofisi ambayo ilikuwa inategemewa zaidi katika kutoa msaada kwa wakimbizi zaidi ya 14,000 wa kipalestina wanaoishi katika kambi ya Nur Shams.
UNRWA kupitia mtandao wa X imesema kitendo cha kushambulia ofis iza UN lazima kikome na badala yake zilindwe wakati wote.
Fri, 01 Nov 2024 - 12022 - ZMBF na harakati zao za kukabili udumavu Zanzibar
Zanzibar Maisha Bora Foundation iliyoko Tanzania Zanzibar, iliyoanzishwa mwaka 2021 tayari inajinasibu na harakati za kusongesha afya ya watoto halikadhalika kupinga udhalilishaji wa kijinsia, masuala ambayo Umoja wa Mataifa kila uchao unasaka wadau wa kuunga mkono ili dunia pawe pahala salama kwa kila mtu na kila mtu aweze kustawi. Ni kwa kutambua hilo, Assumpta Massoi wa Idhaa hii alipopata fursa ya kuzungumza na Muasisi na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Bi. Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mke wa Rais wa Zanzibar, wakati wa ziara yake hapa Umoja wa Mataifa hivi karibuni aliona vema Bi. Mwinyi atufafanulie kwa kina wanachofanya, na alianza na kwa kueleza sababu ya kumulika lishe bora kwa watoto Zanzibar.
Thu, 31 Oct 2024 - 12021 - Jifunze Kiswahili - Ufafanuzi wa neno HEREREZA na Dkt. Mwanahija Ali JumaThu, 31 Oct 2024
- 12020 - 31 OKTOBA 2024
- Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo na mashirika yake lile la mpango wa chakula (WFP) na la chakula na kilimo (FAO), uhaba mkubwa wa chakula unatarajiwa kuongezeka kwa ukubwa na ukali katika nchi na maeneo 22 duniani. Ripoti hiyo inaonya kwamba kuenea kwa migogoro, hasa katika Mashariki ya Kati inasukuma mamilioni ya watu ukingoni.Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, amelaani vikali shambulio la jana usiku lililotekelezwa na Jeshi la Urusi ambapo jengo la makazi la ghorofa nyingi lilipigwa katika mji wa Kharkiv, wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya majiji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amewapigia chepuo vijana akitaka sauti zao na mawazo yao kupewa nafasi kwani kuanzia harakati za chinichini hadi maabara za uvumbuzi, vijana wanasukuma hatua kabambe kukabiliana na tabianchi, wanaunga mkono ujumuishaji wa nishati mbadala, kazi zisizozalisha hewa chafuzi na usafiri safi wa umma, ambayo ni mambo yanayochangia kuunda miji endelevu ambapo kila mtu anaweza kustawi.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEREREZA!
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Thu, 31 Oct 2024 - 12019 - Fahamu kuhusu mtikisiko wa ubongoWed, 30 Oct 2024
- 12018 - UNRWA yamwandikia Rais wa Baraza Kuu la UN baada ya Knesset kupitisha miswadaWed, 30 Oct 2024
- 12017 - 30 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akimulika masuala ya amani na usalama hususan Gaza; afya ya ubongo kwa wanamichezo; biashara ya ndizi kaukau huko India na dansi na kujitambua huko Trinidad na Tobago.
- Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, Philippe Lazzarini amemwandikia barua Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kusaka mshikamano na nchi wanachama baada ya Bunge la Israeli Jumatatu hii kupitisha miswada ya kusitisha shughuli za shirika hilo. Flora Nducha na maelezo zaidi.. Hoja ya ubongo kutikisika (concussion) wakati wa michezo imeibuka katika siku za karibuni na kulazimu Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) kuingilia kati ili kudadavua kwa kina. Akiwa uwanjani akitazama mpira wa Daktari Tarun Dua, Mkuu wa Kitengo cha Afya ya Ubongo WHO, anaeleza kwa muhtasari kuhusu tatizo hilo kupitia taarifa ya Cecily Kariuki.Katika makala, Assumpta Massoi anakupeleka barani Asia, kusikia jinsi wazo la biashara kutoka familia moja lilivyoleta nuru kwa kaya zaidi ya 20.Mashinani tunamulika jinsi dansi kulivyomweka huru mtoto mkimbizi kutoka Venezuela huko nchini Trinidad na Tobago.
Wed, 30 Oct 2024 - 12016 - Mwelekeo ni kutengeneza kaukau za ndizi zenye ladha ya kitunguu na nazi
Uwekezaji rahisi kabisa kwa familia ya Didiki huko nchini India umekuwa na manufaa kwa kaya zaidi ya 20. Zao la ndizi ambalo awali hawakuweza kuongeza thamani ipasavyo lilikuwa na manufaa kidogo kiuchumi. Somo la biashara likamfungua fikra Didiki hadi kupata msaada kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo IFAD kwa ushirikiano na serikali ya India. Msaada umepanua biashara, vijana wamepata ajira, familia zimeongeza kipato na sasa mpango ni kufikia kaya zaidi ya 60,000. Ni kwa vipi? Ungan ana Assumpta Massoi kwenye makala hii.
