Filtrer par genre
Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu
- 1062 - Huu ndiyo uhusiano wa Huruma ya Mungu na Manabii.
Karibu uungane nami Esther Magai katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera, akitufundisha juu ya huruma yake ni ya milele akijikita zaidi katika Manabii na Huruma ya Mungu.
Thu, 21 Nov 2024 - 52min - 1061 - Je, unafahamu huruma ya Bikira Maria kwa Wanadamu?
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, Majibu yanatolewa na Frateri Ayubu Polycarp Mwashibili kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu katoliki Songea, katika Swali hili naomba kueleweshwa juu ya unyenyekevu wa Mama Bikira Maria na Huruma kwa Mama Bikira Maria.
Thu, 21 Nov 2024 - 23min - 1060 - Sikiliza tafakari ya Injili ilivyoandikwa na Luka 19:1-10.
karibu katika kipindi cha Tafakari Nasi, Mwezeshaji ni Padre John Bosco kutoka Jimbo Kuu la Dar es salaam, leo anatutafakarisha juu ya Injili ya Luka 19:1-10.
Thu, 21 Nov 2024 - 25min - 1059 - Fahamu njia rahisi ya kujisajili na mfuko wa bima ya Taifa (NHIF) kwa Wanafunzi.
Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Elimu Jamii, Mwezeshaji ni Dkt. Raphael Malaba, Meneja wa Mfuko wa Bima ya Taifa (NHIF) Mkoa wa Kinondoni, akitufundisha juu ya matumizi ya mifumo katika usajili wa Wanafunzi.
Thu, 21 Nov 2024 - 51min - 1058 - Fahamu historia ya Mfalme Herode.
Karibu katika kipindi cha ujumbe wa Biblia, Mwezeshaji ni Padre Titus, Mtaalamu wa Maandiko Mtakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Jimbo Kuu la Mwanza akizungumzia juu ya Mfalme Herode.
Thu, 21 Nov 2024 - 51min - 1057 - Je, wafahamu Bikira Maria alibaki kuwa Bikira baada ya kumzaa Yesu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Ayubu Mwashibili, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu Katoliki Songea, nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Je, Bikira Maria alibaki kuwa Bikira baada ya kumzaa Yesu?
Wed, 20 Nov 2024 - 26min - 1056 - Fahamu uwajibikaji wa Wanandoa katika kulinda na kutetea Uhai.
Ungana nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Pro Life utetezi wa uhai, Wakufunzi wetu leo Wanaendelea na mada juu ya Utamaduni wa Uhai, mume na mke wamejaliwa kutunza watoto.
Wed, 20 Nov 2024 - 52min - 1055 - Fahamu mambo ya kuzingatia kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Ungana nami Mtangazaji wako Judith Mpalanzi katika Kipindi cha Elimu Jamii ambapo leo tupo na Bwana Stephen Motambi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akizungumzia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na tunapoelekea kwenye Kampeni za uchaguzi huo.
Wed, 20 Nov 2024 - 38min - 1054 - Huruma ya Mungu na Manabii wa Agano la kale.
Ungana nami Judith Mpalanzi, katika Kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera, akiendelea kutufundisha juu ya Huruma ya Mungu akitazama Manabii mbalimbali.
Wed, 20 Nov 2024 - 50min - 1053 - Je Kwanini Makatekista wameonekana hawana thamani?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Maiko Paulo Mangazini, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu Katoliki Songea, nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Je Kwanini Makatekista wameonekana hawana thamani na kuonekana ni watu waliokosa kazi?
Wed, 20 Nov 2024 - 29min - 1052 - Je, wafahamu kwanini Kanisa Inawaombea Marehemu?
Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, akitufundisha juu ya Marehemu.
Wed, 20 Nov 2024 - 27min - 1051 - Fahamu huruma ya Mungu kupitia Vitabu vya Manabii.
Uungana nami Happiness Mlewa, katika Kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera, akiendelea kutufundisha juu ya Huruma ya Mungu akitazama Vitabu vya Manabii.
Wed, 20 Nov 2024 - 51min - 1050 - Ifahamu Sheria Ya Kanisa Na. 1030 -1029 Wenye Daraja Takatifu
Ungana nami Raymond Karega, Katika Kipindi cha Sheria za Kanisa ambapo kwa namna ya pekee Padre Ladslaus Mgaya, Mwanasheria wa Sheria za Kanisa kutoka Jimbo Katoliki Njombe akiwa anaangazia Sheria ya Upadrisho 1030.
Mon, 18 Nov 2024 - 57min - 1049 - Je, Wafiadini Mashahidi wa Uganda wapo Mbinguni?
