Filtrar por género

Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

RFI Kiswahili

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

242 - Vijana pwani ya Kenya waachana na dawa za kulevya na kugeukia shughuli za kiuchumi
0:00 / 0:00
1x
  • 242 - Vijana pwani ya Kenya waachana na dawa za kulevya na kugeukia shughuli za kiuchumi

    Msikilizaji kwa muda sasa, eneo la pwani ya Kenya limekuwa likikabiliwa na kiwango kikubwa cha matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana, Hali hii ikichangia vitendo vya utovu wa nidhamu, kuongezeka kwa magonjwa ya zinaa na ndoa za mapema. Hata hivyo, kutokana na juhudi za mashirika mbalimbali ya kijamii na yasiyo ya kiserikali, vijana wengi walioacha kutumia dawa za kulevya sasa wanajihusisha na miradi ya kibiashara ili kujikimu.

    Makala ua Gurudumu la Uchumi juma hili, inawaangazia vijana wa eneo la Pwani ambao wameamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

    Wed, 13 Nov 2024
  • 241 - Sehemu ya pili: Je kuongeza kodi ni suluhu kwa matatizo ya Afrika

    Msikilizaji kwa muda sasa mataifa ya Afrika yameendelea kupitia changamoto za kifedha, kuanzia katika kukusanya mapato na matumizi kwa ajili ya maendeleo yake, hali ambayo imesababisha nchi nyingi kujikuta pabaya kutokana na kulazimika kukopa fedha toka kwa taasisi za kimataifa au nchi zilizoendelea huku ziklipa riba kubwa katika urejeshaji.

    Lakini je, kuongza kodi ndio suluhu? Mchambuzi wa masuala ya uchumi kutoka Tanzania, Ali Mkimo anafafanua.

    Thu, 07 Nov 2024
  • 240 - Je, nyongeza ya kodi ni suluhu kwa nchi zinazoendelea kujikwamua kiuchumi

    Mataifa ya Afrika yameendelea kupitia changamoto za kifedha, katika kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo, hali ambayo imesababisha nchi nyingi kujikuta pabaya kutokana na kulazimika kukopa fedha toka kwa taasisi za kimataifa au nchi zilizoendelea huku ziklipa riba kubwa katika ureje shaji.

    Lakini je, kuongeza wigo wa kodi kwa mataifa yanayoendelea ndio njia pekee kuwezesha mataifa haya kujikwamua kiuchumi? Tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi na mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tananzania

    Wed, 30 Oct 2024
  • 239 - Athari za Kiuchumi kutokana na ongezeko la watu barani Afrika: Changamoto na fursa

    Msikilizaji dunia inashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu katika miongo 6 iliyopita, ambapo mwaka 1960 idadi ilikuwa bilioni 3 lakini katika miongo miwili tu hadi mwaka 1982 ilikuwa imevuka watu bilioni 5 na November mwaka 2022 kulikuwa na watu bilioni 8 duniani.

    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, tunajadili Athari za Kiuchumi kutokana na ongezeko la watu barani Afrika: Changamoto na fursa.

    Tumezungumza na Walter Nguma, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania

    Wed, 09 Oct 2024
  • 238 - Athari za utoroshaji na utakatishaji fedha barani Afrika

    Tatizo la fedha haramu barani Afrika linaligharibu bara hili kiasi cha dola za Marekani bilioni 50 na bilioni 80 kila mwaka, Asilimia 44 ya utajiri wa kifedha wa Afrika inadhaniwa kuwa nje ya nchi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Uwazi wa Ushuru barani Afrika ya 2023, nchi za Afrika zimeokoa dola bilioni 2 kwa mwaka kutokana na watu kuweka wazi mapato yao, ubora wa kubadilishana taarifa na uchunguzi wa nje ya nchi.

    Tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

    Wed, 02 Oct 2024
Mostrar más episodios