Filtra per genere
- 293 - DRC : Haki ya mtoto kupata elimu na vizingiti vinavyochangiaTue, 12 Nov 2024
- 292 - DRC : Haki ya wanawake kupata elimu
Nchini DRC, kumeripotiwa upungufu wa watoto wa kike katika kupata elimu, hili likidaiwa kuchangiwa na tamaduni zilizopitwa na wakati.
Katika makala haya basi Butua Balingane, mkurugezi wa chuo kikuu cha walimu cha ISP, Goma ambaye anasimulia masaibu anayopitia mtoto wa kike nchini DRC kupata elimu.
Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
Tue, 05 Nov 2024 - 291 - Kenya : Wanawake 97 wauawa kwa kipindi cha miezi tatu
Nchini Kenya, idara ya polisi imekiri kwamba wanawake 97 wameuawa kwa kipindi cha miezi 3, baadhi miili yao ikipatikana imenyofolewa.
Ni visa ambayo vimesababisa viongozi wa ngazi ya juu akiwemo rais William Ruto, ambaye ametoa agizo wa asasi za uchunguzi nchini humo kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika visa hivyo.
Kwenya makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Kenya, ambapo mtaalamu wa maswala ya jamii bi Carolina Situma anaeleza nini kimechangia mauwaji haya.
Tue, 05 Nov 2024 - 290 - Kenya : Visa vya raia kutekwa yaongezeka
Nchini Kenya, visa vya raia kutekwa na kisha baadaye kuachiliwa au kupatikana wameuawa vinazidi kuongezeka, visa kadhaa vikiendelea kugonga vichwa vya habari.
Katika Makala haya George Ajowi angaazia visa hivi na jinsi mkuu wa polisi nchini Kenya alikosa kufika mahakamani kueleza walipokuwa baadhi ya wakenya waliotekwa.
Fri, 25 Oct 2024 - 289 - Hatua zilizopigwa katika kumuinua mtoto wa kikeThu, 24 Oct 2024
- 288 - Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani
Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba, ni fursa ya kuangazia changamoto zinazokabili watoto wa kike duniani na kukuza usawa wa kijinsia.
Katika mwaka 2024, mada ilikuwa "Kutoa sauti kwa watoto wa kike: Fursa na Changamoto katika Utu wa Kike."
Makala haya yataangazia kwa kina haki za mtoto wa kike na hatua zilizopigwa katika kusababisha mtoto wa kike kuskizwa na hata hatua zilizochukuliwa ili kuboresha elimu, afya, na usalama wa watoto wa kike, pamoja na jinsi jamii zinaweza kushiriki katika kuwasaidia kufikia ndoto zao.
Aidha, itajadili umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wazazi katika kufanikisha malengo haya.
Fri, 18 Oct 2024 - 287 - MAMILLIONI YA WATU HASA WATOTO BARANI AFRIKA HAWAJAPATA HAKI ZA CHAKULA
Chakula ni muhimu kwa maisha, kuishi, heshima, ustawi, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa watu binafsi, jamii, na mataifa. Sheria za kimataifa zinatambua haki ya kila mtu kupata chakula cha kutosha na haki ya kuwa huru kutokana na njaa. Haki hii ni ya msingi kwa utekelezaji wa haki zote za binadamu.
Nchini Kenya, ni haki ya kikatiba, iliyoko katika Kifungu cha 43(1)(C) kinachosema: "Kila mtu ana haki ya kuwa huru kutokana na njaa na kuwa na chakula bora na cha kutosha .Lakini je, sheria hii inatambuliwa ? Je, watu wanaelewa haki yao ya chakula? Na hali ya usalama wa chakula nchini Kenya iko vipi leo?
Katika kipindi cha leo ,cha jua haki zako , tunaangazia iwapo watu wanapata haki zao za kupata chakula na jinsi changamoto za kiuchumi na kimazingira zinavyoathiri upatikanaji wa chakula nchini Kenya
Wed, 16 Oct 2024 - 286 - DRC : Wanawake wabakwa katika gereza la Makala nchini
Katika makala haya tunaangazia ripoti ya umoja wa mataifa kusema kwamba zaidi ya wanawake wafungwa ya 260 walibakwa katika jela ya Makala nchini DRC, mapema mwezi huu wakati wa jaribio la wafungwa kutoroka jela.
Ripoti hiyo imebaini kwamba kati ya wafungwa 348 katika gereza hilo la Makala, wafungwa 268, walitendewa vitendo vya unyanyasaji wa kingono ikiwemo ubakaji, wanawake 17 kati ya waliobakwa wakiwa chini ya umri wa miaka 19.
Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa wanawake hao walilazimika kutafuta mbinu za kuzuia magonjwa baada ya kutendewa vitendo hivyo vya kikatili.
Awali serikali ya DRC ilikuwa imekiri kubakwa kwa wanawake hao ila haikotoa idadi ya wanawake waliobakwa.
Kadhalika ripoti hiyo pia imesema wafungwa 129 waliojaribu kutoroka jela waliuawa kwa kupingwa risasi, katika gereza hilo la Makala ambao linastahili kutoa huduma kwa wafungwa 1500, ila lina zaidi ya wafungwa alfu 15.
Rais Felix Tshisekedi aliagiza kufanyika kwa uchuguzi kuhusiana na jaribio hilo la wafungwa kutoka, na mikakati ya kupunguza idadi ya wafungwa katika gereza hilo la jiji Kinshasa.
Thu, 19 Sep 2024 - 285 - Kenya : Watoto wateketea shuleni, je jukumu la nani kumlinda mtoto akiwa shuleni
Nchini Kenya zaidi serikali inaendesha uchunguzi wa chembechembe za DNA, za wanafunzi 21 wa shule ya msingi ya Endatasha baada yao kuteketea kiasi ya kutotambulika, kabla ya miili yao kutolewa kwa familia.
Miili limewaacha wazazi kwenye njia panda wasijue la kufanya, wakati huu maswali yakiendelea kuulizwa je nani wakulaumiwa baada ya mkasa huo wa moto shuleni.
Kufahamu mengi skiza makala haya.
Mon, 16 Sep 2024 - 284 - Kenya: Vikundi vya kina mama vyajitokeza kupinga ukeketaji
Katika makala haya tunajikiti kuangazia uketetetaji ambapo wasichana wamekuwa ukiendelea kukeketewa nchini Kenya licha ya serikali kanzisha kampeni ya kuhamasisha umma kuhusu athari zinazotokana na ukeketaji huo.
Jamii za Kenya, kupitia kwa kina mama na wasichana waliopitia ukeketaji kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii wameanzisha vikundi vya kutetea haki za wasichana ili kuwalinda kutokana na ukeketaji huo.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Tue, 27 Aug 2024 - 283 - Kenya : Jamii za mipakani zataka serikali kuwapa vitambulisho
Jamii zinazoishi mikapani nchini Kenya kwa muda zimekuwa zikikosa huduma muhimu ya kupata vitambulisho kutoka na sababu ambazo wenyewe wanasema serikali inawabagua.
Katika makala haya tunajikiti kuangazia masaibu ya jamii za mipakani nchini kenya kupata vitambulisho.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Sat, 24 Aug 2024 - 282 - Kenya : Mawikili watoa mafunzo ya sheria kwa vijana
Mawakili mjini Mombasa pwani ya Kenya wamenza kutoa mafunzo ya sheria kwa vijana waliokuwa wakiandamana kushinikiza mabadiliko.
Mawakili hao ambao ni wanachama wa chama cha mawakili nchini LSK, wamesema hatua hiyo imechochewa na maandamano yaliokuwa ya vijana maarufu kama Gen-Z leo lengo lao kuu likiwa kuwawajibisha viongozi serikalini.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya
Sat, 17 Aug 2024 - 281 - Tanzania : Human Right Watch lasema Tanzania inawahangaisha raia wa Ngorongoro
Katika makala haya saba yetu inalenga taifa la Tanzania eneo la Ngorongoro ambapo serikali imekuwa ikiwahamisha wenyeji eneo hilo, ili kuihifadhi eneo hilo kutokana na historia yake.
Tuangazia repoti ya shirika la kimataifa la kutete haki za biandamu la Human Watch ambayo imetuhumu serikali ya Tanzania kwa kuwafurusha kwa nguvu mamia ya raia wa kimasaai kutoka eneo la Ngorongoro, maafisa wa wanyama pori wakidaiwa kuwahangaisha kwa kuwapiga wenyeji ili kuwafurusha kutoka katika ardhi za mababu zao.
Karibu kwenye makala haya utaskia kutoka kwa wadau mbalimbali huku tukijadili ripoti hii ya Human Right Watch.