Wed, 30 Oct 2024 - 12015 - 29 OKTOBA 2024
- Baada ya Bunge la Israel hapo jana Oktoba 28 kupiga kura ya kuizuia Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kufanya shughuli zake katika maeneo yote yaliyoko chini ya Israel, viongozi wa Umoja wa Mataifa kuanzia Katibu Mkuu Antonio Guterres wameendelea kupaza sauti kwamba kuizuia UNRWA ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa na italeta zahma kwa maisha ya watu katika eneo hilo la Mashariki ya Kati. Katibu Mkuu Guterres amesema analileta suala hili kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na atahakikisha Baraza hilo muda wote linakuwa na taarifa kwa kadri hali inavyoendelea.Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ukweli nchini Sudan umesema katika ripoti yake mpya ya kina leo kwamba Vikosi vya wanamgambo wa RSF, ambavyo vimekuwa vikipigana na Jeshi la Sudan (SAF) katika mzozo unaoendelea nchini humo, vinahusika na kufanya ukatili wa kingono kwa kiasi kikubwa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao, ikiwa ni pamoja na ubakaji wa makundi na kuwateka nyara na kuwaweka kizuizini waathiriwa katika hali ambayo ni sawa na utumwa wa ngono.Na leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Usaidizi na Matunzo, makadirio mapya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi (ILO), yaliyotolewa leo yanaonesha takribani wanawake milioni 708 duniani kote wako nje ya nguvu kazi zenye ujira kwa sababu ya majukumu ya kutoa usaidizi au matunzo bila malipo. Utafiti huo umefanywa katika nchi 125.Mashinani leo tutakwenda katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Al Matar huko Kassala, Sudan, kusikiliza ujumbe kutoka kwa Ted Chaiban, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, aliyefanya ziara kambini humo.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Tue, 29 Oct 2024 - 12014 - WFP: Bila msaada wa kibinadamu Wasudan watakufa kwa njaa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.
Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika ukurasa wake wa X leo Oktoba 28 na kufafanua zaidi kwamba mtu mmoja kati ya watu wawili nchini humo anatatizika kupata mlo kila siku.
WFP inaeleza kuwa njaa imethibitishwa Kaskazini mwa Darfur na mahitaji ya kibinadamu ni makubwa sana.
Kabla ya taarifa hii ya leo ya WFP, jana kupitia pia ukurasa wa mtandao wa X, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Cindy McCain ambaye hivi karibuni alikuwa Sudan mojawapo ya maeneo yenye njaa zaidi duniani, ambapo watu milioni 25 wanakabiliwa na njaa kali ameandika kwamba WFP iko Sudan inatoa msaada wa kuokoa maisha lakini wanahitaji kwa haraka mambo matatu ambayo ni kuwafikia watu ili kuwasaidia, misaada kuweza kupita katika kila kivuko na usaidizi zaidi wa kimataifa kwa Wasudani walio katika mazingira hatarishi.
Kwa miaka mingi, Sudan imekuwa ikisumbuka na migogoro. Mgogoro wa hivi karibuni zaidi, ulioanza Aprili mwaka jana 2023, umezua janga baya zaidi duniani la watu kuhama makwao na janga kubwa zaidi la njaa duniani linalosambaa Sudan, Sudan Kusini na Chad.
Mon, 28 Oct 2024 - 12013 - Ushindi wa tuzo ya mtu bora wa mwaka wa UN ni ushindi kwa watu wa Kajiado wanaonufaika na mradi wetu - Kipeto
Kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited wamiliki wa mradi wa nishati ya umeme itokanayo na upepo ya Kipeto Energy iliyoko Kaunti ya Kajiado nchini Kenya wamejitwalia tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa. 2024”
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo anasema ushindi huo ni kwa watu wa Kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambao ni wanaufaika wakubwa wa mradi kwani sio tu umewaletea umeme, bali pia umewainua kiuchumi na kijamii kwa miradi mingine mbalimbali kama inabobainisha makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha..
Mon, 28 Oct 2024 - 12012 - 28 OKTOBA 2024
- Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambapo, katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya Lebanon na Israel, walinda amani walioko katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura wamekuwa wakivumilia mazingira magumu. Ushuhuda wa hivi karibuni kutoka kwa walinda amani hao unaonesha ukubwa wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo vitisho vilivyoongezeka kutoka kwa shughuli za kijeshi za Israel zilizo karibu na eneo hilo, vizuizi vya kusafiri, na changamoto za uendeshaji wa shughuli.Makala inatupeleka Nairobi Kenya kwa washindi waliotwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa 2024” ambao ni kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited wamiliki wa mradi wa nishati ya upepo ya Kipeto Energy iliyoko Kaunti ya Kajiado nchini Kenya.Katika mashinani mashinani leo tutakuwa Haiti ambapo nafasi ni yake Andre Rose, mama wa kijana Kerby, akieleza jinsi msaada wa kifedha unaotolewa na Shirika la UNICEF umekuwa mkombozi kwa familia yake iliyolazimika kukimbia makazi yao kutokana na ghasia za magenge ya uhalifu nchini Haiti.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mon, 28 Oct 2024 - 12011 - Walinda amani wa UNIFIL nchini Lebanon wasimilia kinachowakabili mashambulizi ya Israel yakiendelea
Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambapo, katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya Lebanon na Israel, walinda amani walioko katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura wamekuwa wakivumilia mazingira magumu. Ushuhuda wa hivi karibuni kutoka kwa walinda amani hao unaonesha ukubwa wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo vitisho vilivyoongezeka kutoka kwa shughuli za kijeshi za Israel zilizo karibu na eneo hilo, vizuizi vya kusafiri, na changamoto za uendeshaji wa shughuli.
Kupitia video ya Kikosi hicho cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, tunaona picha ya makao makuu yake huko Naqoura, Lebanon. Hapa tunaona ofisi za walinda amani hao, karibu na ofisi hii kuna mnara wa ulinzi, sehemu yake ikiwa imeharibiwa na mlipuko. Meja Kalpani Fernando anaelekeza kwenye mnara huo akieleza kilichotokea.
“Ghafla, tuliona, na kusikia mlipuko. Kisha tukaona vumbi kubwa likitokea na moshi mweusi. Tulikimbia ndani ya ofisi, na ndani ya sekunde chache, mlipuko wa pili ulitokea. Kisha wanajeshi wawili kati ya kikosi changu walijeruhiwa walipokuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Uangalizi cha 6. Walikuwa nje ya Kituo cha Uangalizi wakati huo, na walijeruhiwa kutokana na mlipuko wakati huo. Kisha nikafunga lango, na tukawapeleka hospitalini ndani ya muda wa dakika mbili hadi tatu.”
