Podcasts by Category

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12050 - Jifunze Kiswahili - Ufafanuzi wa maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”
0:00 / 0:00
1x
  • 12050 - Jifunze Kiswahili - Ufafanuzi wa maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE” 

    Thu, 14 Nov 2024
  • 12049 - 14 NOVEMBA 2024

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku kwa mkutan wa COP29, amabyo washiriki wanasaka mbinu za kujumuisha makundi yote katika harakati za kukabili na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na ongezeko la hewa chafuzi. Idhaa ya Kiswahili imezungumza na Naomi mmjoja wao kutoka Tanzania. Pata pia muhtasari wa habari na ujifunze Kiswahili.

      Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa kisukari, shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limesema idadi ya watu wazima wanaoishi na Kkisukari duniani ni zaidi ya milioni 8000 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 4 tangu mwaka 1990.Baku Azerbaijan ambako mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 leo umejikita na na lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres ameainisha jukumu muhimu ambalo miji, mikoa, biashara na taasisi za kifedha lazima zitekeleze katika kuendesha juhudi za dunia nzima kufikia lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa katikati ya karne hii.Nchini Sudan shirika la Umojja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharida OCHA limesema ghasia za kutumia silaha na mashambulizi katika Jimbo la Aj Jazirah zinadhihirisha ukatili wa karibu miezi 19 ya vita nchini Sudan,huku kukiwa na ripoti za ubakaji, mauaji ya halaiki na uporaji mkubwa. Katika chini ya wiki mbili, OCHA inasema uhasama huko Aj Jazirah umefurusha zaidi ya watu 135,000 kutoka makwao, wengi wao walikimbilia majimbo jirani ya Gedaref na Kassala.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”

    Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

    Thu, 14 Nov 2024
  • 12048 - Wananchi tufahamishwe kwa kina majukumu ya MONUSCO ili kukabili habari potofu DRC

    Umoja wa Mataifa unatambua ni kwa kiasi gani habari potofu na habari za uongo kuwa ni mojawapo ya vikwazo vikuu vinavyokabili operesheni zake za  kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.  Hii imesababisha Umoja huo kuhaha kila wakati kuona ni kwa vipi itakabiliana na habari hizo, iwe ni kupitia mafunzo kwa wanahabari, au kusaidia ujenzi wa vyombo vya habari, na hata kuzungumza na wananchi. Hivi karibuni Umoja Wa Mataifa kupitia Idara yake ya Ulinzi wa Amani, kitengo cha uadilifu wa habari, ulituma Tume yake Mashariki mwa DRC kukutana na wakazi ili  kujua ni nini Umoja wa Mataifa unapaswa kufanya ili kupambana na habari potofu na za uongo nchini humo. Mwandishi wetu wa Mashariki mwa DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini, George Musubao alishuhudia ziara hiyo na ametuletea makala hii.

    Wed, 13 Nov 2024
  • 12047 - Patricia Kombo COP29: Ufadhili wa fedha utakuwa jawabu mujarabu kudhibiti mabadiliko ya tabianchi Afrika

    Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 leo ukiingia siku ya nne  mjini Baku Azerbaijan vijana kutoka Afrika wataka ufadhili uongezwe kutoka mataifa makubwa hususan yanayochangia zaidi hewa ukaa ili kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mataifa yanayoendelea ambapomiongoni mwa waathirika wakubwa ni vijana.  

    Asante Bosco na mmoja wa washiriki hao ni Patricial Kombo Mumbua kutoka Kenya  akiwasilisha matakwa ya vijana katika mkutano huo, na akizungumza na UN News  kuhusu ujumbe wake kwa COP29 amesema

    “Kwangu kama kiongozi wa vijana jambo la kwanza ni kuweza kupata zile fedha au kuzikusanya ili ziweze kusaidia mataifa ambayo yanapambana na kukabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi . Pili ni kuhakikisha kuwa viongozi kutoka mataifa ambayo yanazalisha zaidi hewa ukaa yanawajibika ili kuyafanya matifa ambayo yanaendelea kuweza kujilinda , kunufaika , kujiinua dhidi ya janga hilo na pia kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika jamii zao.”

    Na nini anachokitarajia katika mkutano huo wa COP29?

    “Ni kuweza kuona kuwa hili kongamano litaweza kuhamasisha upatikanaji wa hizo hela kwa mataifa ambayo yanakabiliwa na hizi changamoto za mabadiliko ya tabianchi, Na pia wakati ambapo mataifa yanaendelea kurekebisha michango yao ya kitaifa ya mabadiliko ya tabianchi au NDCs, waweze kuleta michango ambayo inaaambatana na zile changamoto ambazo mataifa yao yanazidi kuathiirika nazo za mabadiliko ya tabianchi.”

    Mbali ya masuala ya ufadhil mada zingine zinazotamalaki kwenye mijadala ya leo COP29 ni masuala ya nishani safi , mifumo ya tahadhari za mapemba na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa matifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea.

    Wed, 13 Nov 2024
  • 12046 - 13 NOVEMBA 2024

    Hii leo jaridani tunaangazi ufadhili kwa wakulima huku mkutano wa COP29 ukiendelea Baku, na madhara ya mafuriko kwa wakulima nchini Sudana Kusini tukimulika jinsi Umoja wa Mataifa wanavyohaha kuwasaidia. Makala inatupeleka nchini DRC na mashinani tunasalia huko huko Sudan Kusini, kulikoni?

      Kuongeza kiwango cha fedha kwenye ufadhili wa miradi ya kukabili na kuhimili tabianchi nchi ikiwa ni moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan, leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bila kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi, na kuimarisha miradi ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kila uchumi duniani utakumbwa na madhara makubwa.Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuriko ya msimu yanayokumba eneo hilo mara kwa mara, eneo ambalo ardhi yake ina rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara.Katika Makala George Musubao, mwandishi wetu huko Jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akimulika mkutano ulioandaliwa na watendaji wa Umoja wa Mataifa ya eneo hilo kuangalia jinsi ya kukabiliana na  habari potofu na za uongo.Na mashinani tutakuwa Sudan Kusini, ambako shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linasaidia jamii zilizoathiriwa na mafuriko kupata suluhisho la kudumu.

    Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu! 

    Wed, 13 Nov 2024
Show More Episodes