Karibu katika Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Elikana Nyagabona, Kutoka Seminari Kuu Ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu La Songea, nikijibu swali la Msikilizaji linalosema wakati wanakufa mashahidi wa Uganda waliuawa pia ambao huwakuwa Wakatoliki, Je wapo Mbinguni?
Mon, 18 Nov 2024 - 23min - 1048 - Sakramenti Takatifu zinatupatia nini katika maisha yetu ya Kiroho?
Karibu Katika Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Barnabas Myushi, Kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu La Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema, Sakramenti zinatupatia nini katika maisha yetu ya Kiroho?
Mon, 18 Nov 2024 - 21min - 1047 - Nini maana ya Karisimatiki Katoliki?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Alphonce Mkumi, Kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu La Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Nini maana ya Karisimatiki Katoliki?
Mon, 18 Nov 2024 - 25min - 1046 - Ni, dawa gani bora kwa Ugonjwa wa Kisukari?
Ungana nami Judith Mpalanzi katika Kipindi cha Ijue Afya yako, Kutoka Studio za Radio Maria Tanzania Mwezeshaji ni Daktari Juma Kupewa pamoja Daktari Samweli Salvatory Kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Fransisco Ifakara, wakielezea juu ya Ugonjwa wa Kisukari.
Fri, 15 Nov 2024 - 41min - 1045 - Ifahamu Historia ya Wazazi wa Bikira Maria
Ungana nami Esther Magai Hangu katika kipindi cha Tafakari nasi kutoka Studio za Radio Maria Tanzania, Mwezeshaji ni Padre Fabian Ngeleja Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Josephina Bakhita- Nyamanoro Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akielezea Familia ya Bikira Maria.
Fri, 15 Nov 2024 - 24min - 1044 - Ni, kwanini Yesu alijaribiwa na Shetani?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Daudi Fungameza, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu La Songea, nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Kwanini Yesu alijaribiwa na Shetani?
Fri, 15 Nov 2024 - 29min - 1043 - Je, tunaipataje Huruma ya Mungu katika maisha yetu?
Ungana nami Judith Mpalanzi, katika Kipindi cha Katekisimu Shirikishi Katoliki Kutoka Studio za Radio Maria Tanzania, leo tupo na Padre Dominic Mavula C.P.P.S Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria, akituongoza kujifunza Huruma ya Mungu katika maandiko Matakatifu.
Fri, 15 Nov 2024 - 50min - 1042 - Je ni utaratibu gani unaofuatwa wakati wa kumchagua Papa?
Karibu uungane nami Patrick Paschal Tibanga katika kipindi cha Historia ya Kanisa, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, akijibu swali hili Je ni utaratibu gani unaofuatwa wakati wa kumchagua Papa?
Thu, 14 Nov 2024 - 57min - 1041 - Je, kwanini historia ya Yuda Isikarioti haipo kwenye Biblia Takatifu?
Karibu uungane nami Patrick Paschal Tibanga katika kipindi cha Historia ya Kanisa, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, akijibu swali hili Je, kwanini historia ya Yuda Isikarioti haipo kwenye Biblia Takatifu?
Thu, 14 Nov 2024 - 56min - 1040 - Je, Kuna tofauti gani kati ya Rozari na Novena?
Karibu uungane nami Patrick Paschal Tibanga katika kipindi cha Historia ya Kanisa, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, akijibu swali hili Je, Kuna tofauti gani kati ya Rozari na Novena?
Thu, 14 Nov 2024 - 57min - 1039 - Kwanini Sala ni pambano?
Karibu uungane nami Elizabeth Masanja , katika kipindi cha Utume wa Walei, Leo nipo na Bi.Rosse Gerald, akiendelea kufundisha juu ya mada kwanini Sala ni pambano tutpambanie kuwaombee marehemu.
Thu, 14 Nov 2024 - 57min - 1038 - Mfahamu mfalme Herode mkubwa.
Karibu uungane nami Martin Joseph , katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Leo nipo na Padre Titus Amigu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akiendelea kufundisha juu ya kukoseana na kusamehana akiwatazama Wafalme mbalimbali, leo anamzungumzia Mfalme Herode.
Thu, 14 Nov 2024 - 39min - 1037 - Kwanini huruma yake ni ya milele?
Karibu uungane nami Esther Magai katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominick Mavula C.PP.S Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania.
Thu, 14 Nov 2024 - 51min - 1036 - Ipi nafasi ya mabaraza ya usuluhishi na mahakama kuhusu talaka?
Karibu uungane nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Ijue Sheria ambapo Mwezeshaji wetu Mheshimiwa Hassan Mlanga Hakimu mwandamizi katika Mahakama ya mwanzo Bomani Iringa Mjini,akizungumzia juu ya nafasi ya mabaraza ya usuluhishi na mahakama katika mashauri ya talaka.
