Nach Genre filtern

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu

1081 - Fahamu kwa undani kipindi cha Majilio.
0:00 / 0:00
1x
  • 1081 - Fahamu kwa undani kipindi cha Majilio.

    Karibu katika kipindi cha Tafakari ya Mama Bikira Maria, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, leo anazungumzia juu ya kipindi cha Majilio.

    Tue, 03 Dec 2024 - 29min
  • 1080 - Je, Wanandoa watatambuana Mbinguni baada ya kufa?

    Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, tukiungana na Frateri Franco Abel Ubamba kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea, akijibu swali lililoulizwa na Msikilizaji wetu likihoji hivi, mimi nimefiwa na Mke, na Mke ameenda Mbinguni, na mimi nikifa nikaenda Mbinguni tutatambuana?

    Tue, 03 Dec 2024 - 26min
  • 1079 - Je, wafahamu thamani ya mateso ya Yesu katika maisha yako?

    Ungana nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania, akitufundisha juu ya thamani ya mateso.

    Tue, 03 Dec 2024 - 50min
  • 1078 - Kwanini kipindi cha Majilio Wanakwaya hawaimbi Utukufu?

    Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, tukiungana na Frateri Elikana Nyagabona kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, akijibu swali hili Kwanini kipindi cha Majilio Wanakwaya hawaimbi Utukufu?

    Tue, 03 Dec 2024 - 27min
  • 1077 - Mtakatifu Anna ni nani katika Bibilia?

    Karibu uungane nami Esther Magai Hangu, katika kipindi cha Tumsifu Maria leo tupo na Padre Fabian Ngeleja Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Josephine Bakhita Nyamanoro, Jimbo Kuu Katoliki Mwanza akituelezea maajabu ya Mama mzazi wa Bikira Maria Mtakatifu Anna.

    Fri, 29 Nov 2024 - 59min
Weitere Folgen anzeigen