Tue, 06 Aug 2024 - 280 - Kenya : Haki za wanawake pamoja na kina dada wanaojiuzaSat, 03 Aug 2024
- 279 - Kenya : Haki ya wanahabari kuteleza majukumu yao bila vikwazo
Juma hili tunaangazia haki za wanahabari kupeperusha habari zao bila kuingiliwa na vyombo vya usalama katika mataifa yao.
Shaba yetu bila shaka inalenga taifa la Kenya, nchi ambayo wanahabari wamejeruhiwa wakati wakitekeleza majukumu yao, ya kuangazia maandamano ya vijana wa Gen Z, ambao wamekuwa wakishinikiza mabadiliko nchini Kenya.
Kwa siku sasa kilio cha wanahabari nchini Kenya kimekuwa ni kutaka serikali kuheshimu haki zao kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao bila vikwazo.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Sat, 27 Jul 2024 - 278 - Kenya : Polisi wa Uingereza watuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu
Katika makala haya tunaangazia dhuluma zinazodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Uingereza ambao wana kambi ya mazoezi nchini Kenya leo la Nanyuki.
Wanajeshi hao wanadaiwa kuwabaka na kuwaua wanawake mbali na kuwacha vilipuzi katika maeneo ya mazoezi ambavyo baadaye hulipuka na kusababisha majiraha na maafa.
Wanawake wambao wamekuwa na uhusiano wa kimapaenzi na wanjeshi wa uingreza eneo hilo la Nanyuki wamesumulia namna gani wamesalia na majiraha ya moyo kutokana na kuachwa na wapenzi wao wa kizungu ambao baada ya mazoezi yao, wao hurejea nchini mwao licha ya kuwazalisha.
Tue, 16 Jul 2024 - 277 - Kenya : Wanaume wanapitia dhuluma za kijinsia kwenye ndoa, ila wamesalia kimya
Visa vya dhuluma dhidi ya wanawake vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara katika jamii mbalimbali barani Afrika na hata duniani,jambo ambalo limechangia sheria nyingi kuanzishwa kulinda wanawake,lakini hata hivyo dhuluma hizo zimeanza kuwakumba wanaume wengi kwa kunyanyaswa na kupingwa na wake wao.
Katika makala haya tunaangazia dhuluma za kijinsia dhidi ya wanaume shaba yetu ikilenga taifa la Kenya, ambapo mwanahabari wetu Victor Moturi alitangamana na wanaume ambao wamehangaishwa na kudhulumiwa kwenye jamiii nchini Kenya hasa eneo la Magharibu.
Kufahamu mengi skiza makala haya.
Wed, 10 Jul 2024 - 276 - Sudan Kusini inakabiliwa na hali ya binadamu kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi
Taifa la Sudan Kusini linashuhudia wimbi kubwa la wakimbizi wanaoendelea kukimbia vitra nchini Sudan, licha taifa hilo kuendelea kushuhudia changamoto nyingi tu ikiwemo ukosefu wa amani katika baadhi ya majimbo yake.
katika makala haya tunazama kuangazia ripoti ya shirika la Care in South Sudan ambayo imechangia ripoti kuhusiana na hali ya binadamu nchini Sudan Kusini.
Kufahamu mengi skiza makala haya.
Sat, 06 Jul 2024 - 275 - Kenya : Haki ya raia kuandamana kufikisha ujumbe kwa serikali
Nchini Kenya vijana wamekuwa wakiandamana kulalamikia kile wataja mpango wa serikali kuongeza kodi kwa kutumia mswada wa fedha wa mwaka 2024.
Idadi kubwa ya vijana hao wanapinga mswaada huo wanaosema utaongeza gharama ya maisha kipindi hiki wengi wao wakiwa tayari hawana ajira, makali ya gharama ya maisha nayo yakiendelea kulemaza shughuli zao za kila siku.
Maandamano hayo yameandliwa na kundi la vijana linalojiita Gen Z, yaani kizazi cha vijana waliozaliwa kati ya mwaka 1995 hadi 2010.
Vijana hawa wanadai serikali ya rais William ruto imeanza kuwa dhalimu kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa muhimu kama vile soda za wanawake na vinengnevyo.
Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi
Tue, 25 Jun 2024 - 274 - Amnesty International : Adabu ya kifo imeongezeka zaidi duniani
Idadi ya watu waliopewa adabu ya kifo iliongezeka zaidi mwaka 2023, mataifa ya mashariki ya kati na nchini Somalia abadu hiyo ikiripotiwa kuwa ya juu zaidi.
Kwa mjibu wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, katika ripoti yake ya kila mwaka, zaidi ya watu 1, 153 walipewa adabu ya kifo mwaka 2023 pekee, bila kujumuisha idadi kutoka nchini China, taifa ambalo linaripotiwa kuwa msiri katika kutoa taarifa kama hizi.
Idadi hii ni asilimia 30 zaidi ikilinganishwa na mwaka 2022.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Tue, 18 Jun 2024 - 273 - Kenya : Haki za watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi wanataka kutambuliwa zaidi
Katika makala haya ni awamu ya pili tunaendelea na mazungumzo yetu na bwana meshaka Sisende raia wa Kenya anayeishi na ulemavu wa ngozi.
Juma lililopita tuliangazia pakubwa changamoro wanazopitia raia hawa naoishi na ulemavu wa ngozi na hapa tunazidi kuangazia mananikio ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi.
Miaka kadhaa iliopita mauwaji ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi yalikithiri sana nchini Tanzania, hatua iliochangia viongozi wa tabaka mbalimbali kusimama kidete kukemea mauwaji hayo mamlaka nazo zikiwakamata waliokuwa wakihusishwa na mauaji hayo kwa misingi ya kishirikiana.
Ni hapo ndipo wasanii kama vile Herbert Naktare maarufu Nonini kutoka nchini Kenya aliachilia wimbo wake wa Colour Kwa Face, kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwakumbatia watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Mon, 17 Jun 2024 - 272 - Haki za raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi hapa Africa
Kila mwaka Juni 14 dunia huadimisha siku ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi sherehe zilizoanza kuadimisha tangu mwaka 2014, ili kuhamasisha jamii kwamba watau wanaoishi na ulemavu wa ngozi wao ni watu wa kawaida katika jamii.
Katika makala haya Meshaka Sisende kutoka nchini Kenya anasimulia maisha ya kawaida ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya
Wed, 12 Jun 2024 - 271 - Tume ya haki za binadamu nchini Uganda yatuhumiwa kuegemea upande wa serikali
Makala haya yanaangazia tendekazi wa tume za kutetea haki za biandamu za serikali zetu za Africa mashariki.
Hii ni baada ya lalama kutoka kwa kiongozi wa upinznai nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine kwamba tume ya haki nchini Uganda imekuwa ikiegemea upande wa serikali katika kutekeleza majukumu yake.
Robert Kyagulanyi,amelazimika kuondoa lalama zake mbele ya tume ya haki ya kutetea haki za biandamu nchini Uganda kutokana na madai inayosema tume hiyo imeshindwa kuyashughulikia.
Wine alikuwa amewasilisha kesi yake mwaka 2018 akilalamikia hatua ya polisi nchini Uganda kukiuka haki zake kwa kumzuia kuandaa tamasha za muziki zaidi ya 20, mbali na polisi kuchukuwa nyombo vyake vya mziki, hili akidai lilimzuia kupata haki yake ya kupata mapato kutokana na mrengo wake wa kisiasa.
Fahamu mengi kwa kuskiza makala haya.
Fri, 31 May 2024 - 270 - Kenya : Unyanyapaa wanaopitia kina mama tasa kwa jamii
Katika makala haya tunaangazia haki za kina dada ambao hawajafanikiwa kupata watoto katika jamii zetu za kiafrica.
Barani Afrika wanawake ambao hawana uwezo kupata watoto au wale huchukuwa muda mrefu kupata watoto , hupitia changamoto si haba ,na kukosa haki,kama vile kutotambuliwa na jamii,uridhi wa Mali na hata wengine kufukuzwa kwenye ndoa,hali hiyo ikichochewa na tamaduni ambazo zimekita mizizi.
Kwa mjibu wa twakwimu za shirika la afya duniani WHO ni kwamba wanawake 15 kati ya 100 barani Afrika hawana uwezo wa kupata watoto, na kati ya wanawake 6 angalau mmoja huwa hawana uwezo wa kupata mtoto kidunia.
Swala la kukosa kupata mtoto hushuhudiwa kati ya wanawake na wanaume, ila hapa barani africa kasumbuka mara nyingi huelekezewa kina mama, hili likisababisa dhiki, unynyapaa, ufukara miongoni mwa wanawake wengi wao sasa wakiathiriwa na afya ya akili na hata kisaikolojia.
Licha ya tatizo hili kuwa na suluhu, wengi wamesalia kukosa imani kutokana kwani hawana pesa za kutafuta tatibu husika.
Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
Tue, 21 May 2024
Podcast simili a <nome>
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- Tiempo de Juego COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Les Grosses Têtes RTL
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR