Filtrar por gênero
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
- 242 - Vijana pwani ya Kenya waachana na dawa za kulevya na kugeukia shughuli za kiuchumi
Msikilizaji kwa muda sasa, eneo la pwani ya Kenya limekuwa likikabiliwa na kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana, Hali hii ikichangia vitendo vya utovu wa nidhamu, kuongezeka kwa magonjwa ya zinaa na ndoa za mapema. Hata hivyo, kutokana na juhudi za mashirika mbalimbali ya kijamii na yasiyo ya kiserikali, vijana wengi walioacha kutumia dawa za kulevya sasa wanajihusisha na miradi ya kibiashara ili kujikimu.
Makala ua Gurudumu la Uchumi juma hili, inawaangazia vijana wa eneo la Pwani ambao wameamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.
Wed, 13 Nov 2024 - 241 - Sehemu ya pili: Je kuongeza kodi ni suluhu kwa matatizo ya Afrika
Msikilizaji kwa muda sasa mataifa ya Afrika yameendelea kupitia changamoto za kifedha, kuanzia katika kukusanya mapato na matumizi kwa ajili ya maendeleo yake, hali ambayo imesababisha nchi nyingi kujikuta pabaya kutokana na kulazimika kukopa fedha toka kwa taasisi za kimataifa au nchi zilizoendelea huku ziklipa riba kubwa katika urejeshaji.
Lakini je, kuongza kodi ndio suluhu? Mchambuzi wa masuala ya uchumi kutoka Tanzania, Ali Mkimo anafafanua.
Thu, 07 Nov 2024 - 240 - Je, nyongeza ya kodi ni suluhu kwa nchi zinazoendelea kujikwamua kiuchumi
Mataifa ya Afrika yameendelea kupitia changamoto za kifedha, katika kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo, hali ambayo imesababisha nchi nyingi kujikuta pabaya kutokana na kulazimika kukopa fedha toka kwa taasisi za kimataifa au nchi zilizoendelea huku ziklipa riba kubwa katika ureje shaji.
Lakini je, kuongeza wigo wa kodi kwa mataifa yanayoendelea ndio njia pekee kuwezesha mataifa haya kujikwamua kiuchumi? Tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tananzania
Wed, 30 Oct 2024 - 239 - Athari za Kiuchumi kutokana na ongezeko la watu barani Afrika: Changamoto na fursa
Msikilizaji dunia inashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu katika miongo 6 iliyopita, ambapo mwaka 1960 idadi ilikuwa bilioni 3 lakini katika miongo miwili tu hadi mwaka 1982 ilikuwa imevuka watu bilioni 5 na November mwaka 2022 kulikuwa na watu bilioni 8 duniani.
Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tunajadili Athari za Kiuchumi kutokana na ongezeko la watu barani Afrika: Changamoto na fursa.
Tumezungumza na Walter Nguma, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania
Wed, 09 Oct 2024 - 238 - Athari za utoroshaji na utakatishaji fedha barani Afrika
Tatizo la fedha haramu barani Afrika linaligharibu bara hili kiasi cha dola za Marekani bilioni 50 na bilioni 80 kila mwaka, Asilimia 44 ya utajiri wa kifedha wa Afrika inadhaniwa kuwa nje ya nchi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Uwazi wa Ushuru barani Afrika ya 2023, nchi za Afrika zimeokoa dola bilioni 2 kwa mwaka kutokana na watu kuweka wazi mapato yao, ubora wa kubadilishana taarifa na uchunguzi wa nje ya nchi.
Tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Wed, 02 Oct 2024 - 237 - Fursa na changamoto ya huduma jumuishi za mifumo ya kifedha kidijitali barani Afrika
Msikilizaji kwa mujibu wa benki ya dunia, ni asilimia 49 tu ya watu wazima wanamiliki akaunti benki, takwimu za hivi karibuni zikionesha ongezeko la asilimia 55 mwaka 2021 kutoka asilimia 43 mwaka 2017, hata hivyo kiwango hiki kikiwa kidogo ukilinganisha na wastani wa kidunia wa asilimia 76.
Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili tunajadili kuhusu huduma jumuishi za mifumo ya kifedha barani Afrika. Machambuzi wa masuala ya uchumi ALI MKIMO anajibu maswali kadhaa kuhusu sekta hii.
Wed, 18 Sep 2024 - 236 - Afrika na usalama wa chakula
Msikilizaji juma lililopita Rwanda ilikuwa mwenyeji wa kongamano la mfumo wa chakula barani Afrika, ambapo wadau zaidi ya elfu 4 kutoka kila pembe ya mataifa ya Afrika walishiriki.
Mkutano uliangazia kuhusu mifumo ya chakula, mbinu bora na teknolojia ambazo zinaweza kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula barani Afrika na wakati huohuo kutengeneza nafasi za kazi na fursa kwa wanawake.
Msikilizaji wiki hii nimeshirikiana na mwanahabari wetu wa Kigali, Christopher Karenzi;
Wed, 11 Sep 2024 - 235 - Ndio au hapana, mkutano kati ya Uchina na Afrika
Uchina wiki hii imekuwa mwenyeji wa mkutano kati yake na viongozi wa Afrika, kwa mujibu wa takwimu zilizoko, China ni taifa la pili duniani kufanya biashara nyingi zaidi na bara la Afrika, biashara inayokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 167 kwa mwaka.
Kuangazia mkutano huu na wasiwasi ulioko kuhusu uwekezaji wa China barani Afrika, tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.
Wed, 04 Sep 2024 - 234 - Athari za kutokuwa na usawa wa kijinsia kwa soko la ajira Afrika
Kwa wastani, wanawake hufanya angalau mara mbili na nusu zaidi ya kazi za nyumbani zisizo na malipo kuliko wanaume. Zaidi ya hayo, wanawake hutumia saa 4 na dakika 30 kwa siku kwa kazi ya matunzo bila malipo, ikilinganishwa na saa 1 dakika 20 kwa wanaume katika nchi zinazoendelea.
Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii tunajikita kule mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako baadhi ya wanawake kwenye mji wa Goma, sasa wanalazimika kuponda mawe kujikimu na familia zao.
Wed, 28 Aug 2024 - 233 - Tatizo la ajira na changamoto nyingine kwa vijana wa Afrika Mashariki
Msikilizaji asilimia 70 ya watu katika mataifa ya Afrika yaliyoko Kusini mwa Jangwa la Sahara wana umri wa chini ya miaka 30, hata hivyo ni hatari ikiwa mataifa yatashindwa kuhakikisha vijana wana nafasi nzuri za maisha, kwakuwa Vijana wana haki sio tu ya afya bora, lishe bora na elimu, lakini fursa za uhuru na kazi nzuri.
Kuzungumzia mada hii hivi leo, kwa njia ya simu nimemualika Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa nchini Tanzania.
Wed, 21 Aug 2024 - 232 - Ugunduzi wa tekonolojia ya akili mnemba teknolojia nyingine na mchango wake kwa ukuaji wa uchumi
Msikilizaji kwa mujibu wa Jukwaa la dunia la uchumi, World Economic Forum, ujio wa teknolojia mpya kama akili mnemba (Artuificial inteligency), ikiwa zitatumika vizuri, zitasaidia kujenga uchumi wenye ushindani, unaostahimili changamoto na endelevu.
Katika makala ya gurudumu la uchumi juma hili, tunajadili Kuibuka au ugunduzi wa teknolojia na ushawishi wake katika kukuza uchumi.
Wed, 26 Jun 2024 - 231 - Athari za uchumi na biashara kwenye mji wa Kalemie nchini DRC
Msikilizaji juma hili katika makala ya Gurudumu la uchumi nakuletea mseto wa taarifa za uchumi na biashara toka kwenye kanda ya Afrika Mashariki, katika Makala ya leo mwenzangu victor Abuso, alizungumza na Christian Yoka, mkurugenzi wa shirika la maendeleo la Ufaransa, AFD kanda ya Afrika, lakini pia mwandishi wetu wa Lubumbashi, Denise Mayoo, alizuru mji wa Kalemie nchini DRC ulioathirika pakubwa na mafuriko, ambako shughuli za biashara na uchimi zimeathiriwa pakubwa.
Wed, 12 Jun 2024 - 230 - Afrika iwe makini inaposhirikiana au kusaidiwa na nchi zilizoendelea
Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, mataifa ya Ulaya, Amerika, Asia na sasa Uarabuni, yameongeza kasi ya uwekezaji, utoaji wa mikopo na misaada kwa nchi za Afrika, mataifa haya yamewekeza mabilioni ya dola za marekani kwa bara hilo kwa kubadilishana na rasilimali zake, hatua ambayo mbali na kuonekana kama ni urafiki lakini inaibua maswali kuhusu nia hasa ya nchi hizo kwa bara la Afrika.
Ni juma hili tu, Korea Kusini kwa mara ya kwanza imefanya kongamano na viongozi wa Afrika, ambapo imetangaza msaada wad ola za marekani bilioni 10 kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na biashara kati yake na nchi hizo.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia kasi hii mpya ya nchi za magharibi kwa bara la Afrika, tukijiuliza maswali kadhaa, je nia yao ni safi? Na vipi Afrika inaweza kutumia fursa hii kujikwamua kiuchumi?
Wed, 05 Jun 2024 - 229 - Hofu kwa wafanyabiashara kuhusu muswada wa fedha 2024 nchini Kenya
Msikilizaji kwa wiki kadhaa sasa nchini Kenya, kumekuwa na mjadala mkali baada ya kutolewa kwa mapendekezo ya serikali kuhusu muswada wa fedha wa mwaka 2024 unaolenga kuongeza kodi katika baadhi ya sekta na bidhaa nchini humo.
Wazalishaji na wawekezaji wakitarajiwa kuwa waathiriwa wakbwa ikiwa muswada huu utapitishwa kama ulivyo, ambapo baadhi ya vinavyolalamikiwa na wazalishaji ni nyongeza ya ushuru wa thamani katika malighafi kutoka nje pamoja na tozo za mazingira maarufu kama Eco Levy.
Sekta ya uzalishaji wa viwanda inatarajiwa kuchangia asililia 20 katika pato ghafi la taifa hadi kufikia mwaka 2030.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, imezungumza na mwenyekiti wa shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, Antony Mwangi, kuangazia changamoto na faida za muswada huu.
Jina langu ni Emmanuel Makundi, karibu.
Msikilizaji nilianza kwa kumuuliza Antony, wao wanautazamaje muswada huu?
Insert ///
Msikilizaji kama umeungana nasi Makala ni Gurudumu la uchumi na leo tunaujadili muswada wa fedha nchini Kenya unaoelnga kuongeza ushuru wa bidhaa na wazalishaji, na tunazungumza na Antony Mwangi, mwenyekiti wa shirikisho la wazalishaji nchini Kenya.
Insert ///
Kufikia hapa ndio tunatia nanga ya Makala ya Gurudumu la uchumi kwa juma hili, shukrani kwa Antony Mwangi, mwenyekiti wa shirikishi la wazalishaji nchini Kenya, usikose kuungana nami katika makala nyingine wiki ijayo, ulikuwa nami Emmanuel Makundi, kwaheri.
Wed, 29 May 2024 - 228 - Afrika na jitihada za kutaka kuwa katika meza ya majadiliano ya kidunia na sio mualikwa
Msikilizaji wakati wa kongamano la kimataifa la wakurugenzi wakuu wa kampuni mbalimbali duniani waliokutana nchini Rwanda, maswali kadhaa yaliibuliwa, kubwa lilikuwa ni je bara la Afrika linapaswa kuwa katika meza ya maamuzi au kwenye orodha, na ikiwa huu ni muda muafaka wa kutoa mustakabali wake.
Ni maswali magumu ambayo hata hivyo viongozi wa Afrika walioshiriki, wanakubaliana kuwa bara hili lina rasilimali zakutosha kubadili uelekeo wake na maendeleo kwa raia, lakini pia halipaswi kuwa linaomba kwa viongozi wa magharibi kuwa katika meza ya majadiliano kuhusu mustakabali wa uchumi na maendeleo ya dunia.
Suala la mabadiliko ya tabia nchi na utekelezaji wa mkataba wa biashara huria wa bara hili, maarufu kama AfCFTA, liliibuka, ambapo licha ya utiwaji saini itifaki yake, bado kuna vikwazo vya kufanya biashara baina ya nchi za Afrika.
Wed, 22 May 2024 - 227 - Changamoto na fursa kwa vijana wajasiriamali na ajira kwenye nchi za Afrika Mashariki
Hujambo msikilizaji wa rfikiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu nikukaribishe katika makala ya Gurudumu la Uchumi, na hivi leo tunaangazia ukanda wa Afrika Mashariki, eneo lililojaa nguvu kazi ya vijana pamoja na ari ya ujasiriamali, lakini bado linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira.
Takwimu za hivi karibuni za benki ya dunia zinaonesha uhalisia wa tatizo, takwimu zikitofautiana baina ya nchi na nchi, lakini kiujumla ni kuanzia kati ya asilimia 4 hadi 19 ya vijana hawana ajira, huku wanawake walioko vijijini wakiwa waathirika wakubwa.
Katika makala haya hivi leo, tutaangazia kwa kina namna gani bora ya kukabiliana na tatizo la ajira na kuongeza wajasiriamali wengi zaidi kwenye ukanda.
Kwenye line ya simu nimewaalika, Ali Mkimo, yeye ni mchambuzi wa masuala ya Uchumi pamoja na Emmanuel Cosmas, kijana mbunifu wa masuala teknolojia na nibalozi wa UNICEF, wote hawa wakiwa nchini Tanzania.
Wed, 15 May 2024 - 226 - Mchango wa biashara ndogondogo na kati kwa uchumi wa nchi za Afrika MasharikiFri, 10 May 2024
- 225 - Afrika na madai ya mabadiliko katika mifumo ya kifedha ya kimataifa
Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, wito umeendelea kutolewa na mataifa ya Afrika kuhusu kuwepo usawa na haki katika mfumo wa kifedha duniani, ambao Kihistoria, nchi za Kiafrika zimekuwa katika hali mbaya linapokuja suala la kupata ufadhili, rasilimali, na makubaliano yenye usawa ya kibiashara.
Kuzungumzia hili, nimemualika kwa njia ya simu kutoka Tanzania, Walter Nguma, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara.
Wed, 01 May 2024 - 224 - Wataalamu: Uchumi Samawati utumiwe vizuri kwa maendeleo endelevu
Kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa bluu barani Afrika una uwezo wa kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya bara hilo.
Uchumi wa bluu unatajwa kuchangia dola za Marekani trilioni 1 kila mwaka, Sekta ya uvuvi ikiwa kitovu kikuu na kuajiri zaidi ya watu milioni 12.
Profesa Omary Mbura, mtaalamu na mhadhiri wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, anaangazia sekta hii.
Thu, 11 Apr 2024 - 223 - Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma
Shughuli za sekta binafsi na uwekezaji ni vyanzo vikuu ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na maendeleo endelevu.
Kwa wastani, sekta binafsi inachangia zaidi ya Asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa watu wa kipato cha chini na cha kati, kupitia kodi ya kampuni, kodi ya rasilimali na mapato ya kodi kwa wafanyakazi.
Sekta hii inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya ajira katika nchi zinazoendelea kiuchumi.
Mon, 04 Mar 2024 - 222 - Ukulima wa matunda Kenya na changamoto zakeMon, 04 Mar 2024
- 221 - Changamoto za uhamiaji na fursa zake kwa uchumi
Uhamiaji unaweza kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika ikiwa mtu anaweza kutoa mwelekeo bora wa fedha zinazotumwa na wageni kuelekea uwekezaji na ufadhili wa maendeleo katika nchi za Afrika.
Diasporas wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zetu ambazo kimsingi ni nchi za asili lakini pia nchi mwenyeji.
Wanafanya hivyo kwa kuhamisha pesa, ujuzi, teknolojia, mifano ya utawala, maadili, na mawazo. Serikali ya Senegal inafahamu mabadiliko yanayohitajika tunapojitahidi kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji Salama, Ulio na Utaratibu na wa Kawaida nchini Senegali.
Mon, 04 Mar 2024 - 220 - Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifuMon, 04 Mar 2024
- 219 - Mzozo kati ya Kenya na Tanzania kuhusu mashirika yake ya ndege
Msikilizaji, hatimaye nchi ya Tanzania imeondoa zuio ililoweka juma hili kwa ndege za shirika la Kenya KQ, uamuzi iliyokuwa imeuchukua baada ya Nairobi kukataa kutoa kibali kwa ndege za mizigo za shirika la Tanzania kushusha na kupakia kutokea Kenya.
Uamuzi huo msikilizaji ulisababisha mawaziri wa pande zote kukutana na Jumanne ya wiki hii wakakubaliana kumaliza tofauti zilizojitokeza na sasa safarai za ndege za Kenya na zile za Tanzania zitaruhusiwa.
Mon, 04 Mar 2024
Podcasts semelhantes a Gurudumu la Uchumi
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Affaires sensibles France Inter
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- Espacio en blanco Radio Nacional
- Les Grosses Têtes RTL
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- TED Talks Daily TED
- The Tucker Carlson Show Tucker Carlson Network
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR
Outros Podcasts de Negócio
- Tanguy Pastureau maltraite l'info France Inter
- Les experts BFM Business
- L'édito éco France Inter
- BFM Bourse BFM Business
- Riche d'Expériences Niko et Mehdi
- Entendez-vous l'éco ? France Culture
- Les Vraies Voix Sud Radio
- BFM Crypto Le Club BFM Business
- Culture IA BFM Business
- Libertad Inmobiliaria Carlos Galán
- On n'arrête pas l'éco France Inter
- La France bouge - Elisabeth Assayag Europe 1
- BFM Crypto, les Pros BFM Business
- La Productivité Décomplexée Sophie TAILLIEU
- Les Investisseurs Sereins - Investissement Immobilier Rentable Cyril & Dorine
- Outils du Manager Cedric Watine
- Culture d'entreprise. natif. I Grace Leplat
- Frankly Speaking Curzio Research
- All Ears English Podcast Lindsay McMahon and Michelle Kaplan
- Eduzzcast Eduzzcast