Ingawa mzozo huu umesababisha madhara kwa afya ya walinda amani hawa, huku baadhi yao wakipata upasuaji kutokana na majeraha, bado wanaendelea kuwa na dhamira ya kuhudumu katika ujumbe wa kulinda amani. Mmoja wao ni Koplo Wickramage akisema….
‘‘Wakati nilipokuwa kwenye zamu katika Kituo cha Uangalizi cha 6, kulitokea mlipuko na nikajeruhiwa kwenye sehemu ya nyuma ya bega langu. Nilihamishwa haraka kwenye hospitali ya UNIFIL. Nimefanyiwa upasuaji, na ninaendelea na matibabu. Sasa, ninapata nafuu na natumai kuungana na walinda amani wa Sri Lanka hivi karibuni ili kurudi kuhudumu katika UNIFIL.”
Mbali na majukumu yao ya kawaida, wafanyakazi wa afya wa UNIFIL wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii, wakitoa huduma si tu kwa walinda amani waliojeruhiwa bali pia kwa raia walionaswa katikati mwa mapigano hao kama anayoeleza Luteni Kanali Shilpi Mankotia,
“Mbali na huduma za kawaida za matibabu, siku hizi tunatoa msaada na huduma kwa majeruhi na manusura waliolengwa kimakosa, ikiwa ni pamoja na raia na wahudumu wa kibinadamu. Nilikuwa kwenye likizo niliposikia kuhusu mzozo unaoendelea kwa sasa. Nilirudi kazini mara moja kutoka India. Nilifika Beirut usiku wa manane na baada ya kupambana kwa siku saba, hatimaye niliweza kurudi kwenye kituo changu cha kazi.”
Mon, 28 Oct 2024 - 12010 - Ushindi wa mradi di wa Kipeto UN n ushindi wa wananchi wa Kajiado: Mnufaika
Kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited inayoendesha Mradi wa Kipeto Energy jana Siku ya Umoja wa Mataifa ilitwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa.”
Mradi wa Kipeto wa kampuni hiyo unatoa nishani ya umeme kwa kaya 250,000 katika eneo la Esilanke kaunti ya Kajiado nchini Kenya ukizalisha megawati 100 za umeme tangu 2021 ambazo zinaingizwa kwenye gridi ya taifa, lakini pia unasaidia kuwajengea wananchi nyumba bora na kuwapa huduma muhimu ya maji. Stela Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amezungumza na mmoja wa wanaufaika wa mradi huo wa nishati ya upepo ya Kipeto kuhusu faida za mradi huo, na anaanza kwa kujitambulisha..
Fri, 25 Oct 2024 - 12009 - Grandi: Msaada wa haraka unahitajika DRC wakati wakimbizi wanaendelea kufungasha virago
Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kukwepa machafuko nchini mwao, huku rasilimali zikikaribia kikomo. Ameonya Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, akiwa ziarani nchini Uganda hivi karibuni kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wa DRC na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada.
Wakimbizi wanaokimbia mzozo nchini DRC wanashuhudia matukio ya kutisha ya mauaji na ubakaji amesema Grandi, alipotembelea kambi ya ......aliyetembelea kambi za wakimbizi, Uganda na kusimuliwa hadithi za uchungu mkubwa
“Sijawahi kusikia simulizi za machungu na hofu kama hizi za mauaji, ubakaji wa watoto mbele ya mama zao, wanawake wajawazito kukatwa vipande na makundi yenye silaha, na hofu kutawala maeneo yote ya Mashariki mwa Congo.”
Kutokana na hali hii, Grandi anasema amani ndiyo inahitajika zaidi kwa sasa ili kumaliza dhuluma zinazowakumba wakimbizi wa Congo.
“Ni wakati sasa jamii ya kimataifa ijitolee kwa dhati kusaidia Congo kutoka kwenye hali hii. Nilifanya kazi kama afisa wa eneo zaidi ya miaka 30 iliyopita Mashariki mwa Congo, na hali haijabadilika kimsingi.”
Uganda inahifadhi jumla ya wakimbizi...... wengi wakiwa kutoka DRC, Sudan na Sudan Kusini.
Fri, 25 Oct 2024 - 12008 - 25 OKTOBA 2024
- Hali Gaza inaendelea kuwa tete wakati ucheleweshwji wa kuhamisha wagonjwa hususan watoto wanaohitaji msaada wa haraka wa huduma za afya imekuwa ni hukumu ya kifo kwao huku maelfu ya watu wakiendelea kukosa mahitaji ya muhimu ya kila siku ikiwemo chakula kama mkate, yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kukwepa machafuko nchini mwao, huku rasilimali zikikaribia kikomo. Ameonya Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, akiwa ziarani nchini Uganda hivi karibuni kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wa DRC na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada, kama inavyoeleza taarifa ya Bosco Cosmas.Makala inayotupeleka Nairobi Kenya kwake Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi akizungumza na mmoja wa wanaufaika wa mradi wa nishati ya upepo ya Kipeto Energy unaoendeshwa na kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited ambayo jana Siku ya Umoja wa Mataifa ilitwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa” inayotolewa kila mwaka.Mashinani leo tutaelekea Beni, Kivu Kaskazini kusikia jinsi MONUSCO unavyowasaidia wanawake walio katika mazingira magumu, mmoja wao ni Salome Tatsopa ambaye ni mnufaika wa masomo ya ufundi wa cherahani akitueleza matumani yake baada ya mafunzo hayo.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Fri, 25 Oct 2024 - 12007 - UN: Hali si hali tena Gaza vifo vyatawala hospitali na kwa raia hata mkate ni adimu kupatikana
Hali Gaza inaendelea kuwa tete wakati ucheleweshwji wa kuhamisha wagonjwa hususan watoto wanaohitaji msaada wa haraka wa huduma za afya imekuwa ni hukumu ya kifo kwao huku maelfu ya watu wakiendelea kukosa mahitaji ya muhimu ya kila siku ikiwemo chakula kama mkate, yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kwamba idadi ya watoto wanaohamishwa Gaza kwa ajili ya huduma za dharura za matibabu imeshuka sana hadi kufikia mtoto mmoja kwa siku na kusema kiwango hiki kikiendelea itachukua zaidi ya miaka 7 kuhamisha watoto 2500 wanaohitaji huduma ya dharura ya matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa UNICEF James Elder amesema “matokeo yake watoto wanakufa Gaza sio tu kutokana na mabomu na risasi na makombora yanayofurusmishwa lakini kwa sababu hata kama miujiza inatokea , hata kama mabomu yanalipuka na nyumba kuporomoka, na vifo kuongezeka watoto wananusurika, lakini kisha wanazuiliwa kuondoka Gaza Kwenda kupokea huduma za afya zitakazookoa maisha yao.”
Ameongeza kuwa tangu Januari hadi Mei mwaka huu kwa wastan watoto 296 walihamishwa kwa mwezi kwenda kupata matibabu lakini tangu kufungwa kivuko cha Rafah idadi imeshuka hadi watoto 22 kwa mwezi.
Kwa upande wake shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linasema maisha ya kawaida yanazidi kuwa jinamizi kwani kukidhi mahitaji ya msingi kama chakula ni mtihani mkubwa wengi mathalani katika mji wa Deir al-Balah hata mkate ambao ni chakula kikuu kupatikana ni changamoto,
Kila mtu katika Ukanga wa Gaza anakabiliwa na hatari ya baa la njaa kutokana na kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu, ghasia, kuharibiwa kwa mashamba na wahudumu wa kibinadamu kushindwa kuwafikia wenye uhitaji.
Wataalam wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nao wamesema wanahofia hali mbaya ya Wapalestina wenye ulemavu ambao wamekwama Gaza, wakionya kwamba watu hao wenye ulemavu wanakabiliwa na hatari za ulinzi ikiwemo kutoepuka kifo na majeraha wakati wa mashambulizi ya vikosi vya Israel na hili ni janga juu ya janga wamesema.
Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA likimulika Ukingo wa Magharibi limesema “Makumi ya jamii zinakabiliwa na ongezeko la mashambulizi na vikwazo vya kufikia ardhi yao wakati wa mavuno ya mizeituni ya mwaka huu. Kati ya matukio yote yanayohusiana na walowezi, matukio 104 yamesababisha hasara au uharibifu mkubwa wa mali tangu kuanza kwa mwezi huu wa Oktoba ”.
Fri, 25 Oct 2024 - 12006 - 24 OKTOBA 2024
- Uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) uliotolewa leo jijini New York, Marekani katika Siku ya Kimataifa ya Polio, unaonesha kwamba asilimia 85 ya watoto 541 waliokumbwa na polio duniani mwaka wa 2023 wanaishi katika nchi 31 zenye mifumo dhaifu, zinazokabiliwa na mizozo, halikadhalika zilizo hatarini.Umoja wa Mataifa ulijengwa na ulimwengu, kwa ajili ya ulimwengu, ndivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, alivyouanza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku ya leo ya Umoja wa Mataifa.Na leo Oktoba 24 huko Kazan nchini Urusi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amehutubia mkutano wa viongozi wa kundi la BRICS yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini akisisititiza amani duniani akizitaja Gaza, Lebanon, Ukraine na Sudan, akiwaambia wajumbe wa BRICS, “tunahitaji amani nchini Sudan, huku pande zote zikinyamazisha bunduki zao na kujitolea katika njia ya kuelekea amani endelevuKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEKEMUA!
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Thu, 24 Oct 2024 - 12005 - Jifunze Kiswahili - maana ya neno HEKEMUA!Thu, 24 Oct 2024
- 12004 - 23 OKTOBA 2024
- Mashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWAMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali.Ndoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto katika makazi ya wakimbizi katika wilaya Kyegegwa magharibi mwa Uganda. Hata hivyo, kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF na ufadhili kutoka wahisani wa Uingereza UKaid, maelfu ya wazazi katika makazi ya wakimbizi na jamii zinazohifadhi waakimbizi katika wilaya ya Kyegegwa wamepewa mafunzo juu ya malezi bora ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto, wanawake, na wasichana.Mashinani tunabisha hodi Lebanon, kumsikia Farah, Mkimbizi wa ndani anayepokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, baada ya kujifungua kwenye hema, akieleza alichokabiliana nacho.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Wed, 23 Oct 2024 - 12003 - Mbinu bora za malezi zimebadilisha maisha katika Wilaya ya Kyegegwa - UNICEF Uganda
Ndoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto katika makazi ya wakimbizi katika wilaya Kyegegwa magharibi mwa Uganda. Hata hivyo, kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF na ufadhili kutoka wahisani wa Uingereza UKaid, maelfu ya wazazi katika makazi ya wakimbizi na jamii zinazohifadhi waakimbizi katika wilaya ya Kyegegwa wamepewa mafunzo juu ya malezi bora ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto, wanawake, na wasichana.
Leo tuko katika wilaya ya Kyegegwa nchini Uganda ambapo, kwa msaada wa UNICEF, wafanyakazi wa kijamii, kamati za ulinzi na ustawi wa watoto, na kikosi cha polisi; wote wamepewa mafunzo mwafaka ili kuhakikisha ulinzi wa watoto unaofaa na wa kudumu, na tunakutana na Agnes Karungi mama mwenye umri wa miaka ishirini na mmoja wa wanufaika wa mradi wa malezi bora. Mbali na kukumbana na changamoto za kuwa mama kijana, mwanaye Agnes, ni mwenye ulemavu na zaidi ya hayo akatengwa na familia yake kwa kuzaa akiwa angali mwanafunzi.