Thu, 14 Nov 2024 - 55min - 1035 - Je, kuna ishara gani za mtu kutangazwa Mtakatifu?
Karibu uungane nami Patrick Paschal Tibanga katika kipindi cha Historia ya Kanisa, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, akijibu swali hili Je, kama mtu ni mtakatifu ni lazima Kanisa lione ishara gani ili limtangaze Mtakatifu?
Thu, 14 Nov 2024 - 56min - 1034 - Je, unafahamu maana ya Konstantinopoli.
Karibu uungane nami Patrick Paschal Tibanga katika kipindi cha Historia ya Kanisa, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, akijibu swali lililoulizwa hivi nini maana ya Konstantinopoli.
Thu, 14 Nov 2024 - 56min - 1033 - Je, kuna hukumu baada ya kifo?
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, tukiungana na Frater Daudi Fungameza kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, akijibu swali hili, Kadiri ya waraka Waebrania 9:27 “Mwanadamu baada ya kufa anapewa hukumu” Je, Hukumu hiyo ni ipi?
Thu, 14 Nov 2024 - 30min - 1032 - Fahamu taaluma ya tafsiri na maendeleo yake duniani.
Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Elimu Jamii, Mwezeshaji ni Kusanja Emmanuel Kusanja, Msanifu Lugha kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), leo anatufundisha juu ya taaluma ya tafsiri na maendeleo duniani.
Thu, 14 Nov 2024 - 51min - 1031 - Fahamu umuhimu wa kujitoa Sadaka.
Karibu uungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Tafakari Nasi leo studio tupo naye Padre Frank Mwinami kutoka Jimbo Katoliki Njombe, ujumbe wa leo unatoka Luka 17:5-10. Utumishi usiokuwa na faida.
Wed, 13 Nov 2024 - 24min - 1030 - Je, Wanafamilia wana wajibu gani katika Malezi?
Karibu uungane nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Pro Life utetezi wa uhai, Wakufunzi wetu leo Wanazungumzia mada ya Utamaduni wa Uhai, Malezi bora katika Familia .
Wed, 13 Nov 2024 - 54min - 1029 - Mfahamu mfalme Herode enzi za Utawala wake kabla ya kuja Kristo.
Karibu uungane nami Happiness Mlewa , katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Leo nipo na Padre Titus Amigu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akiendelea kufundisha juu ya kukoseana na kusamehana akiwatazama Wafalme mbalimbali, leo anamzungumzia Mfalme Herode.
Wed, 13 Nov 2024 - 48min - 1028 - Je, wafahamu kwanini Wakatoliki hawachukui hatua pale wanapotukanwa na kuongelewa vibaya?
Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, tukiungana na Frateri Daud Fungameza kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, akijibu swali linalo kwanini Wakatoliki hawakasiriki pale wanapo tukanwa na kuwaongelewa vibaya viongozi wao?
Wed, 13 Nov 2024 - 31min - 1027 - Ifahamu nguvu ya Huruma ya Mungu kadiri ya Maandiko Matakatifu.
Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula, C.PP.S Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania akiendelea na mada Huruma yake ni ya Milele.
Wed, 13 Nov 2024 - 55min - 1026 - Watanzani wahimizwa kusherekea miaka 63 ya Uhuru wa Taifa kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.
Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Elimu ya Jamii Wawezeshaji Mapinduzi Boniface Mdesa Mkuu wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na Daniel Mweta kutoka Kitengo cha Maendeleo na Biashara (TANAPA) mada ni juu Twenzetu kileleni katika Mlima wa Kilimanjaro .
Wed, 13 Nov 2024 - 49min - 1025 - Nitawezaje kuwasaidia Maskini wakati na mimi ni Maskini?
Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika kipindi cha maswali ya husuyo Imani ambapo Frateri Hipolith Olomi anajibu swali lililouliza “Kanisa linahimiza kuwasaidia watu Maskini sasa mimi nitawezaje kuwasaidia wakati na mimi mwenyewe ni Maskini.”?
Tue, 12 Nov 2024 - 29min - 1024 - Ukuu wa Mama Bikira Maria katika vita kuu ya ushindi.
Karibu uungane nami Judith Mpalanzi, katika kipindi cha Tafakari Nasi, Leo nipo na Padre Gidioni Kitamboya Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, akifundisha juu ya ukuu wa mama Bikira Maria katika vita kuu ya ushindi.
Tue, 12 Nov 2024 - 25min - 1023 - Je wafahamu ukuu wa sadaka ya Misa Takatifu?
Karibu uungane nami John Samky, katika kipindi cha Tafakari nasi, Leo nipo na Padre James Singo kutoka Jimbo Katoliki Same, akifundisha juu ya ukuu wa sadaka ya Misa Takatifu.
Tue, 12 Nov 2024 - 25min - 1022 - Mfahamu Mfalme Ahabu na mkewe Malkia Yezebe.
Karibu uungane nami Esther Magai, katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Leo nipo na Padre Titus Amigu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akiendelea kufundisha juu ya kukoseana na kusamehana akiwatazama Wafalme mbalimbali, leo anamzungumzia Mfalme Ahabu na mke wake Malkia Yezebe.
Tue, 12 Nov 2024 - 53min - 1021 - Kwanini huruma yake ni ya milele?
Karibu uungane nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominick Mavula C.PP.S Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania.
Tue, 12 Nov 2024 - 49min - 1020 - Je, kuna ulazima wa kuwaombea Marehemu?
Karibu uungane nami Frateri Ayubu Polycarp Mwashubili nikijibu swali linalohoji “kuna ulazima wa kuwaombea marehemu”?
Tue, 12 Nov 2024 - 27min - 1019 - Je, wafahamu njia salama ya kuendesha Gari Barabarani?
Ungana nami Martin Joseph, Katika Kipindi cha Usalama Barabarani Kutoka Studio za Radio Maria Tanzania leo tupo na Afande Michael Deleli, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, ikiwa mada ni endesha salama ufike salama.
Mon, 11 Nov 2024 - 57min - 1018 - Nini Maana ya Sadaka ya Malimbuko?
Karibu katika Kipindi cha Maswali yahusuyo Imani leo tupo na Frateri Ayubu Mwashibili, Kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu La Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema nini maana ya Malimbuko au Sadaka ya Malimbuko.
Mon, 11 Nov 2024 - 24min - 1017 - Je, Familia ina nafasi gani katika Sakramenti Takatifu?
Ungana nami John Samky, katika Kipindi cha Familia Bora na Nyumba Aminifu Wawezeshaji ni Wakufunzi kutoka Familia bora katika Nyumba Aminifu, wakiendelea kutufundisha juu ya Mlango wa Familia Aminifu.
Mon, 11 Nov 2024 - 56min - 1016 - Ni, vigezo vipi vinatumika kuwateua Watakatifu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Ayubu Mwashibili, Kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu La Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Ni, vigezo vipi vinatumika kuwateua Watakatifu?
Mon, 11 Nov 2024 - 23min - 1015 - Nini maana ya fumbo la Umwilisho?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Cassian Lebba Kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Nini maana ya Fumbo la Umwilisho?
Fri, 08 Nov 2024 - 28min - 1014 - Ni, kwa namna gani tunawaombea Marehemu?
Uungane nami Judith Mpalanzi katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera, akiendelea kutufundisha juu ya msaada wa Binadamu kwa ndugu zetu Marehemu.
Fri, 08 Nov 2024 - 45min - 1013 - Je unaifahamu medali ya miujiza?
Ungana nami Judith Francis Katika kipindi cha Elimu Jamii, Mwezeshaji ni Padre Respicious Sigoma kutoka Jimbo Katoliki Singida, anatufundisha juu ya medali ya miujiza.
Thu, 07 Nov 2024 - 36min - 1012 - Fahamu msaada wa Binadamu kwa ndugu zetu Marehemu.
Karibu uungane nami Esther Magai Hangu katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera, akiendelea kutufundisha juu ya msaada wa Binadamu kwa ndugu zetu Marehemu.
Thu, 07 Nov 2024 - 50min - 1011 - Fahamu kuanzishwa kwa sherehe ya Watakatifu wote.
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, tukiungana na Frateri Cassian Lebba kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, akijibu swali hili sherehe ya Watakatifu wote ilianzishwa lini na nani?
Thu, 07 Nov 2024 - 26min - 1010 - Zifahamu tabia mbaya na madhara yake katika Jamii.
Karibu uungane nami John Samky katika kipindi cha Uraibu, Mwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha kutoka Jimbo Katoliki Moshi, leo anatufundisha juu ya madhara ya tabia mbaya katika jamii.
Thu, 07 Nov 2024 - 52min - 1009 - Mfahamu Mfalme Ahabu na mkewe Malkia Yezebe.
Karibu uungane nami John Samky, katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Leo nipo na Padre Titus Amigu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akiendelea kufundisha juu ya kukoseana na kusamehana akiwatazama Wafalme mbalimbali, leo anamzungumzia Mfalme Ahabu na mke wake Malkia Yezebe.
Wed, 06 Nov 2024 - 54min - 1008 - Ufahamu wajibu wa Mkristo kuwafua Mavazi yetu katika Damu ya Mwanakondoo.
Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika kipindi cha Tafakari Nasi, Mwezeshaji ni Padre Yohanes Kalua, kutoka Parokia ya Bikira Maria Malkia Ihalula Jimbo Katoliki Njombe akitufundisha juu ya wajibu wa kuwafua mavazi yetu katika Damu ya Mwanakondoo.
Wed, 06 Nov 2024 - 26min - 1007 - Fahamu sababu zinazosababisha kutowalea watoto katika Makuzi mema.
Karibu uungane nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Pro Life utetezi wa uhai, Wakufunzi wetu leo wanaendelea na mada juu ya Utamaduni wa Uhai, kipengele cha kumlea Mtoto vizuri katika Makuzi ya kiroho na kimwili.
Wed, 06 Nov 2024 - 51min - 1006 - Je, wafahamu uhusiano Sadaka za kale na za Bwana wetu Yesu Kristo?
Karibu uungane nami Frateri Cassian Leba kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, nikijibu swali linalohoji Je, kuna uhusiano gani katika sadaka za kale za kiyahudi na Bwana Yesu Kristo?.
Wed, 06 Nov 2024 - 27min - 1005 - Ufahamu msaada wa Wakristo kwa Watu walio tangulia mbele ya haki.
Karibu uungane nami Esther Magai Hangu, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi leo tupo na Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa Radio Mbiu Sauti Faraja Kagera – Jimbo Katoliki Bukoba akituongoza kujifunza mada ya juu ya Msaada wetu kwa Marehemu.
Wed, 06 Nov 2024 - 55min - 1004 - Fahamu juu ya tokeo la Fatima.
Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika kipindi cha Tafakari Nasi, Mwezeshaji ni Padre Gidioni Kitamboya OFMCap, kutoka Jimbo Kuu la Dodoma akitufundisha juu ya tokeo la Fatima ni kwaajili yako.
Wed, 06 Nov 2024 - 27min - 1003 - Je, wafahamu kwanini Kanisa liliweka mwezi 11 wa kuwaombea Marehemu?
Ungana nami Emeliana Masondole katika kipindi cha Tafakari Nasi, Mwezeshaji ni Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, anatafakari juu ya mwezi wa kumi na moja yaani mwezi Marehemu.
Wed, 06 Nov 2024 - 28min - 1002 - Fahamu kwanini Wanawake Washiriki katika Uongozi.
Ungana nami Agatha Kisimba katika kipindi cha Jinsia na Maendeleo, Kutoka Studio za Radio Maria Tanzania ambapo leo nipo na Wadau wa Masuala ya Kijinsia Bi. Tabu Ally, Bi.Anna Sangai na Bwana Deogratius Temba mchambuzi, mwezeshaji na mtafiti wa masuala ya Kijinsia akielezea Ukweli kuhusu Wanawake na Uongozi.
Tue, 05 Nov 2024 - 24min - 1001 - Wakristo waaswa kuyaiga yale mema aliyoyaishi Mfalme Suleimani.
Ungana nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Kutoka Studio za Radio Maria Tanzania leo tupo na Padre Titus Amigu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akiendelea kufundisha juu ya kukoseana na kusamehana akiwatazama Wafalme mbalimbali, akiendelea kuelezea Maisha ya Mfalme Suleimani.
Tue, 05 Nov 2024 - 53min - 1000 - Huruma ya Mungu ni nini?
Ungana nami Martin Joseph katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania, akielezea juu ya Huruma yake ni ya Milele.
Tue, 05 Nov 2024 - 52min - 999 - Wito wa Msamaha ni nini?
Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika kipindi cha Fahamu Wito wako, Mwezeshaji ni Padre Innocent Bahati Mushi OFMCap, kutoka Jimbo Kuu la Arusha, akiendelea kutufundisha juu ya Wito wa Utakatifu kupitia Toba na Msamaha.
Tue, 05 Nov 2024 - 56min - 998 - Ni, kwanini Sakramenti Takatifu ni muhimu katika maisha ya Mwanadamu?
Karibu uungane nami John Samky, katika kipindi cha Familia Bora na Nyumba Aminifu leo tupo na Wakufunzi kutoka Famila bora katika Nyumba aminifu, wakielezea Dirisha la Nyumba Aminifu.
Tue, 05 Nov 2024 - 51min - 997 - Je, wafahamu Sheria ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ?
Karibu uungane nami Raymond Karega, katika kipindi cha Sheria za Kanisa Kutoka Studio za Radio Maria Tanzia leo tupo Padre Ladislaus Mgaya, Mwanasheria wa Sheria za Kanisa Katoliki Kutoka Jimbo Katoliki Njombe, ambapo leo anatuongoza kujifunza sheria ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ya Upadre.
Mon, 04 Nov 2024 - 51min - 996 - Nini maana ya Samehe mara Sabini?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Franco Ubamba, Kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu La Songea nikijibu swali la Msikilizaji linalosema, Nini maana ya Samehe Mara Sabini?
Mon, 04 Nov 2024 - 27min - 995 - Je, wafahamu Utajiri wa Mfalme Suleiman?
Karibu uungane nami Esther Magai Hangu, katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Leo nipo na Padre Titus Amigu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akiendelea kufundisha juu ya kukoseana na kusamehana akiwatazama Wafalme mbalimbali, leo anamzungumzia Mfalme Suleiman.
Mon, 04 Nov 2024 - 53min - 994 - Je, Mwamini Mlei anaweza kuwa Mtakatifu?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Desderius Mwambaluka, Kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Jimbo Kuu la Songea, nikijubu swali Msikilizaji linalosema Je, Mwamini Mlei anaweza kuwa Mtakatifu?
Fri, 01 Nov 2024 - 28min - 993 - Ni, utofauti gani uliopo kati ya Mama Kanisa na Mama wa Kanisa?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Valentino Hipolith Olomi, Kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu la Songea, nikijibu swali la Msikilizaji linalosema kuna utofauti gani kati ya Mama Kanisa na Mama wa Kanisa?
Fri, 01 Nov 2024 - 27min - 992 - Je, dalili za Ugonjwa wa Damu ni zipi?
Karibu uungane nami Martin Joseph katika kipindi cha Ijue Afya yako, Kutoka Studio za Radiomaria Tanzania leo tupo na Daktari Abdul Hussein Mogella, Kutoka Hosptali ya Rufaa ya Mtakatifu Francisco wa Asizi Ifakara, akituongoza kujifunza Magonjwa ya Damu kwa ujumla.
Fri, 01 Nov 2024 - 41min - 991 - Kwanini uhai ni muhimu?
Karibu uungane nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Pro life utetezi wa uhai, Wawezeshaji ni Godfrey Mkaikuta, Janeth Akaro na Witness Joachim kutoka Pro life Tanzania, wakitufundisha juu ya utamaduni wa uhai.
Thu, 31 Oct 2024 - 50min - 990 - Je, unafahamu kuwa Sala ni mpambano?
Karibu uungane nami Elizabeth Masanja katika kipindi cha Utume wa Walei, Mwezeshaji ni Padre Vitalis Kasembo, Mkurugenzi wa Utume wa Walei Jimbo Kuu la Dar es salaam, akizungumzia juu ya mada ya Sala ni Mpambano.
Thu, 31 Oct 2024 - 48min - 989 - Sikiliza shuhuda za matumizi ya Nishati safi ya kupikia.
Karibu katika kipindi cha Jinsia na maendeleo katika kipindi hiki tutasikiliza shuhuda za wananchi juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na madhara ya kutumia nishati chafu.
Wed, 30 Oct 2024 - 19min - 988 - Je unafahamu jinsi ya kutengeneza nishati mbadala ya kupikia?
Karibu ufuatilie kipindi cha Jukwaa la Vijana ambapo katika kipindi hiki tunajadili mada kuhusu “utengenezaji wa Nishati mbadala.
Wed, 30 Oct 2024 - 45min - 987 - Fahamu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia?
L'articolo Fahamu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia? proviene da Radio Maria.
Wed, 30 Oct 2024 - 28min - 986 - Ifahamu Ibada ya Moyo safi wa Bikira Maria.
Karibu katika kipindi cha Tafakari ya Bikira Maria, ambapo Padre Gideon Kityamboya kutoka Jimbo Kuu la Dodoma, anatufundisha juu ya Ibada ya Moyo Safi wa Maria.
Tue, 29 Oct 2024 - 23min - 985 - Fahamu uhusiano wa Mfalme Suleimani na Sakramenti ya Upadre.
Karibu katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Mwezeshaji ni Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), akitufundisha juu ya historia ya Mfalme Suleimani.
Tue, 29 Oct 2024 - 51min - 984 - Fahamu nguvu ya kusali Rozari Takatifu katika Familia ya Mungu.
Ungana nami Agatha Kisimba katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania leo anatufundisha juu ya dondoo za kusali Rozari Takatifu.
Tue, 29 Oct 2024 - 50min - 983 - Je, kwanini ubani na chetezo hutumika katika vipindi vya sikukuu na Dominika?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani, ambapo Frateri Constantine Kennedy kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea, anajibu Swali lililoulizwa na Msilikizaji wetu likihoji, Je, kwanini ubani na chetezo hutumika katika vipindi vya sikukuu na Dominika pekee?
Tue, 29 Oct 2024 - 21min - 982 - Je, ni kwa namna gani toba na msamaha hutuletea Utakatifu?
Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika kipindi cha Fahamu wito wako, Mwezeshaji ni Padre Innocent Bahati Mushi, OFMCap kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela kilichopo Jimbo Kuu Katoliki Arusha, akiendelea na mada ya Utakatifu kwa njia ya toba na msamaha.
Tue, 29 Oct 2024 - 51min - 981 - Fahamu mwaliko wa Baba Mtakatifu Fransisko “Enendeni na alikeni kila mtu kwenye karamu”.
Karibu uungane na Happiness Mlewa katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji na Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania, akitufundisha juu ya umisionari.
Mon, 28 Oct 2024 - 52min - 980 - Hii ndiyo nguvu ya neno la Mungu katika maisha ya Mkristu.
Karibu uungane na Padre James Singo kutoka Jimbo Katoliki Same katika kipindi cha Tafakari nasi, leo anatutafakarisha juu ya nguvu ya neno la Mungu katika maisha ya Mkristu.
Mon, 28 Oct 2024 - 20min - 979 - Mfahamu Mwinjili Yohane na alivyofanya utume wake.
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Katoliki Songea, ambapo Frateri Kamfupili anajibu swali lililoulizwa hivi: Je, Mwinjili Yohane aliyeandika Injili ni yule alieyekabidhiwa na Yesu Kristo pale Msalabani kwa Mama Bikira Maria?
Mon, 28 Oct 2024 - 20min - 978 - Fahamu sifa ya Bikira Maria Mfariji.
Ungana nami Happiness Mlewa katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.C, Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania, akiendelea kutufundisha juu ya Bikira Maria Mfariji.
Mon, 28 Oct 2024 - 53min - 977 - Nini maana ya kumkufuru Roho Mtakatifu?
Karibu uungane nami Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Roho Mtakatifu na Kanisa, leo tupo na Mhashamu Josaphat Louis Lebulu, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, akituongoza kujifunza madhara ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
Mon, 28 Oct 2024 - 55min - 976 - Je, ni kweli Makadinali wa Afrika hawachaguliwi kuwa Mapapa?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, ambapo Frateri Noah Joshua Mwamfupe anajibu swali lililoulizwa hivi, Kwanini Makadinali wa Afrika hawachaguliwi kuwa Mapapa?
Mon, 28 Oct 2024 - 26min - 975 - Fahamu tafakaria ya Mama Bikira Maria kikao cha hekima na ukweli.
Karibu uungane nami Esther Magai Hangu katika kipindi cha Tafakari Nasi, Mwezeshaji ni Padre Fredrick Mwabena,OSB Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Benedicto Peramiho, kutoka Jimbo Kuu Katoliki Songea, akiendelea kutufundisha juu Mama Maria kikao cha hekima na ukweli.
Mon, 28 Oct 2024 - 28min - 974 - Fahamu Tafakari juu Kituo cha Hija cha Nyakijoga kilichopo Jimbo Katoliki Bukoba.
Karibu uungane na Mhashamu Method Kilaini, Askofu Msaidizi Mstaafu wa Jimbo Katoliki Bukoba katika kipindi cha Tafakari ya Bikira Maria, leo anatafakari juu na kuelezea kituo cha Hija cha Nyakijoga kilichopo Jimbo Katoliki Bukoba.
Mon, 28 Oct 2024 - 29min - 973 - Je, Watoto wanaweza kuwa na ugonjwa wa afya ya akili?
Karibu uungane nami John Samky katika kipindi cha malezi na makuzi ya Vijana, Mwezeshaji ni Sista Theresia Karubaga kutoka Jimbo Katoliki Zanzibar, akiendelea kutufundisha juu ya afya ya akili kwa Mtoto.
Mon, 28 Oct 2024 - 45min - 972 - Fahamu umuhimu wa ulaji wa Mbogamboga na Matunda.
Karibu uungane nami Elizabeth Masanja, katika kipindi cha Chakula na Lishe Mwezeshaji Bi. Nyamizi Julias, Afisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNS) mada ni juu Ulaji wa Mbogamboga na Matunda .
Mon, 28 Oct 2024 - 49min - 971 - Fahamu kwa kina juu ya Ugonjwa wa Saratani, Aina za Saratani&Dalili zake
Karibu uungane nami Mtangazaji wako Happiness Mlewa katika kipindi Ijue Afya Yako, Mwezeshaji Daktari Florence Peter Boke Kutoka Hospitali ya Good Samaritan Ifakara, akizungumzia juu ya Ugonjwa wa Saratani.
Mon, 28 Oct 2024 - 45min - 970 - Zifahamu Haki na Wajibu wa Mtoto.
Karibu uungane nami Mtangazaji wako Esther Magai Hangu katika kipindi cha ijue sheria, Mwezeshaji ni Bi. Rehema Mayagilo ambaye ni Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wiaya Iringa Mjini, akituongoza kujifunza Haki na Wajibu wa Mtoto.
Fri, 25 Oct 2024 - 45min - 969 - Je, wafahamu makosa yatokanayo na ulaji wa vyakula na madhara yake kiafya?
Karibu uungane nami Judith Mpalanzi katika kipindi cha Chakula na Lishe, Mwezeshaji ni Bi. Maria Ngilisho, Afisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), leo anatuelimisha juu makosa yanayofanywa kwenye Ulaji, uhifadhi na uzalishaji wa vyakula na madhara yake kiafya.
Fri, 25 Oct 2024 - 53min - 968 - Je, wafahamu utofauti kati ya Mafarisayo na Masadukayo?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Daudi Fungameza, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo Kuu Katoliki Songea, nikijibu swali la Msikilizaji linalosema utofauti kati ya Mafarisayo na Masadukayo.
Fri, 25 Oct 2024 - 28min - 967 - Ni, kwa namna gani Bikiria Maria ni Mfariji ?
ungana nami Esther Magai Hangu katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi, Mwezeshaji ni Padre Dominic Mavula C.PP.S, Mkurugenzi wa Matangazo Radio Maria Tanzania, akitufundisha juu ya Bikira Maria Mfariji.
Fri, 25 Oct 2024 - 52min - 966 - Je, wafahamu Sadaka ya Malimbuko?
Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani ukiwa nami Frateri Samson Tibianus, Kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Agustino Peramiho Jimbo kuu la Songea, nikijibu swali la Msikilizaji linalosema Nini maana na asili ya sadaka iitwayo malimbuko katika Kanisa Katoliki?
Fri, 25 Oct 2024 - 23min - 965 - Ni, kwanini Mfalme Suleiman aliomba Hekima?
Karibu uungane nami Esther Magai Hangu, katika kipindi cha Ujumbe wa Biblia, Leo nipo na Padre Titus Amigu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino SAUT Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, akiendelea kufundisha juu ya kukoseana na kusamehana akiwatazama Wafalme mbalimbali, leo anamzungumzia Mfalme Suleiman.
Fri, 25 Oct 2024 - 55min - 964 - Je, unafahamu mlango wa nyumba aminifu?
Karibu uungane nami John Samky katika kipindi cha Familia bora na nyumba aminifu, leo Wanafamilia bora wanaendelea kutufundisha juu ya mlango wa Familia na nyumba aminifu.
Thu, 24 Oct 2024 - 49min - 963 - Je, kwanini Yesu alibatizwa na tunafahamu hakuwa na dhambi?
Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, ambapo majibu yanatolewa na Frateri Baltazary Boa kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu Songea katika swali hili Binadamu tunapata Sakramenti ya Ubatizo kwa maondeleo ya dhambi ya asili, Je, kwanini Yesu alibatizwa na ni nasfi ya pili ya Mungu na tunafahamu hakuwa na dhambi?
Thu, 24 Oct 2024 - 16min
Podcasts similaires à Radio Maria Tanzania
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Espacio en blanco Radio Nacional
- Les Grosses Têtes RTL
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR
Autres podcasts de Religion et Spiritualité
- Joel Osteen Podcast Joel Osteen, SiriusXM
- Neno @ttb.twr.org/swahili Thru the Bible Swahili
- Tagebuch eines Pfarrers Pfarrer Hans Spiegl
- Mufti Menk Muslim Central
- المصحف المجود - محمد محمود الطبلاوي طريق الإسلام
- Unter Pfarrerstöchtern ZEIT ONLINE
- Apostle Joshua Selman Apostle Joshua Selman
- Reggae Revival Dread Lightning HiFi
- The Potter's Touch on Lightsource.com - Audio Bishop T.D. Jakes
- Osho Hindi Podcast Mahant Govind Das Swami
- Sex, Love & Relationship Podcast Joanna Intara
- Islam islamicinspiration
- Praise Worship Praise Worship
- Al Qasas Al Qasas
- Destiny Church Podcast Destiny Church
- Joyce Meyer Enjoying Everyday Life® Radio Podcast Joyce Meyer
- Songs for Worship Eric C. Rose
- The Gospel According to House Dj N-Joi
- Om Nama Shivaya - Shiva Mantra Chants recited by Sandeep Khurana Sandeep Khurana
- Spirit Unlocked Various