Cecily Kariuki anaeleza zaidi katika makala hii..
Wed, 23 Oct 2024 - 12002 - UN: Mashambulizi ya anga ya Israel yalazimisha kampeni ya chanjo kusitishwa Gaza Kaskazini
Mashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA.
Asante Anold, kampeni hiyo iliyoahirishwa ilitakiwa kuanza leo n ani duru ya mwisho ya chango ya kampeni iliyolenga kuwachanja watoto 119,279 kote Gaza Kaskazini kwa dozi ya pili ya chanjo ya polio aina ya nOPV2, lakini hali ya sasa imefanya iwe vigumu kwa familia kupeleka watoto wao kwenye vituo vya chanjo, na kwa wahudumu wa afya kuendesha huduma kwa usalama.
Mashambulizi ya makombora yanayoendelea dhidi ya miundombinu ya kiraia yamepunguza maeneo yanayokubaliwa kwa usitishaji wa uhasama kwa mnajili ya masuala ya kibinadamu kuwa kwenye Jiji la Gaza pekee, ikilinganishwa na wakati wa awamu ya kwanza ya chanjo iliyofanyika tarehe 1-12 Septemba 2024.
Hali hii inahatarisha kufikiwa kwa lengo la angalau asilimia 90 ya watoto kuchanjwa, jambo ambalo ni muhimu ili kukomesha usambaaji wa virusi vya polio na kulinda afya za watoto.
WHO na UNICEF wamesema kuwa kucheleweshwa kwa chanjo ya polio kunaweza kuongeza hatari ya virusi kuenea zaidi Gaza na maeneo Jirani na kuchelewesha utoaji wa dozi ya pili ya chanjo ndani ya wiki sita kunapunguza uwezo wa chanjo hiyo kuimarisha kinga za watoto na kuzuia maambukizi.
Tangu duru ya pili ilipoanza tarehe 14 Oktoba 2024, jumla ya watoto 442,855 wenye umri wa chini ya miaka kumi wamefanikiwa kuchanjwa katika maeneo ya kati na kusini mwa Gaza.
UNICEF na WHO wanatoa wito kwa pande zote zinazohusika katika mzozo kutekeleza usitishaji mapigano wa kibinadamu na kuhakikisha kuwa raia, wahudumu wa afya, na miundombinu ya kiraia kama shule na hospitali inakingwa dhidi ya mashambulizi.
Mashirika hayo yamesisitiza umuhimu wa kuanza tena kampeni ya chanjo mara moja ili kuzuia kupooza kwa watoto na kuimarisha kinga dhidi ya polio.
Katika juhudi za kuhakikisha huduma bora, takribani watoto 357,802 pia walipatiwa virutubisho vya vitamini A kama sehemu ya juhudi za kuunganisha chanjo ya polio na huduma zingine muhimu za afya.
Mashirika ya WHO na UNICEF ymesisitiza kuwa kusitisha vita na kuwezesha chanjo ni hatua muhimu ili kuzuia mlipuko wa polio kuendelea na kulinda afya ya watoto wote Gaza.
Wed, 23 Oct 2024 - 12001 - Dkt. Tedros: Heshima kwa wahudumu wa afya wa Rwanda wanavyopambana na Marburg
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali.
"Ninawapongeza wahudumu wa afya waliojitolea ambao wamejiweka hatarini kuokoa wenzao, na ambao wameendelea kufanya kazi licha ya hatari. Na ninaenzi wale ambao tumewapoteza."
Pia Dkt. Tedros akaeleza kuwa yeye na wenzake wamefurahishwa na namna ya utoaji huduma ambayo haijawahi kutumiwa katika mlipuko ya magonjwa ya namna hii barani Afrika akitolea mfano wagonjwa wawili aliowashuhudia wakiendelea vizuri kwamba waliokolewa kwa kuwekewa mipira iliyopeleka hewa ndani ya mwili.
“Tunaamini hii ni mara ya kwanza kwa wagonjwa wenye virusi vya Marburg barani Afrika kuingiziwa na kutolewa mpira wa hewa. Wagonjwa hawa wangefariki dunia katika milipuko ya hapo awali. Hii inaonesha kazi ambayo Rwanda imefanya kwa miaka mingi kuimarisha mfumo wake wa afya, kukuza uwezo wa huduma muhimu na msaada wa kuokoa maisha ambao unaweza kutumiwa katika huduma za kawaida za hospitali na katika dharura.”
Wed, 23 Oct 2024 - 12000 - Kuanza tena kwa shughuli za Redio RTNC kutawawezesha kupigana dhidi ya taarifa potofu na za uongo - MONUSCO
Umoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika kukabili habari potofu na za uongo hususan huko mashariki mwa nchi ambako vikundi vilivyojihami vinaendelea kushambulia raia na kupambana na jeshi la serikali. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, umeipatia kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini jengo na vifaa vyenye thamani ya takriban dola elfu hamsini za Kimarekani. Hatua hiyo iliwezesha RTNC kuanza tena matangazo yake. Mwandishi wetu wa DRC, George Musubao alifika kituoni hapo kuzungumza na wahusika na wanufaika.
Tue, 22 Oct 2024 - 11999 - 22 OKTOBA 2024
- Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Cairo, Misri, imebainisha kwamba athari za vita zimerudisha nyuma maendeleo huko Gaza kwa takriban miaka 69. Ripoti hiyo iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi na Kijamii kwa Asia Magharibi imeonya kwamba bila kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo, uchumi wa Palestina unaweza kushindwa kurejesha viwango vya kabla ya vita na kusonga mbele kwa kutegemea misaada ya kibinadamu pekee.Kiongozi wa timu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Dkt. Janet Diaz ameeleza kwamba uongozi thabiti wa serikali ya Rwanda umewezesha kufanya uamuzi wa haraka na kuchukua hatua kuanzisha mwitikio wa sekta mbalimbali dhidi ya mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo wa Marburg nchini humo.Na uongozi wa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) umeendelea kusisitiza kwamba pamoja na changamoto zilizopo, walinda amani wa UNIFIL wanaendelea kufanya kazi kwa karibu na jamii za kusini mwa Lebanon ili kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji. Hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi dhidi ya walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa yanayotekelezwa na majeshi ya Israeli.Mashinani kupitia video ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura OCHA tunamuangazia mmoja wa watu waliokimbia makazi yao akiwa katika shule ya Al Rimal, akielezea changamoto wanazokutana nazo katika kukabiliana na hali ngumu inayowakabili raia wa Gaza.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Tue, 22 Oct 2024 - 11998 - Nadipo: Asante WFP kwa mradi wa mizinga ya nyuki sasa familia yangu inatabasamu
Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.
Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa kwenye ukame uliotamalaki? Lakini cha kustaajabisha ni kwamba kwa kuwezeshwa mengi yanawezekana ikiwemo njia bora za kuhakikisha uhakika wa chakula na hata kubadili maisha ya watu kama anavyosema mkulima wa nyuki Nadipo Lotelei mnufaika wa mradi wa mizinga ya nyuki kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. “Hatua iliyochukuliwa na WFP kutupatia mizinga ya nyuki imekuja kama nyota ya jaha kwangu kwa sababu siwezi kutembea umbali mrefu kutokana na ajali niliyopata. Mradi huu umenisaidia sana mimi ili kuweza kusaidia watoto wangu na mke wangu. Mke wangu ameweza kuanzisha biashara ya duka kutokana na faida niliyopata ambayo sasa inatumika kama chnzo cha kipato cha mahitaji ya kaya yetu.”Nadipo ni miongoni mwa wafuga nyuki 1,900 katika kaunti ya Turkana ambao wamepewa mafunzo ya ufugaji nyuki na vifaa kupitia mradi wa WFP kwa ushirikiano na shirika binafsi la HIVE ambalo mwenyekiti mtendaji wake ni Christopher Nzuki. “Tunahusika katika ufungaji na usambazaji wa vifaa. Na wakati huohuo tunatoa mafunzo kwa wafugaji nyuki na kisha kuwapatia masoko. Tunachukua kila kitu wanachozalisha.”Ufugaji wa nyuki wa kisasa si kazi kubwa, na pia unatumia nafasi ndogo na maji kidogo. Nyuki huchavusha asilimia 80 ya miti ya maua ikiwemo mazao ya chakula. Huzalisha asali, nta, mafuta na sumu, bidhaa ambazo huuzwa kwa gharama kubwa sokoni. Kwa sasa WFP inasaidia karibu wafugaji wa nyuki 5,000 katika kaunti 9 nchini Kenya lakini lengo ni kuwafikia wengi zaidi na mradi huu kama anavyosema afisa wa WFP Timothy Koskei. “Dhamira yetu mwisho wa yote ni kuwafikia wastani wa wafuga nyuki 10,000 katika kaunti 9 na kuvuna takriban tani 600 za asali.” Kwa mujibu wa WFP nyuki wana uwezo mkubwa na wanaweza kutoa mavuno mengi ambayo ni neema kwa familia sisizojiweza katika maeneo haya kame. Mkurugenzi wa WFP nchini Kenya Lauren Landis anasema mradi umezaa matunda. “Hivi sasa tunasikia kutoka miongoni mwa wanaufaika ambao awali walikuwa wakipokea msaada wa chakula ,ambao sasa sio tu wanazalisha asali kwa ajili ya faida bali pia wanafikiria kuongeza ununuzi wa pembejeo zaidi kutoka kwa Hive. Hivyo tunachokishuhudia ni mchakato ulio wazi ambapo mtu anatoka kuwa mpokea msaada na kuwa mteja, kuwa mpokeaji wa faida na si mpokeaji wa msaada wa chakula.”Kwa mafanikio haya WFP inasema itaendelea kupanua wigo wa mradi huu ili kunufaisha familia nyingi zaidi.Mon, 21 Oct 2024 - 11997 - Mlo shuleni ulibadilisha maisha yangu- Mkurugenzi wa WFP Somalia
Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.
"Mimi ni zao la mlo wa shule," hayo ni maneno ya El-Khidir Daloum ambaye ana shukrani tele kwa WFP kwa kuendesha programu ya ‘mlo shuleni’ iliyomfaidisha alipokuwa mwanafunzi. Hivi sasa, akiwa Mkurugenzi wa WFP nchini Somalia, Daloum ameweka dhamira ya kazi yake kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa wote. Je Daloum aliifahamu vipi programu ya mlo shuleni ya WFP kwa mara ya kwanza?
“Tulipofika pale, tukakuta ni shule ya bweni, wakati huo wazazi wetu hawangeweza kugharamia shule hiyo. Kwa hivyo, shule ilifanya ushirikiano kati ya serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula Duniani (WFP). Na hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuonja dagaa wa Kijapani, maziwa ya unga kutoka Uholanzi, na jibini ya Denmark, yote yaliletwa kwetu kupitia mlo wa shule.”
Je Daloum anadhani maisha yake yangekuwa vipi kama WFP isingetoa mlo shuleni?
“Nikiwaza kuhusu kizazi changu, hasa wale waliokuwa katika shule za bweni, bila ushirikiano huo kati ya serikali ya nchi yangu na WFP, hatungeweza kumaliza elimu yetu. Ndio maana nakwambia kwamba mimi ni zao la mlo shuleni kutoka kwenye shule ya msingi kwenda katika shule ya kati na hatimaye sekondari, yote haya matatu yalifaulu kutokana na mlo shuleni.”
Mon, 21 Oct 2024 - 11996 - 21 OKTOBA 2024
- Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili.Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.Makala inatupeleka Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame ambako mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Waffiyah Diyah kutoka Lebanon ambaye ni muathirika wa vita vilivyolazimisha maelfu ya watu kufangasha viragoanaelezea hali ya familia yake baada ya kukimbia mashambulizi na kupoteza kila kitu, lakini sasa anapokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mon, 21 Oct 2024 - 11995 - COP16: Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baionuai waanza nchini Colombia
Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili.
COP16 kwa siku 12, viongozi na wadau kutoka kote duniani wanatarajiwa kujadili namna ya wanadamu kuishi kwa amani na asili ya ulimwengu, kama wasemavyo nchi mwenyeji Colombia kwa lugha ya kihispanyola Paz con la Naturaleza yaani amani na asili.
Washiriki, kwa kina watajadili utekelezaji wa mkakati wa Kimataifa wa Kunming-Montreal kuhusu bayoanuai, makubaliano ya kihistoria ya mwaka 2022 ya kusitisha na kubadili upotevu wa asili. Pia watachunguza jinsi ya kuelekeza mabilioni ya dola kwa nchi zinazoendelea ili kuhifadhi na kudhibiti bioanuai kwa uendelevu. Na watajadili sheria za msingi ambazo zinaweza kuhitaji kampuni za kibinafsi kufidia mataifa.
Katika sherehe za ufunguzi wa mkutano huu hapo jana, kwa njia ya video, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye pia anategemewa kuhudhuria siku za mwishomwisho za mkutano huu, amewaeleza wajumbe akisema, “mkakati wa Kimataifa wa Bioanuwai unaahidi kurekebisha uhusiano na dunia na mifumo yake ya ikolojia. Lakini hatuko kwenye mstari. Jukumu lenu katika COP hii ni kubadilisha maneno kuwa vitendo.”
Mon, 21 Oct 2024 - 11994 - Nchi zote pamoja na mashirika ya kimataifa ikiwemo UN yanawajibika kukomesha ukaliwaji wa Palestina
Tume hiyo huru imeyasema hayo katika taarifa mpya ya msimamo wa kisheriia iliyotolewa mjini Geneva Uswis kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina ikiwemo Jerusalem Mashariki ambayo imeweka wazi maoni ya tume kuhusiana na wajibu wa serikali na jinsi Baraza Kuu na Baraza la Usalama linavyoweza kutambua na kutekeleza mbinu na hatua sahihi zinazohitajika kwa kazi hiyo hadi mwisho wa ukaliwaji huo, na kwa haraka iwezekanavyo.
Tume ihiyo imebaini kwamba maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu matokeo ya Kisheria yanayotokana na sera na desturi za Israel katika eneo linalokaliwa la Palestina ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki ni wenye mamlaka na usio na utata kwa kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na sheria ya kimataifa.
Taarifa hiyo ikitolewa Geneva Gaza kwenyenyewe hali inaendelea kuwa tete, kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestinna UNRWA Phillipe Lazzarini, kwani shule nyingine ya UNRWA imeshambuliwa leo Jabalia Kaskazini mwa Gaza, watu kadhaa wameripotiwa kuuawa na miongoni mwao Watoto wengi waliokuwa wakipata hifadhi katika jengo hilo.
Lazzarini amesema hili ni shambulio la tatu dhidi ya majengo ya UNRWA kwa wiki moja. Na pia wafanyakazi wa shirika hilo wanaendelea kuuawa sasa wameffikia 231 tangu kuanza kwa vita hii Oktoba mwaka jana.
Naye msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF James Elder akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo amesema “Gaza ni mfano halisi wa ulimwengu wa kuzimu duniani kwa watoto milioni moja wa eneo hilo. Na hali inazidi kuwa mbaya, siku baada ya siku, tunapoona athari za kutisha za mashambulizi ya anga ya kila siku na operesheni za kijeshi za Israek kwa watoto wa Kipalestina.”
Nalo shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA likiangazia Ukingo wa Magharibi limesema “Vikosi vya Israel vimekuwa vikitumia mbinu mbaya za vita katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kuibua wasiwasi mkubwa juu ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na kuongeza mahitaji ya kibinadamu ya watu.” Ameelezea wasiwasi kuhusu mashambulizi ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina na miti yao ya mizeituni wakati huu wa mavuno ya kila mwaka.
Fri, 18 Oct 2024 - 11993 - Mbegu za asili zinanisaidia kukabili mabadiliko ya tabianchi - Mkulima
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linapigia chepuo uwepo wa mifumo ya uzalishaji chakula inayoendana na kila eneo husika, mathalani kilimo kitumie mbegu za asili za eneo husika kama mbinu ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Kupata aina tofauti tofauti za mbegu za asili kwa eneo husika kunainua kipato cha wakazi wa vijijini na kuongeza mnepo majanga yanapotokea. Na hicho ndio anafanya mkulima kutoka Tanzania ambaye wakati wa maonesho ya siku ya chakula duniani huko mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania alieleza kwa nini ameamua kuchukua hatua hiyo. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.
Fri, 18 Oct 2024 - 11992 - UN Ripoti: Uwezekano wa kifo cha Dag Hammarskjöld kuwa ni hila unaongezeka kutokana na taarifa mpya
Ripoti nyingine mpya ya tathimini ya uchunguzi wa hali na mazingira ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1961 Dag Hammarskjöld imetolewa leo ikiwa na vipengele vinne vipya vikiongeza uwezekano kwamba kifo hicho cha ajali ya ndege kilikuwa ni hila.
Asante Anold kwanza ikumbukwe kuwa hii sio ripoti ya kwanza na huenda isiwe ya mwisho ya kutathimini hali na mazingira yliyochangia ajali ya ndege iliyokatili maisha ya Dag Hammarskjöld tarehe 17 Septemba 1961 akiwa njia kuelekea Congo ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cngo DRC, kujadili usitishwaji wa uhasama ila ni ripoti ya karibuni zaidi
Ripoti inasema mwenyekiti wa jopo la tathimini ya uchunguzi jaji mkuu wa zamani wa Tanzania Mohamed Chande Othman amepokea taarifa mpya muhimu kutoka kwa nchi wanachama ambazo zinajumuisha maeneo haya Mosi: uingiliaji unaowezekana wa Nchi Wanachama wa mawasiliano husika.
Pili: Uwezo wa wanajeshi wa Katanga, au wengine, wa kufanya shambulio linalowezekana kwenye ndege ya SE-BDY,
Tatu: kuwepo kwa askari wa kigeni na wafanyakazi wa kijasusi katika eneo hilo la tukio
Na nne: Taarifa zaidi mpya zinazohusiana na muktadha na matukio yanayozunguka kifo hicho mwaka 1961.
Jaji Othman amemkabidi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ripoti hii ya tathimini ambaye naye ameiwasilisha kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Na kufuatiia tathimini hii Guterres amesema anaizingatia ingawa kihistoria kumekuwa na nadharia nyingi zilizotolewa kama sababu inayowezekana ya ajali hiyo, na anazichukulia nadharia hizo nyingi kuwa zisizo na uthibitisho.
Hata hivyo mwenyekiti wa jopo la tathimini anasema nadharia nyingine ambayo inabaki na inakubalika ni kwamba shambulio la nje au tishio lilikuwa sababu ya ajali.
Pia amesema kuwa dhana mbadala zinazoonekana kuwepo ni kwamba ajali hiyo ilitokana na hujuma, au makosa ya kibinadamu yasiyokusudiwa.
Katibu mkuu amekaribisha ushirikiano uliotolewa na baadhi ya nchi wanachama katika tathimini hiyo lakini bado jopo la tathimini linaaminikuna baadhi ya nchi wanachama wana taarifa muhimu ambazo hawajataka kuzitoa.
Fri, 18 Oct 2024 - 11991 - 18 OKTOBA 2024
- Tume Huru ya Kimataifa ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina leo imesema mataifa yote na mashirika ya kimataifa, ikiwa ni amoja na Umoja wa Mataifa, wana wajibu chini ya sheria za kimataifa wa kukomesha uwepo haramu wa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, wakati mashambulizi Gaza yakishika kazi na kuongeza madhila kwa raia.Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo.Makala inatupeleka Tanzania hususan mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki ambako Assumpta Massoi amezungumza na mhifadhi wa mbegu za asili, mahojiano yaliyofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini humo. Mhifadhi mbegu anaanza kwa kujitambulisha.Na mashinani fursa ni yake Nosizi Reuben Dube ambaye kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), amefanikiwa kupata shahada ya chuo kikuu, akiwakilisha tumaini kwa jamii yake, ambayo imeishi Kenya kwa zaidi ya 50 bila uraia hadi walipotambuliwa hivi karibuni na serikali ya Kenya na kuwapatia vyeti vya uraia
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Fri, 18 Oct 2024 - 11990 - Mohamed hajakata tamaa ya kuwa mwanasoka maarufu - Gaza
Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo.
Jua linazama hapa kwenye ufukwe wa Al Mawasi, kwenye bahari ya Mediteranea, wengine wakiwa wanaogelea, na kwa mbali mahema ya waliosaka hifadhi baada ya kufurushwa kaskazini mwa Gaza, mmoja anaonesha mbwembwe za dana dana ya mpira, anajitambulisha.
"Naitwa Mohamed Abu Jalda, mchezaji wa Klabu ya Rafah Services katika daraja la kwanza. Nilikuwa na ari kubwa ya kuwa mchezaji mkubwa wa soka kama wengine walioko nje ya Ukanda wa Gaza, lakini kutokana na vita, tamaa yangu na maisha yangu yalicheleweshwa, sasa nina zaidi ya miaka 20, nikijaribu kuwa mchezaji wa soka, lakini siwezi kwa sababu naishi Gaza ambapo kuna mapigano ya mara kwa mara. Kila siku nahisi kama ninakufa; Mungu atujalie uvumilivu kuhimili maisha haya."
Mohamed amekuwa akiwa na ndoto ya kucheza soka ya kulipwa tangu akiwa na umri wa miaka 10 na sasa ana umri wa miaka 20 anaona ndoto inayoyoma, lakini ana matumaini..
"Wakati wowote nikipata muda na kutamani kucheza soka,ninakuja ufukweni, kwani ni sehemu pekee naweza kucheza kama mchezaji mwingine. Natumai Mungu atanijalia kufanikiwa kuwa mchezaji wa soka, na najivunia kuwa mpalestina kutoka Gaza. Natamani kucheza soka nje ya Gaza na timu ya taifa ya Palestina, kwa sababu ni haki yangu."
Fri, 18 Oct 2024 - 11989 - Tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa kwa kuchanganya herufi ‘R’ na ‘L’
Katika kujifunza lugha ya kiswahili, matamshi sahihi ya lugha husaidia kufikisha ujumbe sahihi. Kinyume cha hivyo ujumbe utakuwa sivyo ndivyo na ndio maana hii leo, mbobezi wa lugha ya Kiswahili, Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa na mzungumzaji anayechanganya herufi ‘R’ na ‘L’
Thu, 17 Oct 2024
Podcasts ähnlich wie Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
- Global News Podcast BBC World Service
- Kriminálka Český rozhlas
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Espacio en blanco Radio Nacional
- Les Grosses Têtes RTL
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR